Kwa ngoma hii, Ney sasa umekua!

Kwa ngoma hii, Ney sasa umekua!

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Posts
1,691
Reaction score
640
Akiongea na DJ Nico Track(sharp shooter) wa Capital radio, Ney wa Mitego amesema hapendi kuona wanawake wakipigwa na wanaume. Katika wimbo wake mpya unaoitwa Mwanamke Hapigwi, jamaa amesema ametunga wimbo huo kutokana na maisha aliyopitia. Jamaa amesema alikuwa anashuhudia mama yake akipigwa na baba wa kambo, kitendo kilichomfanya awahi kuondoka nyumbani na kuanza kujitegemea.

Kiukweli Ney wa sasa sio Ney aliyekuwa anampenda sana demu wake kuliko anavyompenda mama yake! Katika hili mi nakupa big up sana bro.Hakika sasa umekuwa. Naamini pia huwezi tena kuwadis wabana pua, maana sina hakika siku hizi unafanya type gani ya music, coz tulizoea kuona unafanya hip hop.
 
kwakuwa huyo ni mama yake ni lazima aseme baba wa kambo alikuwa mkorofi, ninahitaji maoni ya baba wa kambo ili tubalance mambo
 
Unamsifia kabla hujaisikiliza ngoma yenyewe,title yake ndio imekuchanganya?

Nimeisikia mkuu. Ni Zouk fulani hivi. Ameimba tu, hajarap. Yeah, ni track nzuri tu, najua itauzika vizuri tu.
 
kwakuwa huyo ni mama yake ni lazima aseme baba wa kambo alikuwa mkorofi, ninahitaji maoni ya baba wa kambo ili tubalance mambo

Yeah, ni kweli. Huu ni ushahidi wa upande mmoja.
Ila kwa jinsi alivyoanza, mi na mpongeza kwa idea hii aliyoitoa. Mkuu ukisikiliza wimbo ule, utakubaliana na mimi kuwa jamaa kweli amekua.
 
Back
Top Bottom