Kwa nia njema kabisa tuachane na kuhamia Dodoma kwa sasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuhamia Dodoma ni ndoto yetu ya siku nyingi sana, lakini sio kipaumbele kutokana na hali yetu ya sasa ya kiuchumi.

Kama tukiyaorodhesha matatizo yetu yanayokwamishwa na ukosefu wa fedha kwa kufuata umuhimu na uharaka wake kuhamia Dodoma haitakuwemo kwenye top 100 ya shida hizo.

Jamani Tanzania ni yetu na Dodoma ni yetu wote bila kujali vyama vyetu. Hebu tuwekeze kodi zetu kwa sasa katika kujenga miundombinu, kukusanya kodi, na kuboresha maisha ya wananchi wetu kwanza.
 
Wazo lako ni zuri, ila kwa sasa umechelewa kwani tayari karibu wizara zote watumishi wamehamia na wamelipwa stahiki zao. Kutengua tena uamuzi huo manake walipwe tena kurudi Dar! Ndo uchumi huo?
 
Wazo lako ni zuri, ila kwa sasa umechelewa kwani tayari karibu wizara zote watumishi wamehamia na wamelipwa stahiki zao. Kutengua tena uamuzi huo manake walipwe tena kurudi Dar! Ndo uchumi huo?
Tupige tu hesabu tuone kama zilizotumika ni nyingi kuliko tutakazohitaji kutumia kukamilisha mission nzima. Hata hao unaosema wamehamia hata familia zao bado ziko DSM hivyo kila wikiend wako DSM

Je, unadhani tunahitaji sh ngapi kuhamishia Dodoma Rais wetu?
 
Dar wameinjoy Sana maisha toka uhuru, wacha nao wakina Matonya wafurahia uhuru wa nchi yao.
 
Mkuu, wazo lako ni zuri, lkn huku jukwaa la Biashara ulipoliweka siko, ni sawa na kwenda kuuza sigara Kanisani kwa walokole. Hili bandiko ungeweka kule jukwaa la siasa ambako wachambuzi wa mambo kama haya wamejaa tele kungekuwa na mjadala wenye tija
 
Kweli angeliweka kwa siasa, lakini msaidie huenda akawa sawa Mada mchanyiko, kila siku tunaishi ni siasa
 
Mkuu, wazo lako ni zuri, lkn huku jukwaa la Biashara ulipoliweka siko, ni sawa na kwenda kuuza sigara Kanisani kwa walokole. Hili bandiko ungeweka kule jukwaa la siasa ambako wachambuzi wa mambo kama haya wamejaa tele kungekuwa na mjadala wenye tija
Sio suala la kisiasa hili ni suala la kiuchumi zaidi. Ningeliweka kule kwenye siasa ningeambiwa chadema au mpinga ilani, lakini uchumi hauna chama.

Hata Mwl. Nyerere alishindwa kuhamia Dodoma kutokana na ughali wake. Kuhamia huko ni luxuary ambayo ingesubiri kila kijiji kiwe na maji ya bomba, umeme, shule, kituo cha police, trekta la kulimia, zahanati, barabara, soko la mazao yao, majosho ya mifugo yao, nk
 
kila weekend wapo dar kwa nauli zao... sio kwa gharama ya serikali
 
hivi jengo la ikulu huko dodoma limefikia hatua gani?
 
kila weekend wapo dar kwa nauli zao... sio kwa gharama ya serikali
Ukiwa Moro Friday jioni nenda pale samaki samaki, tena sasa hivi kuna balcony, nenda kaa juu wakati unapata Serengeti yako au Windhoek check mashangingi (STK, STL....) from Dom yaki rally to Dar.....
 
Kichaa kasema hapangiwi lazima ahamie Dodoma ,kichaa mwenzake wa Home affair keshahamia tayari
 
Endelea kuota mchana kweupe sisi tunasonga mbele! Kama ni kusubiri mbona tumesubiri sana zaidi ya miaka 40.
 
Ukiwa Moro Friday jioni nenda pale samaki samaki, tena sasa hivi kuna balcony, nenda kaa juu wakati unapata Serengeti yako au Windhoek check mashangingi (STK, STL....) from Dom yaki rally to Dar.....
Sio wanarudi baada ya kuhudhuria vikao vya bunge??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…