Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Kwa niliyoyaona Burundi, itoshe kusema Tanzania ni nchi tajiri sana

Aliemzika Yesu alikua ni Tajiri wa Kutupwa masikini walishindwa kumzika Yesu sababu ya Gharama za Mazishi hazikua ndogo na hata kaburi lake lilikua la Nyota 5 sio makaburi ya kapuku km lile alilomfufua Razaro

Yesu pia kuna pahala anawasimulia wanafunzi na makutano juu ya mtu alievamiwa na majambazi na kujeruhiwa vibaya Ila walipita watu wa kanisa wakuu wa Makuhani wakapita kando, walipita wazee wa Busara wakapita kando wasimsaidie Ila akapita Tajiri mmoja akiwa na punda zake akamsaidia kwa kumpa huduma ya kwanza majeraha yake na pia akampeleka hotelini akalipia apewe matibabu hadi pale atakapopona, yaan Tajiri alilipa gharama zote jamaa atibiwe mpaka apone pamoja na kwamba alikua hamjui ilihali masikini walimkimbia jamaa hawakumuokoa sababu ya kukimbia gharama

Umeelewa maana ya hio hadithi ilimaanisha nini ?
Imemaanisha kwamba tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu Ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu ya sindano!
 
Imemaanisha kwamba tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu Ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu ya sindano!
Yea baba that's how it's Ila watu wamemeza matango pori wakahisi utajiri ni mbaya, Ila in reality utajiri sio mbaya, tajiri kuingia kwenye ufalme wa Mungu ni sawa sawa na ngamia kupenye kwenye tundu la sindano
 
Kuna Jiji linaitwa Kinshasa huko sio pa kitoto barabara zake bongo hakuna popote
Kusema Kinshasa ni zaid ya dar ni either huijui dar au huijui Kinshasa.
kilichokuchanganya ni hyo inaitwa Gombe avenue,Kinshasa ni mji mkubwa saana na kuna watu wengi saana ila kimaendeleo haipasogelei dar hata kidogo,umeme tu ni mtihani mji mzima umejaa majenereta kama Lagos,watu ni masikin mno,hakuna maajabu kabisa matajiri wachache hujichimbia kwenye exclusive gated community kama mount-fleury, karibia matajiri wote wa congo ndo wanaishi hapo ila the rest Kinshasa ni ya kawaida mno imezidiwa saana na dar es salaam.Ligi ya dar ni Nairobi tu hyo miji mingine haitoboi.
 
Wewe hujasoma historia ya Africa, are you serious? Ndiyo maana wasomi wanasema siku zote achaneni na hizi dini za kuletewa maana zinawaharibu Waafrika akili kuaminishwa vitu visivyo na vichwa na kudharau historia yetu.
Daaah Yaani ulivyo ni quote kama vile una hakika nimeenda shule, basi bana nilitaka kujua tu . Yaishe mkuu
 
Unaota kumbe..Ethiopia iizidi Kenya??

sijaandika hilo nikiwa na mahaba ya Shakahola kama wewe. soma mwenye hapa chini.​

Nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika mwaka 2016​

Ramani ya Afrika

CHANZO CHA PICHA,WORLD BANK
26 Julai 2022
Bara la Afrika linatajwa kuwa maskini zaidi duniani, huku umaskini wa bara hilo ukichangiwa na hali ya uchumi kuyumba, ukosefu wa usalama, ufisadi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na vitendo vya kigaidi katika bara hilo.
Shirika la Fedha Duniani IMF na Benki ya Dunia, katika ripoti ya pamoja iliyochapishwa mwishoni mwa 2021, zimetangaza nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika.

1. Misri​

Mji wa Cairo

Misri imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ukuaji wa juu wa uchumi kulingana na ripoti hiyo.
Mapato ya kila mwaka ya Misri ni $1.38 trilioni.
Misri ina jumla ya watu milioni 102, na nchi hiyo inategemea kilimo, uchimbaji madini na utalii.

2. Nigeria​

Mji wa Nigeria

Nigeria, ambayo ni ya pili kwa utajiri barani Afrika, ina pato la taifa la dola trilioni 1.14. Nigeria ina jumla ya watu milioni 206.1, ikiifanya kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Afrika Uchumi wa Nigeria unategemea mafuta na kilimo.

3. Afrika Kusini​

Afrika Kusini

Afrika Kusini, ambayo ni nchi tajiri zaidi barani Afrika, inaorodheshwa ya tatu ikiwa na pato la taifa (GDP), inayofikia dola bilioni 861.93 kwa mwaka.
Nchi hiyo ina watu 59,899,576, uchumi wake unategemea madini , hususan dhahabu na mali asili nyingine.

4. Algeria​

Algeria

Algeria ni nchi ya tatu tajiri zaidi barani Afrika, na pato la taifa (GDP) ni dola bilioni 532.57.
Nchi hiyo ina watu 44,911,520 na uchumi wake unategemea mafuta na gesi asilia inayouzwa nje ya nchi.

5. Morocco​

Morocco

Morocco, ambayo iko Afrika Kaskazini na inashikilia nafasi ya nne kati ya nchi 10 tajiri zaidi barani Afrika na Pato la Taifa (GDP) la nchi hiyo ni dola bilioni 302.77.
Nchi hiyo ina wakazi 37,462,423 na uchumi wake unategemea kilimo, madini na utalii.

6. Ethiopia​

Ehiopia

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Ethiopia, ambayo iko Afrika Mashariki na kushika nafasi ya sita kati ya nchi tajiri zaidi barani Afrika, ina Pato la Taifa la $298.57 bilioni kwa mwaka.
Ethiopia ina wakazi milioni 115 na uchumi wake unategemea Kilimo .

7. Kenya​

Nairobi Kenya

CHANZO CHA PICHA,NATIONALGEOGRAPHY
Kenya, ambayo inapatikana eneo la Afrika Mashariki na imeorodheshwa ya saba miongoni mwa kumi tajiri zaidi barani Afrika, ina Pato la Taifa la kila mwaka la $269.29 bilioni.

Kenya ina watu 54,039,625, na uchumi wake unategemea kilimo, utalii na biashara.
Angola

CHANZO CHA PICHA,COVER THE WIKI

8. Angola​

Angola, ambayo iko eneo la kati mwa Afrika, inaorodheshwa ya nane miongoni mwa nchi kumi tajiri zaidi barani Afrika. Ina Pato la Taifa la kila mwaka la bilioni 217.97 za Kimarekani.
Angola ina jumla ya watu 35,601,398, na uchumi wake unategemea mafuta na madini.

9. Ghana​

Ghana

CHANZO CHA PICHA,WIKIPEDIA
Ghana, ambayo ipo magharibi mwa Afrika inaorodheshwa ya tisa miongoni mwa nchi 10 tajiri zaidi katika bara la Afrika ina jumla ya pato la dola bilioni 193.63 kwa mwaka.
Ghana ina watu 33,483,283, na uchumi wake unategema uzalishaji wa viwanda kama vili teknolojia na uchukuzi.

10. Sudan​

Sudan

CHANZO CHA PICHA,AFP
Hatimaye, Sudan, ambayo ipo katika eneo la Afrika Mashariki, inaorodheshwa ya 10 miongoni mwa nchi tajiri barani Afrika, ikiwa na pato la taifa la dola bilioni 189.87 za Kimarekani kwa mwaka.
Sudan ina watu 46,888,316, na uchumi wake unategemea mafuta na kilimo.
Ripoti hiyo ilisema kuwa bara la Afrika lina mali asili nyingi, lakini nchi katika bara hilo zinatumia mali hizo kuzua vita, ufisadi na misukosuko ya kisiasa ambayo imechangia masuala haya.
 
Wabongo bana, kila mkikaribishwa kwenye nchi za watu mnakusanya mabaya tu.

Na ndio maana Waafrika tuna kasoro kubwa sana, badala utumie nguvu zote hizi kuainisha au kuorodhesha fursa ambazo wenzako wanaweza wakaja Burundi kuzichangamkia, wewe muda wote umetafuta mabaya tu.
Umenena vyema kuna shida kwenye vichwa vya baadhi ya wabongo , unashangaa ya Burundi wakati Dar tu watu hawali milo mitatu
 
Kusema Kinshasa ni zaid ya dar ni either huijui dar au huijui Kinshasa.
kilichokuchanganya ni hyo inaitwa Gombe avenue,Kinshasa ni mji mkubwa saana na kuna watu wengi saana ila kimaendeleo haipasogelei dar hata kidogo,umeme tu ni mtihani mji mzima umejaa majenereta kama Lagos,watu ni masikin mno,hakuna maajabu kabisa matajiri wachache hujichimbia kwenye exclusive gated community kama mount-fleury, karibia matajiri wote wa congo ndo wanaishi hapo ila the rest Kinshasa ni ya kawaida mno imezidiwa saana na dar es salaam.Ligi ya dar ni Nairobi tu hyo miji mingine haitoboi.
Hata Nairobi ni ndogo kuliko dar ila imejengekq mno kuliko dar
 
Rwanda ni kweli kabisa, wanajibrand tu ila kiukweli bado wako nyuma sana. Hapo kigali penyewe wanapopasifia ni ka sehemu kadogo tu hata Kariakoo kubwa. Nenda toka huko vijijini pamechoka sana watu maskini wa kutupa. Tusibeze bongo, tupo vizuri sana wakuu.West Africa ni mijini tu, vijijini na miji ya nje pako hoi. Mie naona kwa East Afrika tukiangalia kwa ujumla wake vijijini na mijini. Bongo ni namba 1 kwa hali nzuri. Ni mawazo yangu hayo.
Uganda hawana miji yao sio mikubwa ila vijijini watu wana maisha mazuri sana waganda wanajua kutafuta pesa

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Salum Bitchuka! Muasisi wa Taifa la Burundi! ( wapigania Uhuru )

Alafu kuna Mtanzania ndio aliyeandika Barua ya Kuomba Uhuru wa Burundi ntaambatanisha picha zao muda si Mrefu
 
Nakubaliana na wewe hakukua na dini inaitwa ukristo kabisaa.Hiz ni mambo tukajianzishia wenyewe tu.Kulikua na wafuasi wa kristo so hata leo wanaweza wakawepo wafuas wa kristo na wasiambatane na ma kanuni ya hii dini
Lakini neno, "kristo', maana yake ni," mfalme " japo lipo kigiriki,,
Kiyahudi wakati wako chini ya warumi,, walikua wakisubiri huyo mfalme,, aje awakomboe toka kwa mkoloni Mrumi,,
Masihi wa kwanza wa wayahudi alikua ni mfalme wa Persia,, King cyrus, ambae aliwakomboa wayahudi toka utumwani Babel, na kuwarudisha caanan,
Wakati wa yesu,, wayahudi walikuwa wanatawaliwa na warumi,, hivyo walikuwa wakitegemea ujaji wa masihi mwingine aje awakomboe toka utawala wa kikoloni,
Yesu alipokua, alianzisha hizo harakati, akijiita yeye ndo masihi,, Mfalme wa wayahudi,,
Na pia akajisema anatoka ukoo wa mfalme Daud,, hivyo anakidhi vigezo vya kuwa masihi na mfalme wa uyahudi,
 
Kwenye "kusaka tonge" Nimejikuta mara kadhaa nadondokea kwenye nchi jirani ila hii nchi ya BURUNDI inanifanya kila siku nizidi kuthamini na kuipenda TZ..Burundi ni nchi ambayo imepitiwa na Bonde la UFA "Rift valley" sasa sijui ni geographical area ndo inasababisha umaskini huu au ni nini? Lakini mbona Rwanda Nao ni nchi ndogo tena walikua Level moja kiuchumi miaka kadhaa ila Leo Rwanda iko mbali sana.

MIUNDOMBINU:
Barabara ya TZ ni nyembamba ila ya Burundi ni nyembamba Pro max na inamabonde,Mashimo,Kona na miinuko ya kufa mtu.Ajali ni kila siku tena zinaua kuliko za bongo.Mbaya zaidi wanatumia protocol ya barabara(Left na Right) kinyume na hii yetu hali ya kuwa magari mengi ni (Right hand)Kwaio kuovertake mpama utokeze mzimamzima kuchungulia hapo ndo msala unaanzia.kifuatacho ni INNALILLAH..BWANA ALITWAA..RIP

USAFIRI:
Burundi inamikoa zaidi ya 7 ila Airport iko moja tu nchi nzima (BUJUMBURA tu)..Usafiri wao sanasana ni TAX(probox mchomoko) bodaboda na Baiskeli ndo za Kumwagaa....!!!

MAMBO YANAYONISHANGAZA:

~Sio waislamu wala christians Burundi watu ni wafia dini yani wanajua na wanapenda dini balaa makanisani panajaa miskitini panajaa.Naamini dini zetu zinachangia pakubwa sana kwenye umaskini hapa Mzungu na Mwarabu walituweza washenzi wale...!!!

~Elimu HONGERA kwa Sekta ya Elimu ya TZ japo mtaala ni mbovu ila kwenye uniform TZ ilipatia sana..Haiwezekani wanafunzi wa Burundi sketi hazijawekewa Marinda yani zinachora shepu na vitoto vya sikuizi miaka 14 tu shape hiyoo.Watu kama KENGE tunapata tabu sana Wakuu..pia hata KENYA vyanafunzi vinavaa sketi fupi mno sijajua kwa UG na Rwanda.

Burundi wanapata sana Scholarship za France kwakua ni Colon lao..Elimu ni kuanzia la kwanza mpaka 13-16...

~Burundi hakuna Vivutio vya Utalii wala Mbuga za wanyama.Cha zaidi ni (Game reserve) Kinachoniuma kwenye Geography tulisoma Maeneo yaliyopitiwa na Rift valley yanaasilimia kubwa kutoa milima mirefu kama Oldonyo Lengai,Everest n.k Lakini kwa Burundi Hakuna Mlima hata mmoja wa kivutia cha utalii licha ya kuwa na miinuko,Mabonde nchi nzima

Cha kusikitisha kuna Ziwa Tanganyika ila Hakuna Mamlaka ya maji kama DAWASCO kwa TZ yaani kifupi kuna mgao wa maji hasa kule RUMONGE mkoa mzima umepakana na Ziwa ila kuna shida kubwa sana ya Maji Umeme ndo usiulize.

Mziki wanasikiliza wa TZ na Maeneo kama Rumonge wanaongea kiswaili vzuri kabsa ila Bujumbura ndo kuna baadhi wanaelewa kiswahili licha ya kuwa lugha mama ni Kirundi lakini asilimia kama zote wanabonga Kiswahili

Burundi ni nchi pekee unayoweza kusema wewe ni Tanzanian na wakakushobokea..Yaani pamoja na kwamba Nina ngozi ngumu kama ya KENGE na Sura mbaya kama Lori la Mchele kule Mbeya...Lakini huku kwa warundi nikisema tu mimi M-TZ basi watoto wananishobokea balaa kiasi kwamba wanavuka mpaka na kuniita (Hensam boi) Hapa ndo nikashtuka..Nenda Kenya sasa Useme wwe ni m-bongo uone wanavyokudharau...!!

Pia,Nilichogundua Bongo machokoraa wa stendi ni wasafi kulinganisha na wa Burund...Choko wa Burundi wanajua kuomba aisee hawakuachi na ni vichafu kinoma ukijumlisha Udongo ni mwekundu maeneo mengi basi vinakua vichafuu,,vyeusii..Mungu atuepushe na Umaskini aisee lakini Awezi kutuepusha kama sisi wenyewe tumebweteka kusubiri wazungu watutengenezee kila kitu.

Vilevile Ukitembea jiji zima hakuna nyumba iliotengenezwa kwa Tofali za Block..ni mwendo wa (Tofali za Choma)

Nchi kama hizi Chakula sio shida kwasababu uti wa uchumi wetu ni Kilimo kwaiyo vilevile Burundi Wanakima kila kitu na Kufuga kwaio nyama na Maziwa ni kama zote..Wana Ugali wao wa Roi umetengenezwa kwa Mihogo bongo inabidi tuutumie ni mzuri kwa Afya japo ukiskia unavyotengenezwa unaweza kuhairisha/Kususa kula..

View attachment 2606757
~VYUO VIKUU vinapatikana Bujumbura tu
~AIRPORT ni moja tu nchi nzima
~FARANGA haina thamani kabsaa ukichange 100k Tsh kuwa Faranga wewe ni taita..
~Kama wabongo tu wanaamini South kwa Madiba ndo kuna Maisha yani ukifika umetoboa..
~Maeneo mengi vijijini gari likipita wanalishangaa wakubwa kwa watoto

Pamoja na yote BURUNDI wanazaliana balaa sio ajabu kukuta Mzee anawake wawili na kila Mke anawatoto 10+ nafkir ni kwasababuSTAREHE YA MASKINI NI KUDINYANA

Fursa za Ajira kwa wabongo ukija ukosi kabsaa yani kama unataka utoboe mapema ujenge mapema nenda Burundi kama unaakili ya pesa utapiga sana kwasababu bado wako nyuma ya muda

Narudi kuendelea,bado nipo bujumbura
View attachment 2606756
Hakuna wale mademu warefu kama Rwanda? Ninachofurahi, nimefarijika kusikia kuna mtu anaitwa Nywandi. Nilikutana naye Bukoba mtu kama huyo miaka ya 70.
 
Utajiri sio kua namba ngapi kuna matajiri wengi wanaowazidi wale walio kwenye namba ndio maana mganga hukupeleka makaburini akakuague maana anajua Nafsi na Roho zenye utajiri mwingi zipo pale makaburini kuliko sehemu nyingine yoyote, akili yako ndio utajiri wako, sasa unaitumiaje akili yako ili uwe tajiri kuendana na akili yako hapo ndio kwenye puzzle

Nimekwambia utajiri wangu ni Maarifa yangu niliyonayo, utajiri namba moja ni kuwaongopea masikini wasio na Maarifa kwa kupitia Maarifa uliyonayo, good example wanasiasa au niseme wafanyabiashara za kisiasa, wanatumia Maarifa waliyonayo ya kisiasa kuwaadaa masikini wasiojua masuala ya kisiasa kujiingizia kipato na kutajirika

Una swali lingine uliza uwanja ni wako
Nitakuuliza siku ukijua nini maana ya neno tajiri
 
Hujamuelewa, anasema wanatumia mda mwingi kwenye ibada kuliko kufanya kazi na kuzalisha, pia wanaamini watatoka umaskinini kwa miujiza badala ya mipango na facts.

Bongo tunanafuu kuliko burudi sababu ya siasa safi kama raslimali zingekuwa dili congo ingekuwa tajiri sana so siasa ndo msingi wa kujenga au kubomoa
Robo tatu ya watanzania hawafuati dini kabisa ndio kusema ni matajiri?
 
Mzee wewe itakua Mrundi au Muha kwasababu ni mbishi alaf unachobishia huna maarifa nacho hata punje...Hakuna sehemu ugali wa Roe unasongwa kwa unga...!!
mihogo inachemshwa,Ikikauka inapondwa na kuanikwa.inachemshwa tena na kubumba ugali..Sasa process zote kwa mfano ukiona sehemu wanapoutwanga au ile Migomba ya kufunikia haina uchafu??

Hujui kitu we mrundi
Kitendo cha kusafiri na ugali ni uchafu tosha
 
Back
Top Bottom