Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Maskini wazee wa matusi na makasiriko wasiopenda kuambiwa ukweli watakuja kunisemanga lakini ukweli utabaki palepale.
Haiwezekani eti account inasoma positive ukanyang'anyane siti kwenye daladala. Haiwezekani account inasoma positive ukakae kwenye siti ya daladala huku chini umewekewa ndoo ya samaki yenye shombo.
Mama mmoja namfahamu alikuwa mama nitilie alikufa kwa kukanyagwa na tairi ya daladala Gongolamboto wakati akigombea usafiri.
Wengine wanajiona wajanja wanageuka na siti. Mtu mwenye ufahamu kidogo kichwani huwa anathamini muda kuliko hata fedha, sasa muda wa kuzungushwa huko kisha unarudishwa unakokwenda ni wastage of time na umaskini wa fikra.
Kwa vyovyote vile daladala hapa Tanzania ni usafiri wa kimaskini . Usifananishe public transport ya SA au UK na na hapa Dar es Salaam.
Jitahidi ununue gari, pikipiki au baiskeli utumie kama mbadala wa daladala.