Kwa nini ajira za TRA zinakiuka kanuni za utumishi? Je, wako juu ya sheria?

shinji

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2013
Posts
263
Reaction score
186
Amani iwe nanyi!

Ajira zote za serikali husimamiwa na Sekretarieti ya Ajira, ambapo baada ya mchakato kukamilika, majina ya waliopangiwa vituo hutolewa katika tovuti ili kila mmoja kuona.

Hii imekuwa tofauti kwa TRA, ambao walianza vizuri kwa kutoa majina ya walioitwa kwenye usaili. Cha ajabu ni kwamba majina ya walioitwa kazini wamewatumia wahusika kwa njia ya anwanipepe.

Ninaiuliza serikali, je, TRA wao wako juu ya sheria?
Ni nini kinafichwa katika taifa hili lenye AMANI?
Au, kuna majina yatashitua watu?
Au walioajiriwa si wale waliofanya usaili?
Au ni AMRI kutoka juu?

Naomba serikali na TRA watoe majibu kwa Watanzania.

Ama waseme kwamba Sekretarieti ya Ajira haina mamlaka kusimamia ajira za Taasisi zenye mishahara minono kama TRA hadi majina ya waliopata kufichwa.

Hili si HAKI na linaitia doa serikali.
 
Itakuwa ni utaratibu wao tu. Pia kuna taasisi kama GBT na TCRA zilipoajiri hakuna sehemu yoyote majina ya walioitwa kazini yalikuwa published. Kuna ulakini.

Juzi kati tu hapo, BOT waliajiri na majina yaliwekwa mtandaoni.
 
Gbt mshaajiriwa kumbe?
Tcra mbona huwa wanapitia utumishi?
 
Gbt mshaajiriwa kumbe?
Tcra mbona huwa wanapitia utumishi?
Watu tayari wapo kazini mkuu. Sasa hivi wananipigia simu nikawafungie madishi ya DSTV na AZAM. TCRA wanapitia utumishi ila majina ya walioitwa kazini hayakuwekwa kwenye website. Nao wapo kazini tangu Mwezi February.
 
Labda wana operate kama usalama wa taifa. Kuna mtu amewahi kuona recruitment process ya Tiss ?
Itakuwa ni utaratibu wao tu. Pia kuna taasisi kama GBT na TCRA zilipoajiri hakuna sehemu yoyote majina ya walioitwa kazini yalikuwa published. Kuna ulakini.

Juzi kati tu hapo, BOT waliajiri na majina yaliwekwa mtandaoni.
a wab
 
BOT wanapitia psrs mkuu.
 
Back
Top Bottom