Kwa nini Angela Kizigha asijitokeze kujitetea mwenyewe?

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Angela Kizigha.png

Tangu Rais Samia alipomteua Angela Kizigha kuwa Mbunge Aprili 2, 2026 kumekuwa na maneno mengi mno kuhusu mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EALA).

Chanzo cha maneno hayo ni tuhuma zinazomkabili Kizigha za kutokamilisha tenda ya ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi, ambapo ilibainika kuwa sare hizo hazikuletwa.

Suala hilo liligusiwa na Hayati Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza katika Ikulu ya Dar es Salaam Julai 18, 2016, akisema kuna mtu amelipwa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta sare za Jeshi la Polisi, lakini hazikuletwa na akautaka uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ufuatilie.

Kupitia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2018 ilibainika kuwa kampuni ya Daissy General Traders alipewa zaidi ya Sh16.66 bilioni lakini hakuleta sare hizo.

Ukaguzi wa CAG ulibaini, kuwa maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hayakuzingatiwa na malipo ya Sare za Polisi ambazo hazikuletwa kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi Sh.16,660,000,000 hazikurejeshwa.

Pia Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo, ikiwemo hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), hati ya madai kutoka kwa mtengenezaji (Commercial Invoice), hati ya mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha
za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika zililetwa nchini.
1756863116598.jpg

Kwa mujibu wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, Angela Kizigha aliyekuwa amegombea ubunge Kawe Dar es Salaam mwaka 2020, alienguliwa kwenye ushindani huo na Rais John Magufuli, akitoa sababu hiyo hiyo ya upotevu wa fedha za sare za polisi na alisema watamshitaki.

Hata hivyo, Polepole alishangazwa na ukaribu wa Kizigha na Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya kifo cha Magufuli na hatimaye akawa mtu wake wa karibu.

Kizigha alikuwa mtu wa karibu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 na hatimaye sasa ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Tangu zilipoibuka kashfa za upotevu wa fedha kwa ajili ya sare za polisi, Angela Kizigha hajawahi kujitokeza hadharani akakanusha, wala pengine kuchukua hatua za kisheria kusafisha jina lake.

Kama hiyo kashfa ni ya uongo au kusingiziwa, tungetarajia kumwona akikanusha hadharani au pengine hata chama chake kumshafisha kwamba hahusiki. Lakini suala hilo lilifinyangwa finyangwa baada ya kifo cha Magufuli na hatimaye sasa Kizigha ni mtu wa karibu na rais.

Badala yake sasa wanaibuka chawa kumtetea Kizigha. Wengine wanasema ametokea katika familia ya kiukombozi iliyomsaidia Baba wa Taifa Julius Nyerere alipotaka kuuawa. Kwamba baba yake Kizigha (Charles Kizigha) ndiye aliyefichua njama za kuuawa Nyerere na kufanikisha kukamatwa kwao.

Sasa hata kama ametokea kwenye failia hiyo, inahusikaje na kashfa iliyoko mbele yake? Kwamba mtu akitoka kwenye familia ya ukombozi, basi yuko huru kufanya ufisadi?

Wapo wengine wanasema licha ya Magufuli kutaja kashfa ya ununuzi wa sare za polisi, lakini hakukuwa na uthibitisho. Kama ni hivyo, mbona walikaa kimya bila kujisafisha. Kama kuna uchunguzi ulifanywa na kubaini kwamba Kizigha hana hatia, kwa nini haukuwekwa wazi.

Nimewaita hao watetezi wa Kizigha kuwa ni chawa, kwa sababu wanatetea kitu kisichowahusu. Kama ni kosa anatuhumiwa Kizigha, basi yeye mwenyewe ajitokeze ajitetetee, sio kutuma vibataka wa kumtetea mitandaoni.
Kwa upande mwingine, Rais Samia aliyemteua naye alipaswa kufafanua suala hilo, lakini kama atakaa kimya, basi kuna kitu hakipo sawa.
 
Hakuna chochote cha kufanywa hata asipojitokeza, hana cha kupoteza kwa hiyo ndio maana anawaacha nyie mpige kelele tu mpake mchoke.
 
View attachment 3569282
Tangu Rais Samia alipomteua Angela Kizigha kuwa Mbunge Aprili 2, 2026 kumekuwa na maneno mengi mno kuhusu mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EALA).

Chanzo cha maneno hayo ni tuhuma zinazomkabili Kizigha za kutokamilisha tenda ya ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi, ambapo ilibainika kuwa sare hizo hazikuletwa.

Suala hilo liligusiwa na Hayati Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza katika Ikulu ya Dar es Salaam Julai 18, 2016, akisema kuna mtu amelipwa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta sare za Jeshi la Polisi, lakini hazikuletwa na akautaka uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ufuatilie.

View attachment 3569289

Kupitia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2018 ilibainika kuwa kampuni ya Daissy General Traders alipewa zaidi ya Sh16.66 bilioni lakini hakuleta sare hizo.

Ukaguzi wa CAG ulibaini, kuwa maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hayakuzingatiwa na malipo ya Sare za Polisi ambazo hazikuletwa kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi Sh.16,660,000,000 hazikurejeshwa.

Pia Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo, ikiwemo hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), hati ya madai kutoka kwa mtengenezaji (Commercial Invoice), hati ya mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha
za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika zililetwa nchini.
View attachment 3569290

Angela Kizigha ni untouchable kwa utawala huu, watu aliokula nao hizo pesa za tenda ya sare za polisi ndiyo haohao walioshirikiana kumuua Mwendazake, ndiyo timu hiyohiyo iliyopanga na kufanya massacre ya MO29 so you can see how deeply secretive their cult is.
 
Samia anatudharau sana Watanganyika, hivi kweli CCM walikosa mgombea mwanaume Mtanganyika kuwa Rais wa Tanganyika hadi kutuwekea huyu mwanamke toka nchi jirani ya Zanzibar? Haya ni matusi makubwa sana kwa Tanganyika.
 
Kwa mtu anayewajua watanzania, hawezi kupoteza muda kujibu hisia za watu

"unapokuwa safarini, usipoteze muda wako kumrushia mawe kila mbwa anayekubwekea, kuna wengne wanabweka ili ujue kuwa hapo kuna mbwa"

Mwenye ushahidi atangulie mahakamani mkahojiane huko kizimbani
-utasikia mbwa wengne wanabweka mahakama gani? nasi binadamu tutamjibu "kwa hyo majibu yake yasiyo na shinikizo la kisheria ndo utayaamini kuliko yale ya kizimbani?

kizigha achana nao piga kazi, kelele za kubweka hazijaanza leo.

kizigha huyu huyu akienda huko tecdema ataonekana malaika na hakuna atakaye panua matako wala vidole kuhoji
-mifano ipo..kwa hayati lowassa, sumayi?
kwa hyo msipigie watu kelele maana hamjui siasa wala uongozi wa kisiasa.
 
Unatetea kila uchafu ili ujikimu
 
CCM huwa wanaiba kura kila mara na ushahidi upo, je ulishawahi kuwaona wanajitokeza kukataa hawaibi?
 
View attachment 3569282
Tangu Rais Samia alipomteua Angela Kizigha kuwa Mbunge Aprili 2, 2026 kumekuwa na maneno mengi mno kuhusu mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mbunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EALA).

Chanzo cha maneno hayo ni tuhuma zinazomkabili Kizigha za kutokamilisha tenda ya ununuzi wa sare za Jeshi la Polisi, ambapo ilibainika kuwa sare hizo hazikuletwa.

Suala hilo liligusiwa na Hayati Rais John Magufuli alipokuwa akizungumza katika Ikulu ya Dar es Salaam Julai 18, 2016, akisema kuna mtu amelipwa mabilioni ya fedha kwa ajili ya kuleta sare za Jeshi la Polisi, lakini hazikuletwa na akautaka uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ufuatilie.

View attachment 3569289

Kupitia ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2018 ilibainika kuwa kampuni ya Daissy General Traders alipewa zaidi ya Sh16.66 bilioni lakini hakuleta sare hizo.

Ukaguzi wa CAG ulibaini, kuwa maoni ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hayakuzingatiwa na malipo ya Sare za Polisi ambazo hazikuletwa kwa Boharia Mkuu wa Jeshi la Polisi Sh.16,660,000,000 hazikurejeshwa.

Pia Mzabuni alishindwa kuwasilisha nyaraka za kuthibitisha uletaji wa mzigo, ikiwemo hati ya kupokelea Shehena ya Mzigo Bandarini (Bill of Lading), hati ya madai kutoka kwa mtengenezaji (Commercial Invoice), hati ya mzigo ulipotoka (Certificate of Origin), orodha
za mali zilizopo kwenye meli (Packing List) na cheti cha ukaguzi wa bidhaa (Inspection Certificate) kutoka kwa Mzabuni Daissy General Traders kwa ajili ya kujiridhisha kama bidhaa husika zililetwa nchini.
View attachment 3569290
Kwa mujibu wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, Angela Kizigha aliyekuwa amegombea ubunge Kawe Dar es Salaam mwaka 2020, alienguliwa kwenye ushindani huo na Rais John Magufuli, akitoa sababu hiyo hiyo ya upotevu wa fedha za sare za polisi na alisema watamshitaki.

Hata hivyo, Polepole alishangazwa na ukaribu wa Kizigha na Rais Samia Suluhu Hassan, baada ya kifo cha Magufuli na hatimaye akawa mtu wake wa karibu.

Kizigha alikuwa mtu wa karibu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 na hatimaye sasa ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Tangu zilipoibuka kashfa za upotevu wa fedha kwa ajili ya sare za polisi, Angela Kizigha hajawahi kujitokeza hadharani akakanusha, wala pengine kuchukua hatua za kisheria kusafisha jina lake.

Kama hiyo kashfa ni ya uongo au kusingiziwa, tungetarajia kumwona akikanusha hadharani au pengine hata chama chake kumshafisha kwamba hahusiki. Lakini suala hilo lilifinyangwa finyangwa baada ya kifo cha Magufuli na hatimaye sasa Kizigha ni mtu wa karibu na rais.

Badala yake sasa wanaibuka chawa kumtetea Kizigha. Wengine wanasema ametokea katika familia ya kiukombozi iliyomsaidia Baba wa Taifa Julius Nyerere alipotaka kuuawa. Kwamba baba yake Kizigha (Charles Kizigha) ndiye aliyefichua njama za kuuawa Nyerere na kufanikisha kukamatwa kwao.

Sasa hata kama ametokea kwenye failia hiyo, inahusikaje na kashfa iliyoko mbele yake? Kwamba mtu akitoka kwenye familia ya ukombozi, basi yuko huru kufanya ufisadi?

Wapo wengine wanasema licha ya Magufuli kutaja kashfa ya ununuzi wa sare za polisi, lakini hakukuwa na uthibitisho. Kama ni hivyo, mbona walikaa kimya bila kujisafisha. Kama kuna uchunguzi ulifanywa na kubaini kwamba Kizigha hana hatia, kwa nini haukuwekwa wazi.

Nimewaita hao watetezi wa Kizigha kuwa ni chawa, kwa sababu wanatetea kitu kisichowahusu. Kama ni kosa anatuhumiwa Kizigha, basi yeye mwenyewe ajitokeze ajitetetee, sio kutuma vibataka wa kumtetea mitandaoni.
Kwa upande mwingine, Rais Samia aliyemteua naye alipaswa kufafanua suala hilo, lakini kama atakaa kimya, basi kuna kitu hakipo sawa.
Kilichomfanya Magufuli kushindwa kumfikisha mahakamani kama ni kweli ni nini Hadi iwe nongwa?

Kwa nini usiwe uzushi na vita za Kisiasa Kwa sababu hakuwa mtu wake?

Naendelea kuunga mkono hoja,akae kimya mtafute majibu wenyewe
 
Kwahiyo ajitokeze kuwajibu nyumbu wanaoongozwa na lofa Moja lililojitokeza, bila aibu, kwenye vyombo vya habari na kusema eti Lita Moja kwa Sasa inafika hapa nchini kutoka huko Hormuz kwa Raha.2100?!!!!! Akifanya hivyo basi huyo Kizigha mwenyewe atakuwa punga kama bernard bakar au q.
 
Asipojijijtea nini kitatokea?

Ripoti ya CAG ina madudu kila siku umewahi kuona mtu kajijitea au kuwajibishwa?

Shamba la Heri, mbuzi wa Heri kwahiyo yote heri.
 
Kilichomfanya Magufuli kushindwa kumfikisha mahakamani kama ni kweli ni nini Hadi iwe nongwa?

Kwa nini usiwe uzushi na vita za Kisiasa Kwa sababu hakuwa mtu wake?

Naendelea kuunga mkono hoja,akae kimya mtafute majibu wenyewe
Linyumbu kama linyumbu halina uwezo wa kuchambua mambo kwa namna hiyo. Yenyewe ipo kwa ajili ya kukaririshwa ujinga ujinga tu na kina lissu au kitima basi. Mjulishe kuwa miaka mitano baadae baada ya kutoa kauli hiyo, JPM alikuwa yupo tu na madaraka yake........muda ulimtosha yeye kama yeye kumshughulikia.
 
Kwa mtu anayewajua watanzania, hawezi kupoteza muda kujibu hisia za watu

"unapokuwa safarini, usipoteze muda wako kumrushia mawe kila mbwa anayekubwekea, kuna wengne wanabweka ili ujue kuwa hapo kuna mbwa"

Mwenye ushahidi atangulie mahakamani mkahojiane huko kizimbani
-utasikia mbwa wengne wanabweka mahakama gani? nasi binadamu tutamjibu "kwa hyo majibu yake yasiyo na shinikizo la kisheria ndo utayaamini kuliko yale ya kizimbani?

kizigha achana nao piga kazi, kelele za kubweka hazijaanza leo.

kizigha huyu huyu akienda huko tecdema ataonekana malaika na hakuna atakaye panua matako wala vidole kuhoji
-mifano ipo..kwa hayati lowassa, sumayi?
kwa hyo msipigie watu kelele maana hamjui siasa wala uongozi wa kisiasa.

Kwa Mujibu wa Mwendazake ni kwamba ushahidi alikuwa nao na wote aliowataja hapo kuwa wanajua ni kwamba ushahidi wanao, ni usenge uliopitiliza kutaka raia wa kawaida wawe na ushahidi wa fraud pamoja na embezzlement zinazofanywa na vigogo serikalini.
Kwenye developed countries unaposikia viongozi wanajiuzulu sababu huwa ni fraud/embezzlement allegations na si kwamba panakuwa pameletwa ushahidi mezani na anapogoma kujiuzulu huwa anatoa his/her side of the story lakini si kukaa kimya eti "hili nalo litapita, Watanzania wanasahau haraka".
Mbona kipindi cha Jiwe hamkumuuliza hayo maswali mnayouliza sasa juu ya huyo muhuni Kizigha au kusema aachane na kelele za Jiwe au mbona hamkumwambia Jiwe alete ushahidi na hamkumpinga hadharani kwamba anamsingizia Kizigha.
Where you see smoke definitely there is fire underneath.
NB: Uchawa ni usenge.
 
Back
Top Bottom