Nadhan tutambue penzi la dhati ni lilelinalotoka ndani ya nyama za moyo. Upendo wa dhati huvumilia, pendo halitaki makuu, mimi naamini kuwa hama kitu duniani ambacho kinaweza kumfanya mwanadamu awenafuraha yadhati kama kujua kunamtu anayempenda kwa dhati ya moyo.. Kejeli, kashfa, matusi ni dhihirisho la kilichojifika moyoni.. Maranyingine nadhani ni uvivu wa kufikiri kwa baadhi ya wanawake ama nikutokana na kutokushirikishwa katika maamuzi muhimu ya kifamilia mwanamke anakuwa hana maamuzi na mpangilio wa fedha hapewi fursa ya kuchangia lau kimawazo maendeleo ya familia hii inapelekea ajione mtumwa ndani ya ndoa na asiekuwa na thamani hapa ndipo upendo unapo poa, na zao la upendo kupoa ndio dharau matusi na kejeli.. Wanaume tunapaswa kutazama tulipo jikwaa na sio tulipo angukia, na iwapo mwanamke unamshirikisha vilivyo katika nyanja zote lakini bado akataka vitu vilivyo nje ya uwezo wako! basi tambua huyo hana mapenzi yakweli na wewe... Siku shauri umwache la! kwani sio rahisi malaika kushuka kutoka mbinguni kuja kubadili tabia za wanadamu bali wanadamu tunapaswa turekebishane sisi kwa sisi, kumbuka usije ukatumia shoka ukucha unapofaa... Ahsante