..ngoja FL1, Pretty,MwanajamiOne,Nyamayao, binti Maringo waje najua wanaweza kuwa makungwi wazuri wale. Lakini kwa mtazamo wangu baadhi ya hawa wadada ambao ni wazuri lakini bado wanakosa kuolewa ni kutokana na vitabia vya kuwa na ndoto za may be kupata mume wa class ya juu ambaye huenda kwenye mazungumzo na marafiki zake huwa wanasimuliana. Kwa mfano nakumbuka jamaa yangu mmoja ana mdogo wake wa kike binti kwa muonekano wa nje ni mzuri sana, ana shule nzuri na mwaka jana tu amepata kazi yenye malipo mazuri na trip za nje nyingi. Tukiwa kwenye mazungumzo kwa kuwa tumezoeana akaniuliza kama utani kuwa nimtafutie mchumba naye anahitaji kuolewa, nikamuuliza yule jamaa yako wa tuliyekuwa tukikuona naye vipi? akadai jamaa alishaoa two years ago. Nilishangaa kidogo, lakini binti akaniambia kuwa kwa kuwa umri wake anaona umeenda kidogo na haoni dalili ya kuolewa anafikiria kutafuta at least mtu wa kuzaa nae tu hata kama ni mume wa mtu. Lakini nilichogundua kwa huyo binti ni katabia alikokuwa nako huko nyuma kuwa atapenda apate mume mwenye angalau nyumba mikocheni, awe na gari nzuri, kwa maelezo yake angalau akaunti yenye salio la 5ml na ingekuwa vizuri zaidi kama atakuwa Dr wa tiba, Lawyer au dereva wa ndege (pilot). Mawazo yao si mabaya lakini nadhani uhakika wa kupata watu wanaolingana mitazamo yao ni majaliwa zaidi. na hata wale waliobahatika kuwapata hao hizo ndoa zao hazikufika mbali maana mtu akiyumba kidogo kiuchumi binti anatafuta mbadala. So uchaguzi wao ndio hupelekea kuishia kumegwa tu na hakuna kuolewa.Naona bado hakuna wachangiaji!
Buchanan hii mada ina mashiko sana ila wakishazungumza wao nafikiri na sisi ndio tutapata cha kuongea.
Karibu Mlimba Mkuu upate japo mpunga
Buchanan hii mada ina mashiko sana ila wakishazungumza wao nafikiri na sisi ndio tutapata cha kuongea.
Karibu Mlimba Mkuu upate japo mpunga
Ni bahati kupata Mke/Mume anayefaa.
Kwa kifupi na kwa maelezo rahisi naweza kusema kwamba wanaume wana advantage ya kuchagua wa kumuoa, mwanamke anasubiri kufuatwa na mwanaume ambaye anaona anamfaa kumuoa.Subira hiyo inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu.Wasichana wengine ni kweli wanachagua sana hadi umri unapitiliza na kufanya ushindani kuwa mkali zaidi katika " soko la wachumba".Wengine wanafikiria kujipanga vema kabla ya kuolewa - elimu au kiuchumi na wakati mwingine malengo haya huja kuwa kikwazo katika kupata mchumba mzuri!
Si vizuri kwa mwanamke kukubali kirahisi kuolewa, ni muhimu sana kumjua anaoa ni nani.. Sasa basi, kile kipindi cha kutaka kujua nani anaeoa, ndio mwanamme hukumbia.. Mara nyingi wanawake waliokimbilia kuolewa haraka wamepatwa na matatizo tofauti, unakuta mwanamme anaekuoa kumbe alishaoa mara 2 au 3 nyuma, au ni jambazi la kutumia silaha nk. Lkn si wote wanaokutwa na matatizo hayo. wengine huwa ni kiburi tu! KUTINGISHA kibiriti kama kweli unapendwa na ndio unakuwa mwanzo wa kuachwa.
Ni kweli kabisa WOS kumpata mke kwa sisi vijana limekuwa jaribu kubwa kuliko majaribu mengine. Unaweza pata pesa ya kutosha lakini ukakosa mke anayefaa.Ni bahati kupata Mke/Mume anayefaa.
Narudia tena kusema mada yako ni nzuri sana na inaweza kuwa msaada kwa wanawake na wanaume ambao hawajao wala kuolewaNi kweli wakitoa mawazo wahusika italeta changamoto nzuri badala ya kuwasemea. Mimi nimechokoza tu, na nawasikitikia sana wasichana wenye sura nzuri kwa kuwa wao ndio victims namba moja! Huko Mlimba nilishawahi kufika miaka ya 2005/2006, sijui nitafika lini tena! Nashukuru hata hivyo kwa mwaliko wako, ubarikiwe!
Nimefurahia sana usemaji wako Buchanan!Nashukuru WOS kwa mawazo yako mazuri. Unawashauri nini akina dada, maana msichana akishapita umri wa miaka 30 kuolewa linaanza kuwa jaribu?
Huyu Mkuu ametulia sana kwenye maandiko yake!!! Is among the people ninaowakubali kwakweli. For instance hii mada yake ni mada ambayo kwa undani ni muhimu sana ila ikichukuliwa light itapoteza lengo!!!Nimefurahia sana usemaji wako Buchanan!
Huyu Mkuu ametulia sana kwenye maandiko yake!!! Is among the people ninaowakubali kwakweli. For instance hii mada yake ni mada ambayo kwa undani ni muhimu sana ila ikichukuliwa light itapoteza lengo!!!
Big up Buchanan and PJ too!! You are always in my heart Men