Kwa Nini Baadhi ya Wasichana Wanapata Waume Wa Kuwaoa Haraka Lakini...?


Naam ni bahati kupata Mume. Unaweza kukuta msichana bomba sana katulia na labda madarasa yamepanda ya kutosha tu lakini wanaume wanapishana kila baada ya muda mfupi na huyo mwanadada kuendelea kubaki katika single's club kwa miaka kibao na hata kuanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu biological clock yake. Wengine huanza kwenda hata kwa waganga kutumia miti shamba ili waongeze mvuto ili hatimaye wapate mume.

Ni kweli pia wengine wanakuwa wameweka requirements zao juu sana kiasi ambacho kumpata mtu ambaye anaweza kuzitimiza zote inakuwa ni kazi mno hivyo huishia kung'aa macho na wanapokuja kushtuka it is too late hivyo wanabaki solemba.
 
......Kuna baadhi ya wasichana ni too selective wengine wanataka mwanaume mwenye elimu, mwenye pesa na vitu kama hivyo.

......Kuna baadhi umri unawadanganya, utakuta binti kwenye age ya 20s wanaume wanamfuata sana lakini yeye anasema kuolewa mapema hataki kwa kuwa atabanwa sana na mwanaume, hivyo ana subiri kwanza. Utakuta akifika 30 kuna baadhi ya wanaume hawapendi kuoa mwanamke mwenye 30.

........Kuna wanawake wengine kuolewa hadi awe na vitu vyake, utakuta hadi aje kupata hivyo vitu umri umeshakimbia,wengine tabia tu mbaya utulivu zero.
 
Kuna wanawake wengine wanapenda wanaume warefu tu.

Ila pia ndoa siyo ya kila mtu. Kuna watu wengi maisha ya ndoa hawayawezi. Ni bora kujijua uko kwenye kundi gani kuliko kulazimisha kuingia kwenye kitu kisichokufaa au usichokiweza.

Mimi najijua na sitakuja kuoa.
 

Mh, hapa kazi ipo! Kama utahitaji kuwa na watoto utawazalisha akina dada halafu utalea watoto au huhitaji watoto kabisa? Na kama utahitaji watoto huoni wataingia kwenye tatizo la utunzaji, ie mother/father roles? Jambo jingine ni heshima kwa jamii, mtu asiyeoa anaonekana ni mhuni tu, haheshimiki! Hata mgombea u-Rais akiwa anagombea anatakiwa awe na mke ndio agombee! Japokuwa ndoa ina changamoto zake, kama ukiweza kulea familia basi utaweza pia kulea Kanisa, msikiti, unaweza kuongoza idara au jamii yoyote kwa kuonyesha kujali na kuvumilia! Usije ukafikiri kama huwezi kumvumilia mke basi utaweza kumvumilia mtu yeyote!
 

Suala la kuoa/kuolewa siyo dogo! Kwa msingi huu, uamuzi wa kuchagua mwenzi wa maisha wa kuzeeka naye si uamuzi mdogo.Huwezi tu ukakubali kuolewa kwa vile tu kuna mwanaume kakutamkia nataka kukuoa.

Umeainisha makundi ya wanaume..lakini haina maana kuwa kweli hawa ndio wanaume waliobakia! Wapo wanaume wengi wasomi au hata wenye nafasi zao ziwe za biashara au kazi na wengi pia wako kwenye kigugumizi cha kupata mwenzi. Nasema hivi kwa vile nawaona na kuzungumza nao.Wako wengi wanaosema wanatamani kuunganishwa na wanawake potential lakini tatizo linakuja - ukimuunganisha mtu halafu akaja kukumbana na changamoto za kwenye ndoa akianza kukulaumu utasema nini?Anyway - tukiacha hilo labda niseme kuwa wanawake walio kwenye umri wa kuolewa - miaka 22- 30 wasipoteze muda saaaana kuchagua na kama wako vyuoni watulie watapata wachumba huko.Wengi wamemaliza masomo ya vyuo na kutoka na degree na mchumba.Wakitoka hapo na kuja kuhangaika mitaani kula maisha kwanza basi chances are watajikuta miaka ikienda na hakuna mchumba/mume anatokea.Hata akina kaka ushauri ni huo huo.Mchumba wa kufaa utampata kwenye mazingira unayoshinda muda mwingi ( isipokuwa kwenye vilabu vya starehe na pombe)!

Kuna wanaume huogopa wanawake wasomi.Huu ni woga usio na maana.Mtu kama ni mzuri/mwema mwenye sifa njema haharibiki kwa elimu yake.Kumbuka siyo elimu inayomfanya mtu kuwa mbaya bali ni malezi na ulimbukeni.Chunguza utabaini!
 
Wandugu tutoe michango ambayo ina "the way forward!" Hadi sasa naona akina "she" wengi bado "wamekula jiwe!" Haidhuru, anyway, tuendelee!
 
WOS, wanawake wanataka wanaume wasomi, wanaume hawapendi wanawake waliokula shule either kuwazidi au kulingana! What a coincidence?
 

Kuchagua mwenzi ni sahihi kabisa na wala sipingi hilo!!!ila ni jinsi gani unachagua shida inaanzia hapo.kwa mfano kuna siku nilikuwa nazungumza na Msichana fulani ana umri wa miaka 22 sasa na yuko UDSM mwaka wa pili sasa anakula Nondoz zake pale,akasema yeye anataka akiolewa Tu asikae kwenye Nyumba ya Kupanga!!!na anataka/anapenda aolewe kipindi tu atakapo maliza masomo yake yani by July 2011 awe amefunga ndoa na kwa sasa hana mchumba na sisi ndo wanafunzi wenzake(watu tunaomzunguka) na pia hata kulipia vyumba mtaani pesa hatuna!!!kwa kauli yake tu ilikuwa ikionesha kuwa dada zetu wanapenda sana mabwana ambao tayari wako poa kipesa na hilo linafanya kuwa ngumu kwa sisi ambao tuko nao karibu kuwaoa.

Tatizo lipo sana kwa hawa dada zetu.
 
Kuna siku nilikuwa naangalia Kipindi fulani cha TV "Longa Mwanamume" sijui kama kiipo hadi leo maana siku hizi sipo tena Tz!!!kuna mtu alisema vijana wengi siku hizi hatutaki kuoa/kuolewa maana "TUMEKOSA NDOA ZA MIFANO".
Yaani ndoa za siku hizi watu wanaoana lakini bwana ana VIMADA KIBAO na Bibi nae ana Mabwana wengine wengi tu nje na hili jambo limezidi kuwa kubwa sana kwa jamii yetu ya kitanzania na sijui tatizo ni nini hasa linalopelekea mambo kama haya!!!
Hilo pia linawafanya vijana kutoa na linafanya wanawake wakose waume!!!
 
 
Kumpata mwenza wako mtakae elewana na kuvumiliana ktk maisha haya ni ngumu sana.
Yaani ni sawa na kunguru kunyea manati.

Ishu ni kuwa tamaa imeshika hatamu, na kujiendekeza kumezidi kwa pande zote mbili.

Demu anakuwa na bwana derena tax kwa ajili ya kumsaidia usafiri, muuza mitumba kwa ajili ya mapigo mapya,
Muuza vocha, anakuwa na jibaba lake la kuchuna 2, kisha anakuwa na king'ast wa kuuza nae sura then anakuwa na yule sasa anayemfikisha.

Sasa wahenga wanasema mazoea hujenga tabia, je huyu akiolewa atawaacha?.

Ndio maana wanamegwa na kuachwa...pumnaa
 
mada nzuri sana sema wadada wanaoisoma nina hakika wote wameolewa hapa .
 
Mh, hapa kazi ipo! Kama utahitaji kuwa na watoto utawazalisha akina dada halafu utalea watoto au huhitaji watoto kabisa?

Una maana gani unaposema "utawazalisha"? Hilo neno kwangu halipo. Mtoto mnazaa wote hata kama hamjaoana. Kwa mwajibikaji hakuna ugumu wowote katika kulea mtoto iwe ndani ya ndoa ama nje. Na kuzaa mtoto/watoto si lazima uwe kwenye ndoa.

Na kama utahitaji watoto huoni wataingia kwenye tatizo la utunzaji, ie mother/father roles?

Kama niliposema hapo juu kwa mtu mwajibikaji hakuna ugumu wowote kulea na kutunza mwanao hata kama haujaoana na mzazi mwenzako. Mtoto ni wako mwenyewe kwa nini iwe shida kumtunza? I have zero tolerance for deadbeat parents.

Jambo jingine ni heshima kwa jamii, mtu asiyeoa anaonekana ni mhuni tu, haheshimiki!

Ni watu wenye akili fupi kwenye jamii ndio hufikiri namna hivyo. Kuna watu wengi tu ambao hawajaoa na hawafanyi hata robo ya mambo ambayo watu walio kwenye ndoa wanafanya. Ni unafiki mtupu kumheshimu mtu anayemwibia mwenzake eti kwa vile tu yuko kwenye ndoa. Ujinga kabisa.

Hata mgombea u-Rais akiwa anagombea anatakiwa awe na mke ndio agombee!

Oh really? Hilo sharti liko stipulated kwenye katiba?

Japokuwa ndoa ina changamoto zake, kama ukiweza kulea familia basi utaweza pia kulea Kanisa, msikiti, unaweza kuongoza idara au jamii yoyote kwa kuonyesha kujali na kuvumilia!

Bogus! Papa Benedict hana mke wala watoto (at least anao waclaim hadharani) na anaongonza wakatoliki bilioni moja na pia ni mkuu wa nchi ya Vatican. Na ni viongozi wangapi walio na wake na waume ambao wameshindwa kuongoza? Hebu acha hizo bana.

Usije ukafikiri kama huwezi kumvumilia mke basi utaweza kumvumilia mtu yeyote!

Huu ni uzushi mkubwa. Mahusiano ya kindoa yana uhusiano gani na interaction yako na watu wengine?
 

Ok! Kwa hiyo unategemea kulea "watoto haramu?" (ie watoto wa nje ya ndoa? Au kama wanavyodai kitanda hakizai haramu?) Na vipi kuhusu fact kwamba kuzaa nje ya ndoa ni dhambi kwa Mungu? Au unafikiri maisha yataishia hapa duniani tu?
 
Buchanan hii mada ina mashiko sana ila wakishazungumza wao nafikiri na sisi ndio tutapata cha kuongea.
Karibu Mlimba Mkuu upate japo mpunga

Vipi Mlimba kunasemaje? Hivi ile rest house ya Kihanzi bado inalipalipa?
 
Ok! Kwa hiyo unategemea kulea "watoto haramu?" (ie watoto wa nje ya ndoa? Au kama wanavyodai kitanda hakizai haramu?) Na vipi kuhusu fact kwamba kuzaa nje ya ndoa ni dhambi kwa Mungu? Au unafikiri maisha yataishia hapa duniani tu?

Hebu ntafutie Aya kwenye bible ama msahafu inayoelezea harusi ya Adam na hawa au harusi ya Nuhu au kama Elia na Elisha walioa.
Kama hakukuwa na ndoa basi ukae ukijua sisi wooote ni haramu coz tumetoka ktk kizalia haramu.
 
Hebu ntafutie Aya kwenye bible ama msahafu inayoelezea harusi ya Adam na hawa au harusi ya Nuhu au kama Elia na Elisha walioa.
Kama hakukuwa na ndoa basi ukae ukijua sisi wooote ni haramu coz tumetoka ktk kizalia haramu.

You must be joking, right? I hope you can simply define the words "adultery," "fornication" as well as "sexual immorality!" Beware of your attitude, it will cost on the Day of Judgment when men's secrets are finally exposed!
 
Kuolewa ni Mpango wa Mungu,kwa ninavojua mimi.
Mimi nina experience na akina dada wa aina 2.
1. Wanaoishi maisha ya wokovu( waliookoka)
Kule kanisani kwa uchunguzi wangu mdogo ni kuwa Wanawake ni wengi kuliko wanaume.Na kuna mafundisho kule kuwa ni lazima uolewe na aliyeokoka,kama hajaokoka sio mpango wa Mungu.Na no matter what ni lazima usubiri mpaka muujiza utokee.Ukienda nje ya kanisa kwa maana ya siyeokoka basi ni dhambi na unaweza hata kutengwa.Vilevile wadada hawa waliookoka wakati mwingine wanaweza kukutana na wasiookoka na wakapenda na wakaamua kukubaliana lakini inakuja tatizo kuwa wanaume wasiookoka wanataka mpaka "watest" kabla ya ndoa,jambo ambalo ni dhambi kubwa kwa wadada hawa na wanajikuta wakishindwana.

2.Wanaoishi maisha ya kawaida( i mean church wanaenda lakini hawafuatilii sana mambo hayo)
Mara nyingi wana uhuru mkubwa wa kujichagulia wanayemtaka.Na hii imepelekea kuweka material things mbele na wakijikuta wakichagua sana wakati muda unaenda.
Lakini pia sababu nyingine ukweli bado upo palepale kutokana na takwimu,kuwa wanaume ni wachache kuliko wanawake.Hivyo wanawake wengi ni lazima wabaki bila kuolewa.No way out kwa vile sheria za kanisa zinataka mme 1 na mke 1.
Ni hayo tu kwa leo na ni mtizamo wangu tu.
Asanteni.
 



we ZD mbona unatuchanganya hapo? una maana wanaume waliookoka ndio wengi au? mbona sijakuelewa? fafanua plz
 
Hebu ntafutie Aya kwenye bible ama msahafu inayoelezea harusi ya Adam na hawa au harusi ya Nuhu au kama Elia na Elisha walioa.
Kama hakukuwa na ndoa basi ukae ukijua sisi wooote ni haramu coz tumetoka ktk kizalia haramu.

Nimekugongea senks mkuu,kaangalie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…