Kwa nini bado wafanyabiashara wa rejareja wanauza mchele na karanga ambazo hazijachambuliwa?

Kwa nini bado wafanyabiashara wa rejareja wanauza mchele na karanga ambazo hazijachambuliwa?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Hili swali nimejiuliza kwa muda mrefu sana na sijawahi kupata jibu.

Inakuwaje unaenda dukani unakuta muuzaji anauza mchele au karanga ambazo hazijachambuliwa?

Inafikirisha sana karne hii na zama hizi bado tunanunua mchele wenye mawe, na kwa kuwa unapimwa ule uchafu nao pia unalipia.

Hivi wafanyabiashara hawajaona kwamba ili kujitofautisha na washindani wao katika soko, akiweka kijana pale au mdada akachambua mchele wake au karanga, anaweza akajiongezea wateja?
 
Ni wazo zuri ila sio rahisi kulitekeleza soko la kisutu wanajitahidi sana kuweka bidhaa zao katika usafi na ubora nadhani siku Moja tutafika huko
Mfano mzuri ni wauza matunda wanavyoyapaki vizuri
 
Watanzania wengi wanapenda vya bei ndogo
Mauzo yako yakiongezeka utamlipa huyo anayekusaidia kuchambua au unaweza kuwaomba wateja watoe tip ndogo ndogo kumlipa mchambuaji.

Nafikiri hili tatizo limechagizwa na uwepo wa madada wa kazi majumbani. Watu wanaona kuna mtu nyumbani ataenda kuifanya hiyo kazi.
 
Ni wazo zuri ila sio rahisi kulitekeleza soko la kisutu wanajitahidi sana kuweka bidhaa zao katika usafi na ubora nadhani siku Moja tutafika huko
Mfano mzuri ni wauza matunda wanavyoyapaki vizuri
Kwa nini si rahisi kulitekeleza? Ni suala la mtu mmoja kuona litampa faida ya kiushindani kwenye soko na wateja wakiitika, wauzaji wote watafuata mkumbo.

Kwenye matunda siku hizi naona wanajitahidi ila nilikuwa nashangaa matunda unakuta ni machafu yana udongo umegandiana.
 
Bidhaa nyingi zinafanyiwa packaging nadhani tunaelekea huko bado Mchele ambao nadhani inatokana na wateja ambao ukichambua vizuri ukawaambia 3000 kilo wataenda kwa asiechambua wa 2700 so Bora umuuzie hivyo hivyo ili umpate anaetaka wa kuchambuliwa achukue wa korie
 
Back
Top Bottom