Kwa nini biashara za mtu mweusi akifa mwanzilishi na biashara hufa

Lufthansa

New Member
Joined
Apr 12, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Habari zenu wana jamvi, hivi ni kwa nini biashara za bongo hasa hasa zinazomilikiwa na watz weusi huwa haivuki kizazi zaidi ya kimoja?

Yaani unakuta anapokufa muanzishaji wa ile biashara basi umaskini unapiga hodi kwenye hiyo nyumba ,,kwa ni hatuwezi kurithisha biashara kutoka kizazi kimoja hadi kingine kama wenzetu waarabu na wahindi wanavyofanya ?
 
Biashara yoyote iliyofanikiwa inasiri... Kufanya kaz kama mtumwa, nidham ya pesa, akili mingi n.k

Sasa wazazi wengi ni asili kutopenda watoto wao wapitie magum waliyopata wao, hvyo kutaka kuwapitisha shortcut na hapo ndio kivumbi huanza.....

Unakuta baba n mfanya biashara mzuri lakini watoto wake wote amna anaesomea fani yake hata mmoja, yani hakuna anayeandaliwa kurithi mikoba!!!

Kurithishana biashara tumefeli lakini kwenye uchawi na uganga
tumefanikiwa....... Reason n kuwa wachawi huwaandaa warith wao mapema (kiakili na kiutendaji), pia kweny uchumi wa familia ingefanyika hvyo kisingeharibika kitu

Ushuhuda: kipindi nipo advance nilisoma PGM, darasani tulikaa na watu wa EGM.... Nilichogundua n kuwa EGM na HGE (kombi za biashara) zilikuwa na wahindi pamoja na waarabu wengi,,,,,, sisi kinakinjekitile tunakomaa na calculus!!! Jamaa wakimaliza kusoma wanaenda kufanya kaz kwenye business zao 🚶🚶🚶
 
Angalia watoto wenu kwanza
Je mkiwa na biashara mnawafundisha kazi hizo?
Watoto wanaranda barabarani na vijiweni kazi hawafanyi na wazazi hawana ukaribu na watoto
Umeona watoto wa wenzenu wanakaa vijiweni baada yashule unamkuta dukani anarudisha chenji

Mzazi lazima amfundishe mtoto nidhamu na heshima ya hela
La sivyo mtarogana sana na mtasubiri baba afe tu muuze mali zote kwa sababu hakuwaweka karibu na biashara zake

Hao unaowasema wanawaweka mbali na waswahili ili wasio nyuma kimaendeleo
 
Wenye akili ni wachache, utafutaji ni kazi ngumu, kujitoa, kutumia akili nyingi, kutunza muda,nidhamu ya pesa. Watu wengi wanapenda kufanikiwa bila kuwa tayari to pay the price. Wanapenda kula maisha kutokana na kukulia kwenye lindi la umaskini lenye ukosefu wa vitu vingi.
 
Utajiri wa biashara na mali utabaki TU pale familia itakapokubali kulipa gharama za muda akili na maarifa Yao katika hizo biashara,vinginevyo umaskini unarudi kwenye hizo familia,haiwezekani hata kidogo biashara au mradi wowote kuendelea kama hakuna usimamizi wa kutosha na uwekezaji endelevu wa muda. bahati mbaya kizazi Cha Leo,kinataka miradi Yao iende vizuri huku wao wamelala usingizi mnono,aliwadanganya nani ?
 
Kwa utaratibu wa kiafrika ndugu, watoto walio wengi humthamini mtu na kuwa karibu naye zaidi pale anapofanikiwa tu na huhitaji kutumia kile alichonacho na si kujifunza kufata misingi ya kupata kile alichonacho yeye.

Baada ya mwenye mali kuonyesha kuhitaji kuwafundisha kuvua badala ya kuwapa samaki ndg au watoto hao humchukia na kuona anawanyanyasa.

Final anapokufa hakuna anayejua ni njia gani alitumia kulinda mali na kupata faida pia kuepuka hasara.

All assets must be gone.

NB: Nafanya biashara niliwachukua ndg baadhi kuwafundisha misingi ya biashara na upambanaji so tumeishia kuchukiana ki familia.
 
Warithi wanakosra sifa za mjasiriamali,(traits or entrepreneurial competences), kama huna hata sifa moja ya ujasirimali huwezi kufanya biashara yoyote ile kinachofuata ni lazima uwe na mpango wa biashara, (andiko la biashara), na huo mtaji ambao km biashara ipo siyo tatizo unaangalia namna nzuri ya kukabiliana na changamito zilizopo na zitakazo kuja
 
Inategemea kabila na kabila, sisi watu wa Mpitimbi tunatoboa
 
Ubinafsi
 
Muda mwingine chanzo cha utajiri katika biashara za mtu mweusi zinatokana na dhulma, kuua na pesa chafu mfano uporaji na umafia. So unakuta mhusika kushirikisha wanae inamwia vigumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…