Kwa nini bidhaa feki zisirudishwe zilikotoka

Kwa nini bidhaa feki zisirudishwe zilikotoka

Asamwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
3,711
Reaction score
2,462
Wadau, naamini wote tunaelewa jinsi nchi yetu ilivyogeuka kuwa dampo la bidhaa feki...kuanzia dawa, vyakula, bidhaa za kilimo, elektroniki, umeme, ujenzi n.k n.k. Kila mara bidhaa feki zinapokamatwa hatua inayochukuliwa na Serikali ni Uteketezaji.

Sina hakika kama wahusika wa bidhaa wanalipa gharama, lakini lililo wazi ni kuwa uteketezaji wo wote ule mara nyingi lazima utakuwa na athari kwa mazingira.

Siku za karibuni kulikuwa na taarifa kuwa kuna tani 500 za nondo feki zilikamatwa, na kuna mpango wa kuziteketeza. Binafsi sijui uteketezaji wa chuma unafanyikaje...labda wataalam watujuze.

Kitu ambacho nimekuwa najiuliza mara nyingi na sipati jibu ni:- Kwa nini bidhaa feki zisirudishwe zilikotoka (kwa gharama za muagizaji) ili wakateketeze wenyewe?!

Nina imani kabisa hili likifanyika, nchi zinakotoka bidhaa wangetoa ushirikiano kupambana na tatizo hili. Waagizaji pia wangeachana na hii tabia maana itakuwa inawaletea hasara.

Nini maoni yenu wadau?
 
Back
Top Bottom