Kwa nini Capitalism imeshindwa kuwatoa Kenya?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Kenya ni Capitalistic state tangia day 1, lkn kwa nini imeshindwa kuwaondoa hapo? Je, tatizo ni IQ au ni nini? BTW nchi zote ambazo zimekuwa zikifwata capitalistic economic system ziko mbali sana Kiuchumi, lakini Kenya bado wana matatizo yale yale yanayozisumbua (former) socialistic states, kama chakula, tiba, malazi, na hata vitu kama maji safi ya kunywa bado ni shida, sasa kwa nini Capitalism imeshindwa Kenya?
 
Vigezo gani unatumia kupima maana nijuavyo Kenya ni kanchi kadogo bila madini wala raslimali na zaidi ya nusu yake ni kame tupu lakini kanaongoza kiuchumi na kushinda liinchi kama Tanzania ambalo lenyewe ni muungano wa mataifa mawili na lina rotuba nzuri kila mahali na madini kote kote na kila kitu kizuri, ila lenyewe maskini wa kutupwa.

Sasa wewe hapo mwananchi wa nchi kama hiyo maskini unatumia vigezo gani kuja kujilinganisha na Kenya.

Ona Kenya ilivyo na upweke kwenye hi ramani

 
Asian Tigers nazo ni nchi ndogo zisizo na madini.
Wale kilichowasaidia ni kwamba wote kwa pamoja ni wachapa kazi, nchi kama Singapore ina majirani wachapa kazi wote, sasa sisi hapa tumezungukwa na wazembe hadi inatucost. Binadamu huendana kulingana na mazingira (lipo Kisayansi), ndio maana inashauriwa uhame Tandale bora ukaishi kwenye chumba cha vijakazi Masaki, ili uamke, lakini ukibaki Mbagalla, kutwa utakua unawaza kuwahi ukacheze bao na vigodoro.

Ukiangalia hii ramani, mataifa yenye uchumi bora, wote ni majirani halafu makajamba wa LDC wamekusanyika pamoja, Kenya tu ndio mpweke.
 
Wale kilichowasaidia ni kwamba wote kwa pamoja ni wachapa kazi, nchi kama Singapore ina majirani wachapa kazi wote, sasa sisi hapa tumezungukwa na wazembe hadi inatucost.
Mjanja "hujuwa kula na kipofu", hivyo siyo lazima uzungukwe na "wajuwaji" ili uendelee. Nyinyi ni wajuwaji hamna uchapakazi wowote ndiyo maana mpo mpo tuu.
 
Simlikuwa mnaiba madini ya tz na DRC wezi wa madini wa nchi Jirani wamejificha Kenya chini ya usimamizi wa serikali yenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka capitalism haijafanikiwa kabisa duniani, sio Kenya pekee tu, kwa ujumla Africa, South America, Asia na Caribbean note huko capitalism imeshindwa ukiacha nchi chahe kama South Korea na Singapore.

Nchi ambako zilifanikiwa ni zile nchi zilizowekwa katika" Marshall plan" baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Kwa ufupi ubepari ni mfumo wa kinyama unaotengeneza matabaka, ni mfumo " unaotumia kanuni ya "Survival for the fittest", yaani kunyang'anya" kutoka kwa "weak" na kuwapa "the strongest".

Waingereza walivamia America, Canada na Australia na kuwapokonya ardhi wenyeji wa huko kwa nguvu, na kuja Afrika kuchukua watumwa kwa nguvu kwenda kuendeleza hizo nchi, hiyo ndio asilj ya kufanikiwa kwa " Capitalism " duniani.

Sasa nchi kama Kenya, ambayo haijengi uchumi wake kwa kutumia nguvu au watumwa, kamwe haiwezi kufanikiwa kwa kufuata mfumo wa capitalism. Nchi zinazotumia socialism kwa sasa zinafanya vizuri zaidi kuliko zile zibazotumia capitalism.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hili pambio kila siku unalitoa huku likisheheni makosa lukuki ya kisarufi na kimuundo.

mfano rotuba ni nini kwa kiswahili!!?

Jibu swali la why your primitive capitalist economy is still in vicious circle of poverty?
 

Karne hii ya 21 Suala la Rutuba ya Udongo ni hoja isiyo na Mashiko,
Tazama nchi zilizopo jangwani zinatoa misaada ya vyakula kwa Nchi Maskini zenye Udongo wenye Rutuba..
Hiyo ndiyo hoja ya Mleta mada, Blind capitalism imefanya hata yale mashamba yenye Rutuba kwenye baadhi ya nchi jinga kama kenya yamekuwa mikononi mwa Wanasiasa na Wazungu wanaoishia kulima maua na Chai na kuuza kwenye mataifa yao huko ulaya na marekani, Mwananchi wa kawaida anabaki kutaabika kwenye janga la njaa, umaskini, ujinga na maradhi.
 
Mwenzako juzi kati ya county 47 za kenya kashindwa kuleta county 5 tu ambazo wazungu wanamiliki ardhi...
Kwhyo heri ukakaa kimya tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taja tano tu na wanayowaniliki kati ya hzo 47..
CBD ya dar unaichukuliaje kw sasa

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo walikaririshwa wimbo ambao ilipokezwa mpaka kwa vijana wao.
Mizembe sana hawa, liinchi lote hilo yaani hadi uunganishe Uganda, Rwanda na Kenya ndio zitoshane na Tanzania halafu ina rotuba kila sehemu, full madini lakini maskini wa kutupwa.
 
Tatizo walikaririshwa wimbo ambao ilipokezwa mpaka kwa vijana wao.
Mizembe sana hawa, liinchi lote hilo yaani hadi uunganishe Uganda, Rwanda na Kenya ndio zitoshane na Tanzania halafu ina rotuba kila sehemu, full madini lakini maskini wa kutupwa.
Tatizo lako wewe unatumia reference ya Kenya au Uganda kuwa ndio nchi, kwanini usitumie reference ya Tanzania kuwa ndio nchi na hizo zenu zikawa ni nusu ya nchi?.

Qatar, UAE zinaingia Mara 4 au 5 kwa hapo Kenya, 100% ya ardhi yao ni jangwa, lakini zinawapa misaada ya chakula. Ardhi yenu yenye rutuba ni 20% sawa na eneo la nchi ya Rwanda yote, lakini Rwanda inajitosheleza kwa chakula, ila ninyi mumewapa wazungu wanalima maua na chai, wakati wananchi wa kawaida wanakufa kwa njaa. Hayo madini yetu yangekuwa Kenya, yote yangekuwa chini ya Kenyatta familiy na wanasiasa wachache.

Tatizo la Kenya sio kukosekana kwa rasilimali, ni Sera mbovu za Kibepari, kwamba wachache wenye nguvu kujimilikisha rasilimali zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jibu swali la why your primitive capitalist economy is still in vicious circle of poverty?
Hili swali gumu mnoo, hawawezi wakalijibu yaani lazima tu watoke nje ya mada kutokana na uwezo na ufinyu wao wa kufikiri ni Mdogo mnoo,
Huku wakienda chooni kwa hisani ya vyakula vya misaada.
 
Kenyan capitalism will never work kwa sababu kuna a lot of economic incoherence in the way its capitalism or mode of production has been made. Kwa ufupi mm naweza kusema Kenya haijawahi kupata uhuru mpaka leo hata kama wanajitahidi kubadili katiba na mambo mengi. Ule mfumo wakikoloni ndio unaendelea ,aliondoka mkoloni mweupe akachukua nchi mkoloni mweusi maana hakuna kitu chochote kilichobadilika. Hakuna economic reforms especially interms of land redistribution na mambo mengine. Waliojimilikisha hayo mashamba hawana uwezo wa kutosha wazalisha chakula cha kulisha kenya ,pia walilipa mishahara midogo wafanyakazi wao kiasi kwamba it was just"hand to mouth". So Kenya is a very poor country. Watu wakatumia status zao kuhujumu nchi , wakaomba mikopo IMF and World Bank na kugawana ,so nchi ina madeni kama yote ambayo alienda mifukoni mwa wachache, na viongozi wengine wakawa vibaraka wa wa wazungu kusaidia kuiba Kenya. Hebu wakenya watujibu kwa nn kuna US and UK Military bases kwao zinafanya nn? kama siyo hawo wakoloni weusi walitaka ulinzi ili wasije kupatwa na hasira za wakenya walalahoi? Sina muda wa kuandika mengi ,may be later
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…