''neno ya Muzee, ukabisha
Mwisho utapata shida''....Quotes from Hayati Dakta.
Sasa nirudi kwenye mada yako.
Alichokisema Cosmas ni cha kweli kabisa kwani tumeshashuhudia wasanii kadhaa wa kizazi kipya waliokuwa ndani ya makundi then baada ya kung'aa ktk single moja basi anatoka ktk kundi then akishapewa kagari ''vilts'' na Muhindi anayemnyonya basi nyodo zinaanza.
Au ukija kwenye medani ya muziki wa Dini mambo ni yaleyale, mtu akipata kaujiko basi hata tuzo zinazoitwa na kudhaminiwa na kilevi yeye atataka aende tu ili mradi keshajiona star.
Tuliona kwaya kama Makongoro, kwaya ya mtakatifu Cecilia Mwenge, kwaya ya Nkinga, kwaya ya Ulyankulu barabara ya 13, kwaya ya Mabibo walioimba ''sauti ikatoka'' Maranatha, New life Band...tuliwaona watu kama kina Nyambele, Mzungu Four, Faustin Munishi na wengine weeengi ambao ulikuwa ukisikiliza nyimbo zao ni sawa na kusoma Bilble au kusikiliza mahubiri.
Mfano hii kwaya ya mtakatifu cecilia Mwenge walitamba sana na albam yao inayomsifu Mama Maria mwanzoni mwa miaka ya 90 na mpaka leo ikipigwa utakubali kweli ujumbe unaupata.
Tuje kwa ulyankulu:
Hawa jamaa waliimba nyimbo kama
Nuhu, Samson, na nyingine nyingi zenye ujumbe.
Albam hii iliimbwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Kwani kila nyimbo iliyomo humu ni Mstari ktk Bible.
Kwa mfano kuna nyimbo inayosema ''mtu mkubwa mmoja aliuliza akisema mwalimu, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa Milele?''...huu ni mstari ndani ya Bible na umezungumziwa ktk nyimbo. So ina maana hata kama hujui kinachozungumziwa ktk Bible basi utakielewa ktk nyimbo.
Sasa rudi uje uwasikilize hao wanakwaya wenu wa siku hizi nyimbo zao utasikia ''nibebe'' mara huyo Frola Mbasha ana wimbo unaSema ''mwanamke simama imara'' kauimba kama mchiliku...lool
Ni ushuzi mtupu.