Ni kweli waimbaji wengi wa kizazi si wanamuziki kama wengi wanavyosema siku zote. Lakini hata hivyo katika biashara ya muziki hicho si kitu cha ajabu. Najua wengi wenu mnaosoma maoni haya ni wasomi na mnafahamu namna muziki kwa wenzetu unavyohusisha watu wengi mpaka wimbo ukausikia hewani.
Kuna wanamuziki wengi wa nje ambao ni waimbaji tu(kutoa sauti basi) ambao hawahusiki katika kutunga, kuandaa melody, kupiga chombo chochote cha muziki na zoezi zima la utayarishaji. Kila kitu kinafanywa na mtu mwingine. Lakni niambie jinsi albam zao zinavyouza! Mwimbaji asipoweza kucheza chombo chochote cha muziki haimanishi kuwa hawezi kabisa kupewa heshima yake. Sababu kubwa inayowafanya wanamuziki wa zamani wawadharau wale wa bongo flava ni wivu tu. Walikuwa na nyimbo nzuri sana katu sikatai lakini hazikuwapa chochote.
Leo hii vijana wanaodharauliwa kuwa si wanamuziki bali wababaishaji tu ndo ambao wamefanikiwa hata kuiweka kdg Tanzania kwenye ramani ya muziki duniani. Ni bendi gani ama mwanamuziki gani wa zamani ambaye amewashawahi kutajwa kuwania tuzo yoyote kubwa duniani? Kwa wengine yaweza kuwa ni sababu ndogo lakini hivyo ndo vigezo vya kutambua kama wanamuziki wetu wanatambuliwa nje ya mipaka. Wanamuziki wa zamani waache wivu kwani kulalama hadharani juu ya vijana wa sasa hv hakutasaidia chochote kama ujumbe wao wanautoa kwa dharau.
Pengine hawafurahishwi na maisha wanayoishi vijana wa sasa yaani jinsi wanavyovaa, wanavyoongea, maudhui katika nyimbo zao lakni watambue kuwa hao ni vijana sio wazee. Namheshimu sana mwanamuziki anayeipa heshima kazi ama style ya mwenzie hata kama haipendi.
Michael Jackson kabla ya kufa alikuwa ameshafanya kazi na wasanii wa sasa kama Akon, 50 Cent. Wil.iam kuonesha heshima katika mabadiliko ya muziki na pia kuwavutia mashabiki ambao muziki wa zamani hawaujui. Hayo ni maoni tu.