Johnsecond
JF-Expert Member
- May 4, 2010
- 1,076
- 211
''neno ya Muzee, ukabisha
Mwisho utapata shida''....Quotes from Hayati Dakta.
Sasa nirudi kwenye mada yako.
Alichokisema Cosmas ni cha kweli kabisa kwani tumeshashuhudia wasanii kadhaa wa kizazi kipya waliokuwa ndani ya makundi then baada ya kung'aa ktk single moja basi anatoka ktk kundi then akishapewa kagari ''vilts'' na Muhindi anayemnyonya basi nyodo zinaanza.
Au ukija kwenye medani ya muziki wa Dini mambo ni yaleyale, mtu akipata kaujiko basi hata tuzo zinazoitwa na kudhaminiwa na kilevi yeye atataka aende tu ili mradi keshajiona star.
Tuliona kwaya kama Makongoro, kwaya ya mtakatifu Cecilia Mwenge, kwaya ya Nkinga, kwaya ya Ulyankulu barabara ya 13, kwaya ya Mabibo walioimba ''sauti ikatoka'' Maranatha, New life Band...tuliwaona watu kama kina Nyambele, Mzungu Four, Faustin Munishi na wengine weeengi ambao ulikuwa ukisikiliza nyimbo zao ni sawa na kusoma Bilble au kusikiliza mahubiri.
Mfano hii kwaya ya mtakatifu cecilia Mwenge walitamba sana na albam yao inayomsifu Mama Maria mwanzoni mwa miaka ya 90 na mpaka leo ikipigwa utakubali kweli ujumbe unaupata.
Tuje kwa ulyankulu:
Hawa jamaa waliimba nyimbo kama
Nuhu, Samson, na nyingine nyingi zenye ujumbe.
Albam hii iliimbwa kwa ustadi wa hali ya juu sana. Kwani kila nyimbo iliyomo humu ni Mstari ktk Bible.
Kwa mfano kuna nyimbo inayosema ''mtu mkubwa mmoja aliuliza akisema mwalimu, nifanye nini ili nipate kuurithi uzima wa Milele?''...huu ni mstari ndani ya Bible na umezungumziwa ktk nyimbo. So ina maana hata kama hujui kinachozungumziwa ktk Bible basi utakielewa ktk nyimbo.
Sasa rudi uje uwasikilize hao wanakwaya wenu wa siku hizi nyimbo zao utasikia ''nibebe'' mara huyo Frola Mbasha ana wimbo unaSema ''mwanamke simama imara'' kauimba kama mchiliku...lool
Ni ushuzi mtupu.
Hivi Bongo fleva nao ni wanamuziki?
Mi huwa siwafagilii hata chembe..namfagiliaga prodyuza siku zote kwa ku copy, cut and paste mirindimo na mautamu ya nyimbo za watu na kuwawekea mabongo fleva!
Mnakumbuka prodyuza alivyoiba wimbo wa watu akamuwekea TID... TID akajiona yuko juu hadi alipoteremshwa kwa aibu kwa kuwekewa wimbo original sambamba na ule wake feki?
AIBU!
Sina tatizo na waimbaji wale wasiokuwa na dini maana wenyewe ni ile free style tu. Ila wale sasa wa dini wanaharibu sana na ndo maana hata wa miziki mingine wanawapaka. Angalieni muziki wa shaggy church heathen
Wanamuziki wa zamani walifanyakazi zao kwenye mazingira magumu ukilinganisha na wanamuziki wa Bongo flavor.
Enzi za Chidumule na wanamuziki wa zamani hawakuwa na fursa nyingi kama ilivyo kipindi hiki cha wanamuziki wa kizazi kpya.studio za kurekodi ilikuwa moja hapa Tanzania RTD kuliwa pia masharti ya nyimbo kurekodiwa mashairi yalifanyiwa uhariri kabla nyimbo haijaruhusiwa kurekodiwa.Wanamuziki wa Tanzania walilazimika kwenda nchi jirani ya Kenya kurekodi muziki kwenye santuri mahandalizi ya safari pamoja na gharama kubwa zilihitajika kabla ya Bendi ya muziki kwenda Kenya.Muziki wa zamani ulitumia vyombo [hala] za muziki hivyo ujuzi wa ulihitajika zaidi.Vipaji vya wanamuziki ilikuwa ni jambo lisilokwepeke hata kidogo.
Muziki wa kizazi kipya ni vurugu kubwa hakuna wataalamu wa kupiga hala za muziki eg Solo guita,Rhyzim,Bass,Saxphone,Drum,Tumba na kinanda.Wapo waimbaji wa mashairi ambao ukiwapa hata kinanda hawawezi kutumia.hawana ujuzi wa muziki hata kidogo mara kadha nimehudhuria maonyesho ya muziki wa kizazi kipya nimegundua wameathiria sana na utamaduni wa wanamuziki wa Marekani na Ulaya.Utakuta mwanamuziki wa Kizazi kipya anashusha suruali chini ya makalio,katoboa masikio,kasuka nywele,kajichubua na upuuzi mwingine mwingi unaoufahamu.
Wanamuziki wa Injili wa siku hizi tofauti na wa zamani hawana ujuzi wa muziki mbaya zaidi hawatumii neno la Mungu kwenye muziki wao maneno ya mitaani yamejaa kwenye muziki wanaouita muziki wa Injili.Muziki wa Injili unapaswa kwa namna yoyote ujikite kwenye maandiko matakatifu na si vinginevyo.Muziki wa Injili unapaswa kutumia tune ya kanisa na si Sebene au Rhumba na nk.Sebene na Rhumba hazina nafasi kwenye muziki wa Injili [Kanisa].Uchezajiwa wa wanamuziki wanaojiita wanamuziki wa Injili hauna tofauti na wanamuziki wa bendi za muziki wa dansi kabisa wakati mwingine nalazimika kubadiluisha chanel kukwepa kuangalia wanamuziki wa Injili wanvyodhalilisha kanisa na ukristo.Uvaaji wa wanamuziki wa Injili unatia kichefu chefu.
Wapo wanamuziki wa Injili na kwanya mbali mbali zinazojitahidi kufuata njia sahihi ya uimbaji wa muziki wa Injili lakini hazipewi umuhimu wa kipekee kwenye TV station zetu pengine uelewa wa mdogo wa muziki wa Injili ndani ya vyombo vyetu vya habari umechagia kuporomosha muziki wa Injili.