Kwa nini dhana ya ukiritimba(monopoly) utumike kwenye ununuzi wa pamba msimu huu 2025/26?

Kwa nini dhana ya ukiritimba(monopoly) utumike kwenye ununuzi wa pamba msimu huu 2025/26?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,199
Tunajua Tanzania tunatawaliwa na soko huria ambapo kunaruhusiwa ushindani. Juzi Mhe. Mpina aliposhauri kuwa ni kwa nini tunatumia mtindo wa ukiritimba (monopoly) katika ununuzi wa pamba msimu huu alipingwa vikali sana na Mhe. Bashe Waziri wa Kilimo.

Mazao mengine kama korosho, ufuta na mengineyo ununuzi unafanyika kupitia soko huria. Soko huria unaleta ushindani na uwezekano mkubwa wa kupanda kwa bei. Ninajiuliza kwa nini utaratibu wa ukiritimba uwe tu kwa ununuzi wa pamba?.

Nashauri tutumie soko huria katika ununuzi wa pamba kama alivyoshauri Mhe. Mpina akipigwa vita na Mhe. Bashe. Mtu anapotoa hoja ajibiwe kwa hoja na siyo chuki na mashambulizi yasiyokuwa na maana.
 
Nakubaliana na wewe, ushindani wa soko huria huwanufaisha wakulima kwa bei nzuri. Pamba isibaguliwe, nayo ifuate mfumo wa mazao mengine.
 
Back
Top Bottom