Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Dr. Idris Rashidi aliteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu baada ya kifo cha Gilman Rutihinda mwaka 1993. Aliweza kudumu hapo kwa kipindi cha miaka sita toka 1994-1999, kipindi kilichogubikwa na wingu zito la ufisadi lililohusisha hii Benki ya Wananchi. Katika kipindi hicho tulishuhudia serikali ikiingia mikataba mbalimbali iliyoifunga serikali na kuisababishia madeni makubwa.
Baada ya hapo na katika kipindi cha miaka sita alifanya kazi katika taasisi tatu tofauti ambako inasemekana alijiuzulu kwa sababu zisizojulikana mpaka alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco. Mwaka 2007 alitingisha kiberiti kwa kutishia kujiuzulu lakini JK, kwa sababu zisizojulikana, akaamua kumtetea na kukataa kumkubalia .
Je, ni uswahiba peke yake ama kuna zaidi ?
Na alitingisha kiberiti kwa kesi mbuzi ya Tanga Cement! Kama alivyoshughulikia ishu ile ndio menejimenti style yake, basi kweli tumekwisha!
Amandla............