Kwa nini hakushika ujauzito?

dropingcoco

Senior Member
Joined
Jun 21, 2008
Posts
124
Reaction score
11
Mimi na mke wangu tumekuwa tukitafuta mtoto kwa muda wa miezi 6 sasa. Muda mwingi mimi huwa safarini kwa shughuli za kikazi kwa hiyo kukutana huwa si mara kwa mara. Mara ya mwisho yeye kuona hedhi ilikuwa tar 13Aug,tukakutana kimwili tar 24/25 kisha nikasafiri.Leo amenipigia simu anasema ameanza kuona siku zake, mzunguko wake ni siku 28, je! tatizo litakuwa lipo wapi? Alishakwenda hospital na akaambiwa yupo sawa hana tatizo lolote, mimi nina mtoto niliempata ujanani. Wadau msaada wenu
 
Nendeni hospitali mkapimwe mjue tatizo nini?? acha mambo ya kizamani eti nina mtoto wa ujanani unajuaje kama ni wako??
 
suala la kushika mimba ni complicated sana kwa wengine,miezi6michache sana Hass ukizingatia hamkai pamoja Mara zote yawezekana mnazikosa zile siku bila kujua cha muhimu kuweni karibu kwa miezi angalau3 mkomuomba mungu,asikudanganye mtu eti relax ni ngumu wakati unahitaji kitu,kuweni na subira
 
Nendeni hospitali mkapimwe mjue tatizo nini?? acha mambo ya kizamani eti nina mtoto wa ujanani unajuaje kama ni wako??

Mkuu,mtu anapokuja kuomba ushauri hapa sio kwamba hajui anachokifanya, kama hufahamu kitu bora ukae kimya
 
jaribuni kukutana siku mbili kabla ya siku ya 14 ,siki ya 14 na siku mbili baada ya siku ya 14 kutoka alipopata hedhi mara ya kwanza
 
Calmdown wala usiwe na hofu huwa ni hali
tu na kwa kuwa mko safi itashika ni ku do
Hatimaye mtapata unajua pia tunaamini
mtoto Mungu ndiyo anatupatia na sio sisi.
 
tatizo hapo ni muda mwafaka ambao unakutana na mkeo.kutunga mimba ni timing tu wakati wa hot days za mkeo so inawezekana huwa unakutana na mkeo jirani kabla ya siku za kutunga mimba then unapata safari but moyoni unakuwa na hope kuwa mambo tayari.kumbe wakati ushaondoka ndo siku mwafaka sasa ya kutunga mimba.so my take ni kuwa tenga muda wa hata miezi miwili hadi sita uwe ni special for that assignment tu.pia muone daktari akushauri vyakula vinavyosaidia kurutubisha mbegu za kiume.kwa kipindi hiki punguza kabisa kunywa pombe kama unatumia.vileo vinapunguza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba.vilevile mtangulize mungu katika jambo hili.
 
Ngoja Daktari aje, wengine tunashauri kidunia. Miezi sita is nothing to complain, wapo wenye miaka 20 kwenye ndoa hawajapata watoto. kuwa mvumilivu. Ikibidi safiri na mwenza wako kama uko njiani mara nyingi.
 
mkuu ili kuongeza probability fanya yafuatayo
-fanya siku ya 14 baada ya hedhi kuanza.
-ikiwezekana msifanye wiki nzima kabla ya hiyo siku ya 14 ili kuongeza sperm count.
-usiwe unavaa boxer zinazobana sana,yani akikisha p*mbu hazipati joto.
 
Mwambie mkewa apunguze stress/ disparate za kupata mimba.
 
Jaribu pia kufanya mara kwa mara, pia usisahau siku ya 14 after menstruation!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…