Kwa nini humu Lugha ni Kujiajiri au Ujasiriamali? Humu hatuzungumzii jinsi ya Kuajiriwa.

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Kuna watu nazani huwa wanaumia sana tena mno wanapo kutana na post mbali mbali za wadau mbali mbali zinazo sisitiza watu kuwa waajiri na sio waajiriwa

Nazani wanao umia huwa wanapotea njia kwa sababu hili jukwaa ni la Ujasiriamali na Biashara. Hili sio jukwaa la ajira.Humu hatupost jinsi ya kufanya kazi za wanaume wengine

Hili sio jukwaa la wafanyakazi, mimi binafisi huwa naamini humu ni wajasiriamali sasa kama kumbe ni tofauti basi samahani.

Ila kama wewe unahisi Post za wakina Ontarioa na wengine wengi wanao zungumzia kujiajiri kama unaoa huwa ni kero kwako iwe unapita tu.

Humu Lugha ni Ujasiriamali na si kutafuta kazi au kufanya kazi za watu wengine,

Humu kuna watu wana jiandaa na ambao tiyari wameajiri waleo waoga.

Kule jukwaa la Ajiria huwa some time na post ila huwa sipost mambo sawa na ninayo.post humu kwa sababu naamini kule kweli watu wanatafuta kazi.

HUMU KAMA KUNA WATAFUTA KAZI AU WAFANYA KAZI SAMAHANI NA WATU WA AINA HIYO WAWE WANAPITA TU
 
Mkuu mbona kama umepanic baada ya watu kukukosoa kwenye uzi uliopita??...Relax and take it easy.!!
 
kweli kabisa humu sio sehemu ya kupumzikia na anaye tafuta kazi kuna jukwaa lake vinginevyo ma Mod wabadili jina, Huwezi kwenda jukwaa la Mapishi ukaenda kuongelea ujasiriamali watakushangaa sana
 
Lazima tugawane kuna walioajiliwa na wanaoajiri.Ukifungua biashara utahitaji wa kukuuzia ambaye ni mwajiriwa.Vyovyote vile hawa watu wanategemeana sana
wanategemena ki ajie? sema walio ajiriwa wanawategemea walio waajiri, Swala ni kwamba humu watu wanajadili ujasiriamali na si ajira na sio sehemu ya wafanya kazi humu hakuna TUKTA au CWT
 
Jukwaa ni Biashara, uchumi na ujasiriamali msigeuze maana. Swala la uchumi ni mtambuka hata kuajiriwa ni sehemu ya uchumi.

Hakuna aliyekukataza kupost hoja zako za kujiajiri mkuu ila chunga kauli zako, usioneshe kama vile kuajiriwa ni dhambi au ni kosa! Hata wewe kama ni mjasiriamali kuna angle ukiangalia ni kama umeajiriwa tu. Ukifungua biashara ya kuku kwa mfano kule unapoenda kununua viranga na chakula cha kuku kama unawauzia bidhaa zao tu, ni kama wamekuajiri tu.

Kuajiriwa sio dhambi mkuu. Na narudia tena ulimwengu mzima hawawezi kuwa waajiri!
 
kweli kabisa na waajiri wengi walikua waajiriwa
 
kweli kabisa na waajiri wengi walikua waajiriwa
Nazani watu wanakuwa wagumu sana kuelewa. Hivi mfano lile jukwaa la Mapenzi na uhusiano hivi unaweza enda kuanzisha mada ya kuuuza hisa?,si utaonekana fala?

Humu watu wanajadili Kujiajiri na si kuajiriwa kuna jukwaa la kuajiriwa humu ni kujiajiri.
 
Shida zenu humu huwa nazani ni sehemu ya kupita baada ya kuchoka, haya majukwa ilikuwa zamani na sio wakati huu. zamani watu hadi wanakutana now day humu kumevamiwa sana

Jamii forumu kuna majukwaa mangapi?

Humu tunajadili jsini ya kuajiri na sip kuajiriwa.

Tunajadili jinsi ya kutengeneza ajira na sio jinsi ya kuajiriwa.

Kama unataja kuajiriwa kuna sehemu Yake ila kama unataka kutengeneza ajira humu ndo pake
 
Jamaa hawataki kuamini hivi mkuu
Humu tunajadili jinsi gani tuajiri. Humu hatujadili kuajiriwa bali kuajiri. Halafu hata kama nafuga kuku ni kazi yangu mimi na sio wewe so acha.

Kuna jukwaa la ajira tafuta post zangu kule uone kama zinafanana na za huku.
 
Humu tunajadili jinsi gani tuajiri. Humu hatujadili kuajiriwa bali kuajiri. Halafu hata kama nafuga kuku ni kazi yangu mimi na sio wewe so acha.

Kuna jukwaa la ajira tafuta post zangu kule uone kama zinafanana na za huku.
Ishu sio kujadili kuajiriwa au kuajiri ishu ni usitumie lugha ya kuonesha kuajiriwa ni kebehi mkuu. Kama unavyoheshimu kuajiri kwako heshimu na kuajiriwa kwa wengine, simple! Unaweza kujadili tu kwa lugha nzuri mbona.

Wewe unataka watu waache ufugaji wako wa kuku mbona wewe unazungumzia kuajiriwa kwangu?
 
Sijui haya yametoka wapi coz inaonekana kuna chanzo,

Lakini ni sahihi kwamba jukwaa hili biashara,uchumi na ujasiriamali,

Ukileta maad humu lazima ulenge ujasiriamali(kujiajiri),Biashara in any means lakini uongelee biashara na uchumi kwa ujumla,

Huyo atakayeleta maada kwa ajili ya kutafuta kazi atakuwa anakosea kwa sababu kuna jukwaa la hayo mambo,

Lakini kuajiriwa sio dhambi na mwajiriwa pia anaweza kuleta maada yake kuomba ushauri kuhusu ujasiriamali.

Hatuna haja ya kulumbana
 
Nahisi lengo lake ni kuwamotivate na kuwa-inspire watu watoke upande mmoja waende mwingine ambao yeye anahisi ni mzuri zaidi.

Sometime kum-convice mtu inabidi umuonyeshe U-hasi wa kile anachokifanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…