Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imefafanua kwa nini wapiga kura hawataruhusiwa kupiga picha ya ballot paper baada ya kuweka alama kwa mgombea wanayemtaka katika Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Kamishna wa IEBC Ann Nderitu amesema hatua hiyo inalenga kulinda moja ya misingi muhimu ya uchaguzi -usiri wa kura.
Kwa mujibu wa IEBC, mtu anapopiga picha ya kura yake, picha hiyo inaweza kutumika kama ushahidi wa kuonyesha kwamba alipigia kura mgombea fulani. Hali hii inaweza kufungua mwanya wa kununua kura, ambapo mpiga kura anaweza kutakiwa kuthibitisha kwa picha kwamba ametekeleza makubaliano kabla ya kulipwa.
Hofu hiyo si mpya. Kabla ya uchaguzi mdogo wa Novemba 2025, maafisa wa IEBC walitoa onyo kama hilo kufuatia madai kwamba baadhi ya wanasiasa walikuwa wakiwashawishi wapiga kura kupiga picha za kura zao ili baadaye wapate zawadi au malipo.
Hata hivyo, IEBC imeweka wazi kuwa simu hazijapigwa marufuku kabisa katika vituo vya kupigia kura.
Baada ya kura kuhesabiwa na matokeo kutangazwa katika kituo, wananchi wataruhusiwa kutumia simu zao kupiga picha za fomu rasmi za matokeo. Kwa IEBC, tofauti ni kwamba ballot paper ni kura ya siri ya mtu binafsi, huku fomu ya matokeo ikiwa rekodi ya umma baada ya kuhesabu kura.
Kwa hivyo, unapokwenda kupiga kura 2027:
Ballot paper yako – no photos.
Results form baada ya counting – unaweza kupiga picha.