Ninasikitishwa na kiongozi wa Simba anayemlalamikia kipa kwa eti kuurudisha mpira uwanjani.
Hizi ni lawama za kipumbavu sana na zinakatisha tamaa.
Hazisaidii kuongeza umakini ila zinaleta kutojamini na hatimae kushuka kwa viwango.
Hivi kwa nini iwe kila mara wachezaji wa Simba tu ndio watuhumiwe kuuza mechi?
Wao hawajitambui?
Kwa nini kipa wa yanga asiuze mechi?
Hamuoni kama kweli ni hivyo ni udhaifu wa uongozi?
Binafsi niliwaonya sana kuruhusu mchezaji akatambe eti kuwafunga yanga!! Hivi hamjifunzi kuwa hiyo husababisha timu pinzani kuhamasika na kuhakikisha wanakudhibiti ili wakufunge mdomo!
Hivi mkinyamaza kwenye derbi huwa mnawashwa nini?
Ujinga utawaumiza mashabiki wenzangu wa Simba maana sijui kwa nini mnadanganyika na kelele za msemaji wakati yule ni mchekeshaji hana jipya
Sent from my Infinix X626 using
JamiiForums mobile app