Kwa nini Kenya imeshindwa ku take- off hata baada ya miaka 50 ya Capitalism?

Kwa nini Kenya imeshindwa ku take- off hata baada ya miaka 50 ya Capitalism?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Nchi ya Kenya kwangu mimi inanishangaza kwani nashindwa kuelewa ni kwa nini imeshindwa kuwa developed country kama vile Singapore, Korea au hata Malaysia wakati imekuwa ikufuata capitalistic economic system tangu kuanzishwa kwake?

I mean, Kenya haijawahi kuwa na maadui hata tu self imposed sanctions kama vile TZ yetu haijawahi kuwa nazo, Kenya imekuwa ikifanya Biashara hata na AK wakati wa apartheid, SAA ilikuwa inatua Nairobi wkt wa apartheid na kuleta Watalii wa Kikaburu, Kenya ilikuwa upande wa USA na siyo communism kama sisi, sasa ni kwa nini mpaka leo hii bado wana struggle na matatizo yale yale yanayoisumbua TZ, Uganda au Rwanda, Burundi au hata Ethiopia?

Nilishangaa kusoma kwenye Gazeti Raisi wa Kenya amekwenda Cuba kuomba Madaktari kuja kufundisha Wakenya, I mean really, Cuba ni communist country, na imewekewa sanctions na Dunia nzima hata Watalii wengine walikuwa hawaruhusiwi kwenda Cuba na wanategemea cigar tu lkn Kenya nchi yenye capitalism wanakwenda kuomba msaada Cuba, hii imekaaje? Nilitegemea Cuba waje kuomba msaada Kenya na siyo kinyume chake.

Sasa swali langu ni hilo, ni kwa nini nchi ya Kenya imeshindwa kutake off hata baada ya miaka zaidi ya 50 ya capitalism?

Ikumbukwe moja kati ya visingizio/sababu ya tunazotoa ya TZ yetu kushindwa kutake-off kwa miaka mingi ni Ujamaa, Ujamaa haukuruhusu accumulation of capital and wealth, lkn Kenya siyo hivyo, ...
 
Vipi ile topic yako Watanzania kushindilia mambo ya Kenya? Mbona kujitega mwenyewe?

Haya Karibuni Wadanganyika kwenye mjadala mwingine wa kudiscuss Kenya.
 
Kwani Russia haikua nchi ya kikomunisti? Mbona bado imeendelea? nchi kuwa capitalist sio sababu ya kuendelea wala nchi kuwa communist sio sababu ya kutoendelea.
 
Kwani Russia haikua nchi ya kikomunisti? Mbona bado imeendelea nchi kuwa capitalist sio sababu ya kuendelea wala nchi kuwa communist sio sababu ya kutoendelea.

Urusi haijaendelea kama ambavyo ilivyopaswa kuwa na hata hayo maendeleo unayoyaona leo hi Urusi yamekuja baada ya kuchukuwa capitalism na kuacha communism, ndiyo maana bado Urusi iko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na Ulaya Magharibi, USA, au hata East Asian!
 
Mlalapo muamkapo,mtembeapo ni kuifikiria kenya tu!
mijitu mna mijimambo,nchi ndogo ya kenya tumewapa kichapo halisi na kuwapiga chenga despite kuwa na challenges here and there
Zidi kutusoma namba kabisaaaaaa!
Sisi ni wale aggressive,yaani wale wasee!
 
Lkn bado haujanisaidia, ningependa kujua sababu ni ipi hata baada ya kuwa na Capitalism kwa zaidi ya miaka 50 lkn bado nchi iko chini tu?
 
Urusi haijaendelea kama ambavyo ilivyopaswa kuwa na hata hayo maendeleo unayoyaona leo hi Urusi yamekuja baada ya kuchukuwa capitalism na kuacha communism, ndiyo maana bado Urusi iko nyuma kimaendeleo ukilinganisha na Ulaya Magharibi, USA, au hata East Asian!
Kwani ulitaka iendeleaje mkuu? Mbona China bado ni communist na ni among the world's biggest economies.
 
Nchi ya Kenya kwangu mimi inanishangaza kwani nashindwa kuelewa ni kwa nini imeshindwa kuwa developed country kama vile Singapore, Korea au hata Malaysia wakati imekuwa ikufuata capitalistic economic system tangu kuanzishwa kwake?

I mean, Kenya haijawahi kuwa na maadui hata tu self imposed sanctions kama vile TZ yetu haijawahi kuwa nazo, Kenya imekuwa ikifanya Biashara hata na AK wakati wa apartheid, SAA ilikuwa inatua Nairobi wkt wa apartheid na kuleta Watalii wa Kikaburu, Kenya ilikuwa upande wa USA na siyo communism kama sisi, sasa ni kwa nini mpaka leo hii bado wana struggle na matatizo yale yale yanayoisumbua TZ, Uganda au Rwanda, Burundi au hata Ethiopia?

Nilishangaa kusoma kwenye Gazeti Raisi wa Kenya amekwenda Cuba kuomba Madaktari kuja kufundisha Wakenya, I mean really, Cuba ni communist country, na imewekewa sanctions na Dunia nzima hata Watalii wengine walikuwa hawaruhusiwi kwenda Cuba na wanategemea cigar tu lkn Kenya nchi yenye capitalism wanakwenda kuomba msaada Cuba, hii imekaaje? Nilitegemea Cuba waje kuomba msaada Kenya na siyo kinyume chake.

Sasa swali langu ni hilo, ni kwa nini nchi ya Kenya imeshindwa kutake off hata baada ya miaka zaidi ya 50 ya capitalism?

Ikumbukwe moja kati ya visingizio/sababu ya tunazotoa ya TZ yetu kushindwa kutake-off kwa miaka mingi ni Ujamaa, Ujamaa haukuruhusu accumulation of capital and wealth, lkn Kenya siyo hivyo, ...
Singapore,S . Korea na Malaysia siku hizi nazo zipo group la developed countries?
 
Cha ajabu tulikuwa tunashindana kiuchumi tulivyokuwa chini ya Ujamaa yaabi GDP yetu ilikuwa juu yao! Wakati mwingine nafikiri free market ilitupeleka nyuma tungekaza kama Uchina na Ethiopia.

Njooni mjibu huku, topic murua!

nomasana, sam999, NairobiWalker, hbuyosh, msemakweli, simplemind, Kimweri, Bulldog, MK254, Kafrican, Ngongo, Ab_Titchaz, mtanganyika mpya, JokaKuu, Ngongo, Askari Kanzu, Dhuks, Yule-Msee, waltham, Mzee, mombasite gabriel, Juakali1980, Boda254, mwaswast, MwendaOmo
, Iconoclastes, oneflash, Kambalanick, 1 Africa, saadeque, burukenge, nyangau mkenya, Teen-Upperhill Nairobi, kadoda11
 
Nafikiri huu mjadala unaweza kutumika kwa manufaa mapana sana ya kitaifa. Ni kweli mara nyingi ujamaa na kujitegemea ni sera zinazopigiwa kelele na wengi kwamba ndio zimachangia Tanzania kuwa kwenye huu mdororo.

Ikiaminika kwamba ubepari/ukabaila (sijui kama nimepatia) ni sera zilizoleta maendeleo kwa nchi nyingi hasa za ulaya na magharibi.

Tujikite kwenye kuchambua kwanza, Je, ni kweli ujamaa ni sera za kutokufanikiwa na kila walioegemea capitalism wanafanikiwa?

Ndugu zetu Kenya na wengine waliochagua capitalism wamekosea wapi? Na Cuba ni kipi tofauti amefanya akaendelea licha ya kuwa mjamaa?

Tanzania tuna kipi cha kubadili au koboresha kutokana na majibu ya hayo maswali ya juu?
 
Kwani ulitaka iendeleaje mkuu? Mbona China bado ni communist na ni among the world's biggest economies.

Tofautisha kuwa na big economy ambapo ni volume tu kwa sababu ya idadi kubwa ya watu na per capital income, hivyo ni vitu viwili tofauti, kwa ubora wa maisha yaani kipato cha Mwananchi mmoja mmoja hata Malaysia ni tajiri kuliko Uchina.
Hivyo Uchina bado ni nchi masikini ukilinganisha na capitalistic countries kama Singapore, Taiwani, Korea, Japan, USA au Ulaya Magharibi!
 
Singapore,S . Korea na Malaysia siku hizi nazo zipo group la developed countries?

Ndiyo sina uhakika na Malaysia, lkn Taiwani, Singapore, Korea Kusini ni developed countries, kwanza Singapore ni nchi ya tatu kwa utajiri Duniani!
 
Haha do your research well, Singapore,Taiwan zipo juu kwa kipato cha raia mmoja mmoja ukilinganisha na China? Mfano mzuri ni USA it has a big economy ukilinganisha na Russia lakini individually matajiri ni wachache sana ukilinginisha na wananchi wenye kipato cha kati yaani there is a very big gap wakati Russia wananchi matajiri ni wengi as well as wananchi wenye kipato cha kati yani kwa kiasi kuna balance.
 
Ndiyo sina uhakika na Malaysia, lkn Taiwani, Singapore, Korea Kusini ni developed countries, kwanza Singapore ni nchi ya tatu kwa utajiri Duniani!
[emoji1] [emoji1] [emoji1] utajiri gani unaoongelea hapa kwa upande wa Singapore?
 
Kenya kuna matatizo ukabila umewafanya Kenya kuendelea kuogelea katika dimbwi la umasikini tatizo ni walio nacho hujiangalia wao na wamekosa ubunifu wa elimu ya kumukomboa mwanainchi katika fikira finyu ndio maana utamkuta kila mkenya akili yake inafikiria America na Europe lakini mwili wake na maisha yapo Kenya Africa.

Tatizo wa Kenya wamelala sana wamejisahau na wasipo gutuka watajikuta hata Burundi imewapita binafsi sipendi maisha ya wa Kenya wanaishi pretend kama wazungu.

Kenya hawawezi kuendelea tena wamejisahau
 
Kenyans r generally lazy people, imagine 50 years after independence they can not even sustain themselves with food! Look at who r behind their tea n flower farms! Whitemen n few politicians while majority of them specialise on being tenants at their estates.

Feudalism at its highest peak. Believe me if a random survey is to be conducted here in JF, it will yield a null result for those with a 30 acres land to cultivate. But they make a lot of noises in here. Magufuli knows how to fix them he is on a mission to erase all their middlemen way of surviving in an economic pyramid.
 
Haha do your research well, Singapore,Taiwan zipo juu kwa kipato cha raia mmoja mmoja ukilinganisha na China? Mfano mzuri ni USA it has a big economy ukilinganisha na Russia lakini individually matajiri ni wachache sana ukilinginisha na wananchi wenye kipato cha kati yaani there is a very big gap wakati Russia wananchi matajiri ni wengi as well as wananchi wenye kipato cha kati yani kwa kiasi kuna balance.
Kenya ukabila unawatafuna na hamtaweza kuendelea uchumi wenu unadidimia, maisha ya wachache ndio yenye unafuu 65% ni masikini huwezi kuwa una kundi kubwa la walipa kodi masikini ukategemea uchumi kuimarika Kenya mjitafakari anguko lenu linazidi.
 
Mlalapo muamkapo,mtembeapo ni kuifikiria kenya tu!
mijitu mna mijimambo,nchi ndogo ya kenya tumewapa kichapo halisi na kuwapiga chenga despite kuwa na challenges here and there
Zidi kutusoma namba kabisaaaaaa!
Sisi ni wale aggressive,yaani wale wasee!
Hii ni Kenyan Forum, acha kukimbia hoja kwa kusema watu walalapo waamkapo wanawaza kenya.

Watu wanaoonekana jukwaa hili ni fraction ndogo sana watanzania waliopo jf.
 
Kwa nchi kuendelea lazima iwe na majirani wanaoendana kwa kasi pamoja, Kenya imezungukwa na mataifa ambayo yote yameorodheshwa kwenye LDC, yaani maskini wa kutupwa.
Kenya imejaribu sana maana ni kainchi kadogo, nusu yake kame tupu, bila madini lakini kameshinda mijitu kama DRC na Tanzania
 
Back
Top Bottom