Mada za kihivi huwa unazianzisha, ukijibiwa unatoweka halafu baada ya miezi michache unaibuka tena na swali lile lile, na ndio unaona Wakenya hawahangaiki kukujibu maana ushajibiwa mara nyingi tu.
Inafaa ikuingie kwamba mfumo wa nchi sio sababu pekee ambayo inawezesha nchi kuboreka kiuchumi, cha msingi na muhimu ni uwezo wa wananchi wa nchi husika kujituma. Afrika hii, hata majirani zenu wote akina Zambia, Malawi n.k. wote walikumbatia ubepari, lakini bado mnaorodheshwa pamoja kama mataifa maskini wa kutupwa dunia hii.
Ukiangalia hata Uganda ambayo haina eneo kame kama ilivyo Kenya, pia mpo kwenye kundi moja. Nchi yetu ni mfano wa kuigwa, maana nusu yake ni kame tupu, jangwa lakini hatupo nanyi kwenye kundi la maskini. Nyie kilichowaponza, ni kwamba hamkuuelewa mfumo wa communism, ilikua ni kazi ya mtu mmoja tu Nyerere ambaye hakutaka kushauriwa, mkaishia kuwa wavivu na wazembe hadi liinchi likubwa, yaani muungano wa nchi mbili zenye kila aina ya raslimali lakini maskini hadi noma.
Siri ya Kenya ni kujituma, huwa tunajituma kwa kwenda mbele, ni kweli hatuwezi kujilinganisha na Japan, wapo mbele yetu, ila inafaa uelewe wale walianza mapinduzi ya viwanda (industrial revolution) mwaka wa 1870 wakati huku tukiwa gizani. Na mataifa yote yaliyowazunguka walipata huo mwanga, lakini sisi huku tumezungukwa na mivivu.