Kwa nini kimeitwa 'kibao cha mbuzi' na si neno jingine?

Kwa nini kimeitwa 'kibao cha mbuzi' na si neno jingine?

Murano

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Posts
2,056
Reaction score
1,102
Habari zenu wanajamvi wa jukwaa hili la lugha, husika na kichwa cha habari hapo juu, why waungwana waliamua kukiita kibao cha mbuzi na si cha nazi? mbuzi katumikaje hapo?

Nitashukuru kwa majibu/maoni yenu.

TAFADHALI: usijibu kwa kejeli au matusi,kama hujaelewea ipite post kama ilivyo

nawasilisha
 
Swali zuri hili hata mimi nimetafakari kwa kina lakini sikupata jibu. Jina muafaka lingestahili kuwa kibao cha kukunia nazi.
 
...point of correction,kinaitwa mbuzi,hili la kibao cha mbuzi la kichina zaidi...
 
Habari zenu wanajamvi wa jukwaa hili la lugha, husika na kichwa cha habari hapo juu, why waungwana waliamua kukiita kibao cha mbuzi na si cha nazi? mbuzi katumikaje hapo?

Nitashukuru kwa majibu/maoni yenu.

TAFADHALI: usijibu kwa kejeli au matusi,kama hujaelewea ipite post kama ilivyo

nawasilisha



Kwa sas majina yote mawili yanatumika. Kimsingi utoaji majina wa vitu si kwamba watu wanaokota popote la hasha! Nitakupa mdokezo wa njia tatu alafu utatafakari ni hipi iliyotumika:-

1-msamiati uendana sambamba na maumbile ya kitajwa, hii huangalia mfanano wa kifaa na jina husika. Kwahyo ukiangalia mbuzi haina nasaba ya karibu sana mbizi mnyama?

2-matumizi ya kifaa husika, mathalani mkatumia neno kibao ya nazi.

3-Pia huwa kunaangaliwa lugha za kibantu kama kipo kifaa kama hicho katika kabila fulan na kukipajina kifaa hicho kifaa kipya
Angalizo, kila kitu hakijakamilika hivyo kama jina kibao cha nazi...wapo watu wangehoj pia kuwa kwani kinatengenezwa na vifuu vya nazi au mnazi.
Ahsante.
 
Shukrani kwa swali lako angalau nimejifunza kuhusu kibao chambuzi.

Siwezi kuwalaumu sana wanaokiita kibao cha mbuzi kwa sababu wanalitumia sana hilo neno kwenye kutamka na sio kuandika, kama tulivyoona ukitamka bila kuona linavyoandikwa ni rahisi sana kukiita kibao cha mbuzi kuliko kibao chambuzi.
 
na kimepewa jina hilo kutokana na jinsi kinavyofanya kazi ikiwa ni mojawapo ya mbinu unayotumika kuviita vitu majina katika lugha yetu
 
kiswahli bhana, sometimes kinafurahisha sana
 
Back
Top Bottom