Kwa nini Kipindi cha uchumi TBC lugha ni kiingereza?

Kwa nini Kipindi cha uchumi TBC lugha ni kiingereza?

kluger

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
2,093
Reaction score
1,899
Habari,

Leo baada ya king'amuzi changu kuisha salio nimebakiwa na channel moja ya kutazama, si nyingine bali TBC.
Naona hapa kipindi cha "this week in perspective". Wanajadili mambo mazuri ya hali ya uchumi hivi sasa hapa nchini.

Binafsi lugha hii wanayotumia yaani Kiingereza hainipi shida, ila nimejaribu kuwaza wazee wa vijijini kule, na vijana wenzangu wengi tu nina hakika muda huu watakuwa wanaangalia yaliyojiri kwnye fiesta.

Swali langu hapa kwenda uongozi WA TBC, je ni kwa nini kipindi hiki kipo kwa lugha ya kigeni ili hali hata rais wetu anatumia zaidi lugha ya taifa, yaani kiswahili?
Hamuoni kiswahili kingekuwa bora zaidi kufikisha ujumbe kwa hadhira kubwa zaidi hasa kuhusu mambo haya ya uchumi ambao hali yake inakanganya wengi ?

Uchumi unakuwa lakini haufanyi vizuri mifukoni mwetu walio wengi, nondo hizi zinazoshushwa hapa zingesaidia wengi kuelewa hali ya uchumi wetu kwa sasa!.

Ahsante, jaribuni kufikiria juu ya hili.
 
Kwasababu watanzania Elimu duni ccm wanawafumba macho mkapa kawaita wapumbavu


Swissme
 
Back
Top Bottom