Je waliofanya huo uvamizi wa hovyo huko Itaq wameshachukuliwa hatua au imeishia kwenye kulaani tuAfghanistan Taliban waliambiwa wawakabidhi Osama na Al Qaeda yake waliokiri kufanya ugaidi wa September 11 lakini Taliban walikataa, walionza kutangaza vita walikuwa ni Al Qaeda.
Syria imeingia vitani katika wimbi la Araba spring kwa sababu ya udikteta wa Bashar Al-Asaad, majeshi ya nje yalienda kutuliza hali iliyochafukia na ikiwezekana kumng'oa kwa sababu yeye na utawala wa miaka 40 wa familika yake ndio chanzo cha machafuko Syria.
Uvamizi wa Iraq ulikuwa wa hovyo na ulipingiwa na watu wengi hata huko West kwenyewe mfano kina Nancy Pelosi, Bernie Sanders, Jeremy Corbyn hadi na baadhi ya wakuu wa majeshi wa zamani.
Na kama majeshi ya nje yanaona ni vema kuingilia nchi nyingine ili kutetea raia wa nchi husika
Mbona hawaendi Congo,Msumbiji ili wasaidie wananchi wanaoteseka maeneo hayo
Lakini pia mbona hayo majeshi hayajaingia moja kwa moja pale Ukraine ili wamsaidie kuliko kuishia kulaani na kuweka vikwazo.