izzo
JF-Expert Member
- May 31, 2015
- 2,812
- 6,409
Tunapozungumzia uchumi unakuwa tunazungumzuia makusanyo si matumizi, ndio maana uchumi unapimwa kwa GDP (Gross domestic product) kwa maana pato la taifa maana ya pato ni kile unachokusanya aidha kwa kuuza au kutoza au kwa maana nyingine ni thamani ya bidhaa au huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kwa kipindi cha mwaka mzima GDP ya nchi inapimwa kwa C + I + G + (X-M)
C=Customer Spending
Haya ni matumizi au manunuzi tunayofanya kila siku katika soko la bidhaa(Product market)
I= Investments on Capital Goods
Huu ni uwekezaji unaofanywa ndani ya nchi aidha na wawekezaji au serikali
G = Government Spending
Haya ni jumla ya Matumizi ya Serikali kwa Bidhaa na Huduma za Mwisho
X=Exports na M=Import
Uchumi wa Dunia kwa sasa ni zaidi ya US$78.28 trillion huku PPP (purchasing power parity) ikiwa ni zaidi ya US$107.5 trillion sasa uchumi wa Africa yote ni US$3.3 trillion huku PPP ikiwa ni US$ 6.757 trillion ukiangalia uchumi wa bara zima la Africa katika Dunia ni 4.2% kiwango ambacho ni kidogo sana pamoja na hayo kuna vitu vinaangaliwa pia
A Uchumi
B Maendeleo
C Nguvu ya sarafu
Katika vitu vitatu vinavyoendesha dunia tukianzia Uchumi nchi nyingi kwa sasa zimejikita katika uchumi wa foreign direct investment (FDI) na tukisema Top 13 Duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi 2014-2017kwa mujibu wa WB na IMF namba (13) China 7.10% (12) Rwanda 7.12% (11) Tanzania 7.15% (10) Mozambique 7.30% (9)Bhutan 7.55% (8) India 7.57% (7)Papua New Guinea 7.60% (6)Cote d'Ivoire 7.80% (5)Uzbekistan 7.87% (4) Myanmar/Burma 8.30% (3)Democratic Republic of the Congo 8.62% (2) Turkmenistan 9.07% (1) Ethiopia 9.70%
Ukiangalia nchi zinazofanya vizuri kiuchumi zinatoka mabara mawili yani ASIA na AFRICA ,pia Africa tumetoa nchi 6 tukiangalia upande mwingine factor zingine yani
MAENDELEO na NGUVU YA SARAFU
Maendeleo bado yamebaki Ulaya na America pia na nduvu za sarafu bado wazungu wanazizibiti kwa kiwango kikubwa sana. Swali linabaki pamoja na kukua kwa kasi ya uchumi wa Africa bado hakuendani na maisha ya wanachi walio wengi ukilinganisha na nchi zingine za Asia ambazo ni growing economies tatizo ni nini kwa Africa? kwa kuwa Africa sababu zinafanana hapa tunaiangazia Tanzania
TANZANIA
Tanzania ni nchi ambayo kwa kipindi cha miaka 15 uchumi wake umekuwa ukikua na kuweza kufikia record ya 7.7% na kushuka kidogo mpaka 6.8% so kwa mwaka Tanzania uchumi wake umekuwa ukikua kwa kiwango cha 6-7%
Watanzania 75% wanategemea kilimo kuendesha maisha yao, pia zaidi ya 70% ya watanzania wanaishi chini ya kipato cha dola 2 kwa siku huku watanzania milioni 12 wakiishi kwenye umasikini na watanzania million 4 wakiishi kwenye ufukara yani kiwango kikubwa kabisa cha umasikini je tatizo lipo wapi na wakati kwa mwaka uchumi unakuwa kwa kiwango cha 6-7%?
BOT
Bank kuu ya Tanzania ndio tumaini pekee la nchi katika maswala yote ya kiuchumi huku kazi ya Bank kuu ya Tanzania ni
1 Print money
2 Control supply of money
3 Set the Reserve Requirement
4 Influence Interest Rates
5 Engage in Open Market Operations
6 Control inflation
Ukiangalia katika maswala ya kifedha Tanzania ni nchi ya pili Africa baada ya South Africa kuwa na taasisi nyingi za maswala ya kifedha , tukiangalia mzunguko wa fedha kama engine kuu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja
Mzunguko unatakiwa kuendana na vitu hv
Money supply
price level
National income na Velocity of circulation
kitu ambacho kwa Tanzania hakikuwapo ikapelekea mpaka interest rates kufikia 21.42% na inflation ya 5.6% kwa nchi ambayo hakuna vita na wala hakuna vikwazo vya uchumi ni hatari sana pamoja na kuwa na taasisi nyingi za kifedha lakini ilifikia kipindi interest rates kufikia 21.42% ni hatari hata uchumi ukikua lakini taasisi zinazowezesha wananchi kuwa na access ya uchumi wao kuwa na riba kubwa ni tatizo, swala hili tayari linamwathiri mwananchi wa kawaida moja kwa moja chumi nyingi zilizoendelea Duniani zinabebwa na sector ya kifedha hasa Banks
Mfano China kupitia Banks zake za BANK OF CHINA,AGRICULTURAL BANK OF CHINA,CHINA CONSTRUCTION BANK na INDUSTRIAL AND COMMERCIAL BANK kwa pamoja wana hifadhi ya dola 10.68 Trillion fedha ambayo ni zaidi ya uchumi wa nchi zote duniani kasoro US na China wenyewe na ndio wawekezaji wakubwa wa miradi mbalimbali ya foreign direct investment (FDI) so unaweza kuona sector ya kifedha ikiwa strong inaweza kusaidia serikali lakini serikali nying za Africa zinataka zenyewe kumiliki uchumi kitu ambacho faida yake kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana je tumekosea wapi?
Zipo sababu kama 15 ambazo zinafanya nchi za Africa pamoja na kupanda kwa chumi zao lakini maisha ya wananchi wao bado yako chini
1 UCHUMI WA AFRICA UNASHIKILIWA NA WAGENI
Ninaposema chumi zimeshikiliwa na wageni namaanisha zile Economic booster za uchumi bado ziko mikononi mwa wageni Mfano ukiangalia sector ambazo ndizo zinafanya uchumi wa nchi nyingi za Africa kukua ni
1 Usafirishaji
2 Utalii
3 Mawasiliano
4 Banking
5 Madini
Ukiangalia sector hizo kwa Africa zinafanywa na wawekezaji kutoka nje, na bahati mbaya sana makampuni makubwa yanayofanya biashara hizo yanajulikana kwa umafia wao wa kukwepa kodi na matumizi makubwa ya kutumia rushwa wanapotaka jambo lao, pia ni kazi ambazo zinachukua watu wachache sana kama nguvu kazi (wafanyakazi) so watakao kuwa na access na kazi hizo ni watu wachache na wasomi tu tukumbuke 90% ya waafrica si wasomi ni watu wenye elimu ya kawaida tu, pia fedha zinazopatikana katika shughuli hizo au uwekezaji huo zinapelekwa nje ya nchi hazibaki nchini kwa ajili ya kuingia katiaka mzunguko wa fedha wa nchi ulipo uwekezaji bali zinakwenda kuingia katika mzunguko wa nchi anapotoka mwekezaji.
2 SELIKARI NYING ZA AFRICA ZIMEJIKITA KWENYE UCHUMI WA TAX COLLECTION TU
Itaendelea........