Kwa nini kupanda kwa uchumi wa nchi nyingi za Africa ikiwamo Tanzania hakuendani na maisha ya wananchi?

izzo

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
2,812
Reaction score
6,409
Tunapozungumzia uchumi unakuwa tunazungumzuia makusanyo si matumizi, ndio maana uchumi unapimwa kwa GDP (Gross domestic product) kwa maana pato la taifa maana ya pato ni kile unachokusanya aidha kwa kuuza au kutoza au kwa maana nyingine ni thamani ya bidhaa au huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kwa kipindi cha mwaka mzima GDP ya nchi inapimwa kwa C + I + G + (X-M)
C=Customer Spending
Haya ni matumizi au manunuzi tunayofanya kila siku katika soko la bidhaa(Product market)

I= Investments on Capital Goods
Huu ni uwekezaji unaofanywa ndani ya nchi aidha na wawekezaji au serikali

G = Government Spending
Haya ni jumla ya Matumizi ya Serikali kwa Bidhaa na Huduma za Mwisho
X=Exports na M=Import

Uchumi wa Dunia kwa sasa ni zaidi ya US$78.28 trillion huku PPP (purchasing power parity) ikiwa ni zaidi ya US$107.5 trillion sasa uchumi wa Africa yote ni US$3.3 trillion huku PPP ikiwa ni US$ 6.757 trillion ukiangalia uchumi wa bara zima la Africa katika Dunia ni 4.2% kiwango ambacho ni kidogo sana pamoja na hayo kuna vitu vinaangaliwa pia
A Uchumi
B Maendeleo
C Nguvu ya sarafu
Katika vitu vitatu vinavyoendesha dunia tukianzia Uchumi nchi nyingi kwa sasa zimejikita katika uchumi wa foreign direct investment (FDI) na tukisema Top 13 Duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi 2014-2017kwa mujibu wa WB na IMF namba (13) China 7.10% (12) Rwanda 7.12% (11) Tanzania 7.15% (10) Mozambique 7.30% (9)Bhutan 7.55% (8) India 7.57% (7)Papua New Guinea 7.60% (6)Cote d'Ivoire 7.80% (5)Uzbekistan 7.87% (4) Myanmar/Burma 8.30% (3)Democratic Republic of the Congo 8.62% (2) Turkmenistan 9.07% (1) Ethiopia 9.70%

Ukiangalia nchi zinazofanya vizuri kiuchumi zinatoka mabara mawili yani ASIA na AFRICA ,pia Africa tumetoa nchi 6 tukiangalia upande mwingine factor zingine yani
MAENDELEO na NGUVU YA SARAFU
Maendeleo bado yamebaki Ulaya na America pia na nduvu za sarafu bado wazungu wanazizibiti kwa kiwango kikubwa sana. Swali linabaki pamoja na kukua kwa kasi ya uchumi wa Africa bado hakuendani na maisha ya wanachi walio wengi ukilinganisha na nchi zingine za Asia ambazo ni growing economies tatizo ni nini kwa Africa? kwa kuwa Africa sababu zinafanana hapa tunaiangazia Tanzania

TANZANIA
Tanzania ni nchi ambayo kwa kipindi cha miaka 15 uchumi wake umekuwa ukikua na kuweza kufikia record ya 7.7% na kushuka kidogo mpaka 6.8% so kwa mwaka Tanzania uchumi wake umekuwa ukikua kwa kiwango cha 6-7%

Watanzania 75% wanategemea kilimo kuendesha maisha yao, pia zaidi ya 70% ya watanzania wanaishi chini ya kipato cha dola 2 kwa siku huku watanzania milioni 12 wakiishi kwenye umasikini na watanzania million 4 wakiishi kwenye ufukara yani kiwango kikubwa kabisa cha umasikini je tatizo lipo wapi na wakati kwa mwaka uchumi unakuwa kwa kiwango cha 6-7%?

BOT
Bank kuu ya Tanzania ndio tumaini pekee la nchi katika maswala yote ya kiuchumi huku kazi ya Bank kuu ya Tanzania ni
1 Print money
2 Control supply of money
3 Set the Reserve Requirement
4 Influence Interest Rates
5 Engage in Open Market Operations
6 Control inflation

Ukiangalia katika maswala ya kifedha Tanzania ni nchi ya pili Africa baada ya South Africa kuwa na taasisi nyingi za maswala ya kifedha , tukiangalia mzunguko wa fedha kama engine kuu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja
Mzunguko unatakiwa kuendana na vitu hv
Money supply
price level
National income na Velocity of circulation
kitu ambacho kwa Tanzania hakikuwapo ikapelekea mpaka interest rates kufikia 21.42% na inflation ya 5.6% kwa nchi ambayo hakuna vita na wala hakuna vikwazo vya uchumi ni hatari sana pamoja na kuwa na taasisi nyingi za kifedha lakini ilifikia kipindi interest rates kufikia 21.42% ni hatari hata uchumi ukikua lakini taasisi zinazowezesha wananchi kuwa na access ya uchumi wao kuwa na riba kubwa ni tatizo, swala hili tayari linamwathiri mwananchi wa kawaida moja kwa moja chumi nyingi zilizoendelea Duniani zinabebwa na sector ya kifedha hasa Banks

Mfano China kupitia Banks zake za BANK OF CHINA,AGRICULTURAL BANK OF CHINA,CHINA CONSTRUCTION BANK na INDUSTRIAL AND COMMERCIAL BANK kwa pamoja wana hifadhi ya dola 10.68 Trillion fedha ambayo ni zaidi ya uchumi wa nchi zote duniani kasoro US na China wenyewe na ndio wawekezaji wakubwa wa miradi mbalimbali ya foreign direct investment (FDI) so unaweza kuona sector ya kifedha ikiwa strong inaweza kusaidia serikali lakini serikali nying za Africa zinataka zenyewe kumiliki uchumi kitu ambacho faida yake kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana je tumekosea wapi?

Zipo sababu kama 15 ambazo zinafanya nchi za Africa pamoja na kupanda kwa chumi zao lakini maisha ya wananchi wao bado yako chini

1 UCHUMI WA AFRICA UNASHIKILIWA NA WAGENI
Ninaposema chumi zimeshikiliwa na wageni namaanisha zile Economic booster za uchumi bado ziko mikononi mwa wageni Mfano ukiangalia sector ambazo ndizo zinafanya uchumi wa nchi nyingi za Africa kukua ni
1 Usafirishaji
2 Utalii
3 Mawasiliano
4 Banking
5 Madini
Ukiangalia sector hizo kwa Africa zinafanywa na wawekezaji kutoka nje, na bahati mbaya sana makampuni makubwa yanayofanya biashara hizo yanajulikana kwa umafia wao wa kukwepa kodi na matumizi makubwa ya kutumia rushwa wanapotaka jambo lao, pia ni kazi ambazo zinachukua watu wachache sana kama nguvu kazi (wafanyakazi) so watakao kuwa na access na kazi hizo ni watu wachache na wasomi tu tukumbuke 90% ya waafrica si wasomi ni watu wenye elimu ya kawaida tu, pia fedha zinazopatikana katika shughuli hizo au uwekezaji huo zinapelekwa nje ya nchi hazibaki nchini kwa ajili ya kuingia katiaka mzunguko wa fedha wa nchi ulipo uwekezaji bali zinakwenda kuingia katika mzunguko wa nchi anapotoka mwekezaji.

2 SELIKARI NYING ZA AFRICA ZIMEJIKITA KWENYE UCHUMI WA TAX COLLECTION TU
Itaendelea........
 
Tofautisha kati ya economic development na economic growth
Ndugu huwezi kuzungumzia Maendeleo ya kiuchumi bila ya ukuaji wa kiuchumi

Maendeleo ya Kiuchumi(Economic development ) inahusisha kupanda kwa kiwango cha uzalishaji katika uchumi pamoja na maendeleo ya teknolojia, kuboresha viwango vya maisha na kadhalika.lakini yote ufanyika baada ya stage ya kwanza ya Economic Growth (Ukuaji wa kiuchumi) reflection za Economic Growth ndio tunakuja kuziona kwenye Economic development kama final product

Ukuaji wa uchumi (Economic Growth)ni mchakato wa moja kwa moja. Tofauti na maendeleo ya kiuchumi(Economic development), ambayo ni matokeo ya shughuli zinazopangwa na matokeo ya Ukuaji wa Uchumi (Economic Growth)

Ukuaji wa uchumi (Economic Growth) unaweza kupimwa wakati kuna mabadiliko mazuri katika mapato ya kitaifa, ambapo maendeleo ya kiuchumi (Economic development) yanaweza kuonekana wakati kuna ongezeko la mapato halisi ya kitaifa so hatuwezi kuzungumzia maendeleo ya kiuchumi wakati hakuna Ukuaji wa kiuchumi (Economic Growth)

Ukuaji wa uchumi ni mchakato wa muda mfupi unaozingatia ukuaji wa uchumi wa kila mwaka. Lakini ikiwa tunazungumzia juu ya maendeleo ya kiuchumi ni mchakato wa muda mrefu na unahusisha vitu vingi sana ambapo ndipo kinapatikana kitu kinachoitwa Maendeleo kiujumla nimesema kuna vitu vitatu
1 UCHUMI
2 MAENDELEO
3 NGUVU YA SARAFU

Economic development(Maendeleo ya kiuchumi) inatumika katika nchi zinazoendelea ili kupima ubora wa maisha kumbuka katika nchi zinazoendelea hata China na India zipo lakini Economic development(Maendeleo ya kiuchumi) inatumika katika nchi zilizoendelea kupima maendeleo
Ukuaji wa uchumi (Economic Growth) unaweza kupimwa kwa kipindi fulani. Kinyume na maendeleo ya kiuchumi(Economic development) ni mchakato unaoendelea ili uweze kuonekana na unachukua muda mrefu hata China wanazungumzia Ecomonic Growth so huwezi kuleta excuse ya kutokuonekana ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa wakaida eti kwa vile tupo katika Ukuaji wa kiuchumi si Maendeleo ya kiuchumi na kama unasubiri Maendeleo ya kiuchumi hili tuweze kuona matunda ya ukuaji wa kiuchumi Trust me huwezi kuyaona hasa kwa nchi za Kiafrica rabda miaka 200 ijayo
 
Mkuu Malcom Lumumba maoni yako pia ni muhimu katika kujua Tanganyika tumekwama kwapi kiuchumi wakati kila mwaka mnaambiwa uchumi unakua kwa kasi lakini mitaani uchumi unapungua kwa kasi
 
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania
Tanzania.
 
Mkuu kwenye uchumi kuna macro economics na micro economics ni vitu viwili tofauti.
Ni kweli kabisa kwenye nchi nyingi zinazoendelea hakuna balance Kati ya kukuwa Kwa uchumi mkubwa macro economics na uchumi mdogo micro economics.
Uchumi mkubwa ndio hayo mambo ya ukuaji was GDP na uchumi mdogo ndio unahusisha wanachi Kwa ujumla.
Unaambiwa uchumi wa nchi umeongezeka lakini wanachi wengi hasa wanaoishi vijijini bado wanaoishi maisha ya umasikini vilevile au hata zaidi.
Ukitaka kuishuhudia hiyo hali tembelea India, jamaa uchumi wao unakuwa Sana, wanajenga maflyover,Wana matreni ya umeme ( metros), Shirika kubwa la ndege, Hadi nyuklia,na mavitu makubwa makubwa kibao.
Ila India ndio nchi inayoongoza kuwa na masikini wa kiwango kikubwa ( destitute) wengi kulipo nchi nyingi yeyote hapa duniani
 
binafsi sijui sana maswala ya kiuchumi.. nataka hapa liwe darasa kwangu nitoke na angalau kauelewa flani hivi...

nini kinachangia kukua na kushuka kwa thamani ya fedha..?(naombeni jibu lenye kudadavua vyema,haya maswala huwa yananipiga chenga).
Mengine yaja mkinijibu hili
 
Ndugu India wamejitaidi sana kupunguza umasikini kulinganisha na walivyoachwa na mkoloni wao Mwingerezawakati Waingereza wanaondoka India mwaka 1947 waliacha 70% wa wahindi ni masikini wa kutupwa kwa kipindi cha miaka 70 baada ya uhuru India masikini wa kutupwa ni 21.9% 2011-2012 leo ni 12.4% sawa na watu million 172 ya wakazi 1.3 Billion ndio wanaishi chini ya dola1.90 sawa na fedha za India Rs 123.5 ni kweli India ndio inaongoza kuwa na watu wengi masikini ikifatiwa na sub-Saharan Africa 70% ya wahindi wanaishi vijijini tofauti na nchi nying zinazoendelea kama China ambao ni 43.22 %
nimeweka China kutokana na wingi wao zipo sababu kama 8 ambazo zinafanya bado maisha wa wahindi kuwa masikini pamoja na uchumi wao kukua lakini viwango vya umasikini vinapungua kwa kasi sana kulinganisha na umasikini ulioachwa na waingereza mwaka 1947 ambapo wahindi 70% walikuwa ni masikini wa kutupwa now tunazungumzia 12.4% tofauti na Nchi za Africa ukiangalia walivyoachwa na wakoloni pamoja na upunguaji wa umasikini na ukuaji wa chumi zao
 
Tunapozungumzia uchumi unakuwa tunazungumzuia makusanyo si matumizi, ndio maana uchumi unapimwa kwa GDP (Gross domestic product) kwa maana pato la taifa maana ya pato ni kile unachokusanya aidha kwa kuuza au kutoza au kwa maana nyingine ni thamani ya bidhaa au huduma zinazozalishwa ndani ya nchi kwa kipindi cha mwaka mzima GDP ya nchi inapimwa kwa C + I + G + (X-M)
C=Customer Spending
Haya ni matumizi au manunuzi tunayofanya kila siku katika soko la bidhaa(Product market)

I= Investments on Capital Goods
Huu ni uwekezaji unaofanywa ndani ya nchi aidha na wawekezaji au serikali

G = Government Spending
Haya ni jumla ya Matumizi ya Serikali kwa Bidhaa na Huduma za Mwisho
X=Exports na M=Import

Uchumi wa Dunia kwa sasa ni zaidi ya US$78.28 trillion huku PPP (purchasing power parity) ikiwa ni zaidi ya US$107.5 trillion sasa uchumi wa Africa yote ni US$3.3 trillion huku PPP ikiwa ni US$ 6.757 trillion ukiangalia uchumi wa bara zima la Africa katika Dunia ni 4.2% kiwango ambacho ni kidogo sana pamoja na hayo kuna vitu vinaangaliwa pia
A Uchumi
B Maendeleo
C Nguvu ya sarafu
Katika vitu vitatu vinavyoendesha dunia tukianzia Uchumi nchi nyingi kwa sasa zimejikita katika uchumi wa foreign direct investment (FDI) na tukisema Top 13 Duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi 2014-2017kwa mujibu wa WB na IMF namba (13) China 7.10% (12) Rwanda 7.12% (11) Tanzania 7.15% (10) Mozambique 7.30% (9)Bhutan 7.55% (8) India 7.57% (7)Papua New Guinea 7.60% (6)Cote d'Ivoire 7.80% (5)Uzbekistan 7.87% (4) Myanmar/Burma 8.30% (3)Democratic Republic of the Congo 8.62% (2) Turkmenistan 9.07% (1) Ethiopia 9.70%

Ukiangalia nchi zinazofanya vizuri kiuchumi zinatoka mabara mawili yani ASIA na AFRICA ,pia Africa tumetoa nchi 6 tukiangalia upande mwingine factor zingine yani
MAENDELEO na NGUVU YA SARAFU
Maendeleo bado yamebaki Ulaya na America pia na nduvu za sarafu bado wazungu wanazizibiti kwa kiwango kikubwa sana. Swali linabaki pamoja na kukua kwa kasi ya uchumi wa Africa bado hakuendani na maisha ya wanachi walio wengi ukilinganisha na nchi zingine za Asia ambazo ni growing economies tatizo ni nini kwa Africa? kwa kuwa Africa sababu zinafanana hapa tunaiangazia Tanzania

TANZANIA
Tanzania ni nchi ambayo kwa kipindi cha miaka 15 uchumi wake umekuwa ukikua na kuweza kufikia record ya 7.7% na kushuka kidogo mpaka 6.8% so kwa mwaka Tanzania uchumi wake umekuwa ukikua kwa kiwango cha 6-7%

Watanzania 75% wanategemea kilimo kuendesha maisha yao, pia zaidi ya 70% ya watanzania wanaishi chini ya kipato cha dola 2 kwa siku huku watanzania milioni 12 wakiishi kwenye umasikini na watanzania million 4 wakiishi kwenye ufukara yani kiwango kikubwa kabisa cha umasikini je tatizo lipo wapi na wakati kwa mwaka uchumi unakuwa kwa kiwango cha 6-7%?

BOT
Bank kuu ya Tanzania ndio tumaini pekee la nchi katika maswala yote ya kiuchumi huku kazi ya Bank kuu ya Tanzania ni
1 Print money
2 Control supply of money
3 Set the Reserve Requirement
4 Influence Interest Rates
5 Engage in Open Market Operations
6 Control inflation

Ukiangalia katika maswala ya kifedha Tanzania ni nchi ya pili Africa baada ya South Africa kuwa na taasisi nyingi za maswala ya kifedha , tukiangalia mzunguko wa fedha kama engine kuu ya uchumi wa mtu mmoja mmoja
Mzunguko unatakiwa kuendana na vitu hv
Money supply
price level
National income na Velocity of circulation
kitu ambacho kwa Tanzania hakikuwapo ikapelekea mpaka interest rates kufikia 21.42% na inflation ya 5.6% kwa nchi ambayo hakuna vita na wala hakuna vikwazo vya uchumi ni hatari sana pamoja na kuwa na taasisi nyingi za kifedha lakini ilifikia kipindi interest rates kufikia 21.42% ni hatari hata uchumi ukikua lakini taasisi zinazowezesha wananchi kuwa na access ya uchumi wao kuwa na riba kubwa ni tatizo, swala hili tayari linamwathiri mwananchi wa kawaida moja kwa moja chumi nyingi zilizoendelea Duniani zinabebwa na sector ya kifedha hasa Banks

Mfano China kupitia Banks zake za BANK OF CHINA,AGRICULTURAL BANK OF CHINA,CHINA CONSTRUCTION BANK na INDUSTRIAL AND COMMERCIAL BANK kwa pamoja wana hifadhi ya dola 10.68 Trillion fedha ambayo ni zaidi ya uchumi wa nchi zote duniani kasoro US na China wenyewe na ndio wawekezaji wakubwa wa miradi mbalimbali ya foreign direct investment (FDI) so unaweza kuona sector ya kifedha ikiwa strong inaweza kusaidia serikali lakini serikali nying za Africa zinataka zenyewe kumiliki uchumi kitu ambacho faida yake kwa wananchi wa kawaida ni ndogo sana je tumekosea wapi?

Zipo sababu kama 15 ambazo zinafanya nchi za Africa pamoja na kupanda kwa chumi zao lakini maisha ya wananchi wao bado yako chini

1 UCHUMI WA AFRICA UNASHIKILIWA NA WAGENI
Ninaposema chumi zimeshikiliwa na wageni namaanisha zile Economic booster za uchumi bado ziko mikononi mwa wageni Mfano ukiangalia sector ambazo ndizo zinafanya uchumi wa nchi nyingi za Africa kukua ni
1 Usafirishaji
2 Utalii
3 Mawasiliano
4 Banking
5 Madini
Ukiangalia sector hizo kwa Africa zinafanywa na wawekezaji kutoka nje, na bahati mbaya sana makampuni makubwa yanayofanya biashara hizo yanajulikana kwa umafia wao wa kukwepa kodi na matumizi makubwa ya kutumia rushwa wanapotaka jambo lao, pia ni kazi ambazo zinachukua watu wachache sana kama nguvu kazi (wafanyakazi) so watakao kuwa na access na kazi hizo ni watu wachache na wasomi tu tukumbuke 90% ya waafrica si wasomi ni watu wenye elimu ya kawaida tu, pia fedha zinazopatikana katika shughuli hizo au uwekezaji huo zinapelekwa nje ya nchi hazibaki nchini kwa ajili ya kuingia katiaka mzunguko wa fedha wa nchi ulipo uwekezaji bali zinakwenda kuingia katika mzunguko wa nchi anapotoka mwekezaji.

2 SELIKARI NYING ZA AFRICA ZIMEJIKITA KWENYE UCHUMI WA TAX COLLECTION TU
Itaendelea........

Siyo kweli, ukuaji wa Uchumi unawafikia watu wengi tu sema ongezeko la watu linaathiri pia ili uweze kuona mabadiliko ni lazima Uchumi ukuwe kuanzia 10% sasa TZ hatujawahi hata kufikia 9% hivyo bado sana!

Lkn mabadiliko ya Kiuchumi yapo sana tu, mfano sasa hivi Bibi yangu Kijijini anaangalia TV wkt jambo ambalo miaka 10 iliyopita halikuwezekana!
 
Unaposema si kweli unatakiwa kuwepo na sababu za kuelezea hoja yako Uchumi si Siasa ndugu siasa anaweza fanya hata anayejua kusoma na kuandika tu lakini si uchumi ndugu sidhani kama leo bibi yako kuangalia TV kijijini ni jambo la kujisifia na kusema ndio maendeleo ya ukuwaji wa uchumi wa nchi za Kiafrica tokea miaka ya 1960

Miaka ya 1960 uchumi wa Africa na Nchi nying za Asia ulikuwa ni sawa na ukuaji wa uchumi wa nchi za Africa kuanzia mwaka 1961 ndipo Africa tulipoanza kupotea nakupa mifano tu ya ukuaji wa Uchumi wa Africa na nchi za Southeast Asia kama Vietnam, Indonesia, Thailand, Singapore na Malaysia

Mwaka 1961–72 1973–80 1981–90 1991–2000
Africa 1.3 0.7 - 0.9 -1.0
Southeast Asia 3.2 4.9 4.3 6.6

Kumbuka nchi za Southeast tulikuwa nazo sawa kiuchumi miaka ya 1960 sasa ukiangalia ukuaji wao wa kiuchumi toka 1961 mpaka 2000 haujawai kufika 10% hyo unayosema wewe lakini angalia walivyopiga hatua kimaendeleo ukilinganisha na Nchi za Africa wakati wenzetu wanasongambele kiuchumi sisi tunapiga reverse kiuchumi haya sasa uchumi wetu unakua mpaka kufikia kiwango cha 7.12% mpaka 9.70 kwa kipindi cha kuanzia 2014-2017 je refection yake kwa jamii ni kuangalia Tv kijijini kwa bibi yako?

Ukizungumzia idadi ya watu zungumzia pia na idadi ya rasilimali zinazopatikana Africa tofauti na India na China nchi zenye idadi kubwa za watu
 
Labda ungerekebisha swali lako kwanza, isitoshe ubora wa maisha ni relative term hivyo inategemea kwako unamasnisha nini, leo hii USA wanaongelea kwao kuna watu wengi masikini lkn je wanatumia kigezo gani? Masikini wa USA ni upper middle class wa nchi nyingi Duniani!

Hivyo kusema ukuaji wa Uchumi TZ hauleti maendeleo ni relative inategemea na kigezo chako lkn kwangu kuna tofauti kubwa sana kati ya TZ ya leo na ile ya miaka 60’ na kiashiria kimoja wapo ni life expectancy imeongezeka sana na hii maana yake ni kwamba maisha yamekuwa bora, watu pia wameongezeka tulikuwa milioni 18 baada ya Uhuru leo hii tuko zaidi ya milioni 40 maana yake ni kwamba watoto wanaozaliwa wanaweza kukua kinyume na hapo zamani ambapo wengi walikuwa wanakufa kabla ya kufikia utu uzima, sasa hii ni tofauti kubwa sana!
 
Ukifuatilia sana uchumi huu na takwimu za BOT waweza ugua
 
binafsi sijui sana maswala ya kiuchumi.. nataka hapa liwe darasa kwangu nitoke na angalau kauelewa flani hivi...

nini kinachangia kukua na kushuka kwa thamani ya fedha..?(naombeni jibu lenye kudadavua vyema,haya maswala huwa yananipiga chenga).
Mengine yaja mkinijibu hili
Kuna njia mbili za kuona au kujua thamani ya fedha yako
1 Kupitia kubadilisha fedha yako dhidi ya fedha za nchi nyingine
2 Kupitia nguvu yake sokoni hasa katika manunuzi ya bidhaa

Tukizungumzia Exchange rate yaani kiwango ambacho sarafu moja inabadilishwa kuwa sarafu nyingine. Kuna aina mbili za kiwango cha ubadilishaji
1 Fixed exchange rate
2 Flexible exchange rate

Kuanguka na kupanda kwa thamani ya sarafu inaitwa Appreciation na Depreciation kupanda kwa thamani ya fedha au kushuka kwa thamani ya fedha ni kutokana na mahitaji ya soko lenyewe kwani Nguvu ya soko ndio uamua thamani ya bidhaa au huduma sokoni

Yote kwa yote inatokana na Sera za Benki Kuu katika (kudhibiti viwango vya riba, kununua na kuuza fedha katika soko la kimataifa).

Vile vile kushuka kwa thamani husababishwa na kuingia kwa wingi fedha za nje ya nchi ndani ya nchi ambazo upunguza thamani ya sarafu kutokana na mahitaji ya hiyo fedha ya nje ndani ya nchi kitu kingine kinachoshusha thamani ya fedha ni mfumuko wa bei

Kingine uagizaji mkubwa wa bidhaa nje ya nchi(Import) ambapo tunatumia fedha za kigeni kununua hizo bidhaa kifupi zipo sababu nying tu lakini kuna nchi zinaweza kuamua kushusha thamani ya fedha yake yani Devaluation
 
Back
Top Bottom