Ndugu huwezi kuzungumzia Maendeleo ya kiuchumi bila ya ukuaji wa kiuchumi
Maendeleo ya Kiuchumi(Economic development ) inahusisha kupanda kwa kiwango cha uzalishaji katika uchumi pamoja na maendeleo ya teknolojia, kuboresha viwango vya maisha na kadhalika.lakini yote ufanyika baada ya stage ya kwanza ya Economic Growth (Ukuaji wa kiuchumi) reflection za Economic Growth ndio tunakuja kuziona kwenye Economic development kama final product
Ukuaji wa uchumi (Economic Growth)ni mchakato wa moja kwa moja. Tofauti na maendeleo ya kiuchumi(Economic development), ambayo ni matokeo ya shughuli zinazopangwa na matokeo ya Ukuaji wa Uchumi (Economic Growth)
Ukuaji wa uchumi (Economic Growth) unaweza kupimwa wakati kuna mabadiliko mazuri katika mapato ya kitaifa, ambapo maendeleo ya kiuchumi (Economic development) yanaweza kuonekana wakati kuna ongezeko la mapato halisi ya kitaifa so hatuwezi kuzungumzia maendeleo ya kiuchumi wakati hakuna Ukuaji wa kiuchumi (Economic Growth)
Ukuaji wa uchumi ni mchakato wa muda mfupi unaozingatia ukuaji wa uchumi wa kila mwaka. Lakini ikiwa tunazungumzia juu ya maendeleo ya kiuchumi ni mchakato wa muda mrefu na unahusisha vitu vingi sana ambapo ndipo kinapatikana kitu kinachoitwa Maendeleo kiujumla nimesema kuna vitu vitatu
1 UCHUMI
2 MAENDELEO
3 NGUVU YA SARAFU
Economic development(Maendeleo ya kiuchumi) inatumika katika nchi zinazoendelea ili kupima ubora wa maisha kumbuka katika nchi zinazoendelea hata China na India zipo lakini Economic development(Maendeleo ya kiuchumi) inatumika katika nchi zilizoendelea kupima maendeleo
Ukuaji wa uchumi (Economic Growth) unaweza kupimwa kwa kipindi fulani. Kinyume na maendeleo ya kiuchumi(Economic development) ni mchakato unaoendelea ili uweze kuonekana na unachukua muda mrefu hata China wanazungumzia Ecomonic Growth so huwezi kuleta excuse ya kutokuonekana ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa wakaida eti kwa vile tupo katika Ukuaji wa kiuchumi si Maendeleo ya kiuchumi na kama unasubiri Maendeleo ya kiuchumi hili tuweze kuona matunda ya ukuaji wa kiuchumi Trust me huwezi kuyaona hasa kwa nchi za Kiafrica rabda miaka 200 ijayo