Kwa nini Maaskofu waliyakalia kimya mambo haya?

Kwa nini Maaskofu waliyakalia kimya mambo haya?

Walinyang'anywa Shule zao wakakaa kimya

Walinyang'anywa Hospitali zao wakakaa kimya.

Walinyang'anywa vyuo vyao wakakaa kimya.

Leo waliosoma kwenye shule walizonyang'anywa ndio hao hao wanaosema kuwa maaskofu wanachanganya dini na Siasa.

Wale wale wanaotumia Hospitali za Kanisa badala ya kujenga za umma ndio hao hao wanaosema Kanisa linapendelewa na Serikali kupewa ruzuku ya kuziendeshea Hospitali hizo.

Wanasiasa waliodhulumu mali za Kanisa ndiyo hao hao leo wanawaambia Maaskofu wasichanganye Dini na Siasa.

Anayesema hivyo ni Mwanasiasa Muislam akiwa kwenye madhabahu ya Kanisa.

Yeye kimempeleka nini kanisani wakati siyo mkristo? Siyo yeye ndiye anayepeleka Siasa kanisani?
Haya yote umeyaandika kwa sababu tu wametoa maoni yao kukosoa BP World? Suppose wangesema ni mkataba safi usio na mawaa, ungesema nini?
 
Back
Top Bottom