Kwa nini mashabiki wa Yanga wanaiponda Simba

han2710

Member
Joined
Aug 5, 2016
Posts
41
Reaction score
17
Hivi karibuni kumetokea mijadala mitaani ikihusisha mashabiki wa klabu ya simba pamoja na yanga katika maswala ya ubadilishaji wa mfumo wa uendeshaji wa timu. Lakini klabu ya simba hapo jana kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Haji Manara kwamba kimsingi klabu yao imekubaliana na maamuzi ya wanachama yaliyotolewa kwenye kikao kilichofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba wanaitaji mabadiliko, lakini jambo la kuchekesha ni pale mashabiki wa yanga huku mitaani wakiwa wanawaponda simba kwa kuwakashifu kwamba wameuza timu na kuwaambia wajiandae kwa vipigo. Sasa nn tatizo la yanga kwa simba, maana wao mpaka sasa mchakato wao wa kukodisha haujafika tamati.
 
kwa sababu simba wanaiponda yanga
 
Walikua wanaongea hivyo wakati hawajui nini kilikua akilini mwa muhindi.. walisahau misemo hii ya wa wahenga;
1. Usitukane mamba kabla ya hujavuka MTO.
2. Umejifungua salama, usifute namba za wakunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…