han2710
Member
- Aug 5, 2016
- 41
- 17
Hivi karibuni kumetokea mijadala mitaani ikihusisha mashabiki wa klabu ya simba pamoja na yanga katika maswala ya ubadilishaji wa mfumo wa uendeshaji wa timu. Lakini klabu ya simba hapo jana kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Haji Manara kwamba kimsingi klabu yao imekubaliana na maamuzi ya wanachama yaliyotolewa kwenye kikao kilichofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita kwamba wanaitaji mabadiliko, lakini jambo la kuchekesha ni pale mashabiki wa yanga huku mitaani wakiwa wanawaponda simba kwa kuwakashifu kwamba wameuza timu na kuwaambia wajiandae kwa vipigo. Sasa nn tatizo la yanga kwa simba, maana wao mpaka sasa mchakato wao wa kukodisha haujafika tamati.