Kwa nini matumizi ya mabomu ya machozi viwanjani yanataka kuhalalishwa? Mara ya pili mfululizo mechi za Simba yanapigwa

Kwa nini matumizi ya mabomu ya machozi viwanjani yanataka kuhalalishwa? Mara ya pili mfululizo mechi za Simba yanapigwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Hivi ni kwamba Polisi wanataka kuhalalisha matumizi ya mabomu ya mchozi viwanjani? kwamba kulikuwa na tukio hatari la kushindwa kuwadhibiti mashabiki mpaka mtumie nguvu kiasi hicho hadi kupiga abomu kuwtawanya mashabiki ambao wamelipa pesa kwenda uwanjani kutazama mchezo?

Haya mpaka lini? Ni mara ya pili mfululizo yanapigwa mabomu, mara ya kwanza ni mechi kati ya Simba na TRA United iliyoahirishwa kwa kushindwa kuchezwa kisa uwanja umejaa maji kwa mvua kubwa, leo tena machi 1 226 uwanja wa CCM Kirumba mabomu ya machozi yanapigwa kwa sababu mashabiki wameonesha hasira dhidi ya waamuzi wakimtuhumu kutowatendea haki na kuanza kurusha chupa za maji, hivi hakukua na njia ya kumlinda mwamuzi na kumtoa uwanjani mapaka mpige mabomu?

Ona sasa mnasababisha watu wanapoteza fahamu kisa mabomu yenu, hebu badilikeni acheni matumizi ya nguvu bila sababu yaani tangu uchaguzi ni kama hamjui kipi cha kufanya kipi cha kuacha.

Matumizi ya mabomu ya machozi yatasababisha hofu, mashabiki wataacha kwenda viwanjani kwa hofu ya kutokea tafrani na kupata madhara. Tafuteni utaratibu mwingine wa kuwatuliza mashabiki tofauti na huu utamaduni wa mabomu unaonekana kushika kasi sasa.

Pia soma: Mabomu ya machozi yarindima kuwatawanya mashabiki Uwanja wa CCM Kirumba baada ya mchezo kuisha 1-1
 
Polisi wanalinda raia na Mali zao
Huko uwanjani wapo Watanganyika
Sasa mlete fujo
Muumize wengine, polisi watazame tu

Police piga hao mbumbumbu

Leo Kwa mara ya kwanza nawaunga mkono police
 
hapa nchi kama wote tungeungana kwanza kupambania fikra zetu lingekua jambo jema sana, mashabiki wanafanya vitu vya kihuni sana
 
Polisi wakubwa wao wamekuwa wauaji au wenye hamu ya kuua! Na wameanza kuzoea, Sasa watakuja na risasi za moto kama walivyo zoea kwenda walipo Chadema. Tunasema kila siku haya mambo hayafai mnaona ni utani haya kutokea!
 
Simba ndio CHADEMA wa anga za michezo na burudani, wacha wale moshi hadi CCM itakapong'oka.
 
Back
Top Bottom