matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 9,514
- 23,523
Sio Mimi ni Bibilia.
1 Timotheo 2:1-2
Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
Amani haiji KWA kuwaombea watawala na viongozi wafe, wapate ajali, wapatwe mabaya au wapinduliwe.
Hayo ni maombi yanayoongozwa na mashetani. Hata kama wanafanya mabaya kiasi gani. Ni kuomba vibaya.
Amani inakuja KWA kuwaombea haohao wanayotawala wakati huo ili walete amani na utulivu. Kama hautaomba usitegemee nafuu.
Majibu ya maombi yako mikononi mwa Mungu na Sio maelekezo ya Muombaji.
1: Haohao wabaya wanaweza KUWA wema. Mungu akawateka nyara fahamu ZAO wakaanza kutenda sawasawa na Maombi yetu. Mfano Koreshi alitekwa MOYO akavunja KANUNi kandamizi KWA wayahudi akawaruhusu watoke utumwani. Ezra 1:1
2: Mungu kufanya regime change kama alivyomtoa Belshazzar na Kumuwekea Dario. Daniel 5:
3: Anaweza kuruhusu system ya watu wenye USHAURI sahihi na ushawishi KWA watawala wakaanza kusikiliza na mawayo yao ndio yakawa yanaendesha nchi.
Mfano Yusuph Misri. Mwanzo 41:37-44
Hizi ni chache kati ya njia zaidi ya trillioni ambazo Mungu atafanya kuhakikisha analeta amani na utulivu KWA nchi ambayo watu wake wamehamia kuomba vitu hivyo vizuri.
Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi