Kwa nini Mourinho hajawahi kuwa kocha bora wa mwezi msimu huu?

Nokla

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2012
Posts
3,190
Reaction score
1,774
Ukiangalia takwimu Morinho amebena ubingwa wa epl zikiwa zimesalia mechi tatu, pili ametoa mchezaji bora wa mwaka kwa mujibu wa PFA, na pia timu yake Imetoa wachezaji sita wa msimu. Inakuaje kwa jamaa kutopata tuzo ya kocha bora wa mwezi hata mara moja? Au ndio anasubiri kocha wa mwaka? Hii imekaaje au Morinho ni bora kocha na si kocha bora?
 
Kwani ni lazima? Au hamna makocha wengine.
Vigezo na masharti kuzingatiwa, ikitokea kuna mwezi akaperform vizuri atapewa na kama msimu mzima in general amefanya vizuri atapewa kama kocha wa msimu usilazimishe mambo.
 
Hapo kigezo ni input vs output !😆
 
Sasa atachaguliwaje kuwa kocha bora wa mwezi wakati hakuna wakushindana nae,waliobaki ndio wanauwezo wa kushindana wenyewe kwa wenyewe
 
kwa sababu mpira wake unaboa park bus style

Kwa wapinzani lazima waboreke sana! Jamaa kaongoza ligi toka day one! mpaka anabeba taji! wamesubiri ajikwae wakajikwaa wenyewe! Anafanya kazi nzuri ya kuleta raha kwa mashabiki wa darajani na kilio kwa kambi pinzani! Mourinho anabeba taji la kocha bora wa msimu!
 
Sasa atachaguliwaje kuwa kocha bora wa mwezi wakati hakuna wakushindana nae,waliobaki ndio wanauwezo wa kushindana wenyewe kwa wenyewe

Duuu hili jibu poor kabisa? Kwa taarifa yako Morinho kafundisha epl kawa kocha bora kwa mara 3 katika mechi zaidi ya 200, kifupi yule jamaa ni bora kocha
 
Hata kama ukimponda, mataji aliyobeba yanazungumza! Huu ni msimu wake wa pili katika ujio wake wa pili na tayari kubeba taji! Wakati kocha kama Wenger toka amwache kipindi cha kwanza mpaka sasa hajawahi kupata taji la epl! Wote wanaoshiriki EPL miaka nenda rudi hao ndio ma bora kocha!
 
Kwani ni lazima? Au hamna makocha wengine.
Vigezo na masharti kuzingatiwa, ikitokea kuna mwezi akaperform vizuri atapewa na kama msimu mzima in general amefanya vizuri atapewa kama kocha wa msimu usilazimishe mambo.

Hivi unaweza ukaongoza ligi mwanzo hadi mwisho halafu hakuna hata mwezi mmoja timu ilifanya vizuri???
 
Siamini kama hiki kilikuwa kipaumbele kwa Morinho, malengo yake yametimia.

Puljin kachukua ubingwa lakini siyo bora na mbona hushangai hapo.
 
Back
Top Bottom