Kwa nini Msumbiji iliwakabidhi Rwanda majukumu ya kusaidia ulinzi badala ya nchi majirani zake wa SADC?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kutokana na uasi uliochanganyikana na ugaidi kushamiri katika jimbo la Cabo Delgado mwaka 2021 serikali ya Msumbiji baada ya kuzidiwa sana waliingia makubaliano na nchi Rwanda kupeleka majeshi yake katika jimbo hilo kurudisha hali ya utusalama na utulivu.

Baada ya kuona ufanisi mkubwa wa kikosi cha wanajeshi 1,000 waliopelekwa awamu ya kwanza Msumbiji iliendelea kutoa idhini ya wanajeshi wengine kuongezwa zaidi ambapo sasa inakadiriwa wamefika zaidi ya 3000.

Kwa nini Msumbiji haikuomba msaada au kuingia makubaliano kama hayo na majirani zake wa karibu kwenda kusaidia kuweka amani nchini humo?

 
Sadc wamewapa wenyewe uwanja wa Mafunzo kupata uzoefu na pesa, Leo wanateseka.
 
RPF wako serious na discipline, PK hayupo haka Msumbiji Bure, amesaini mikataba kibao makampuni ya Rwanda yapate kazi hapo it's a business.

Like pia yupo hapo strategically - Fanya utafiti utaelewa.

SADC na AU hawapo serious, sio watu wakuwategemea sana kwenye mission serious.
 
Rwanda anataka kuitawala nchi zote za maziwa akuu.. M23 wanasema wana ichukua congo nzima then watajitanua
 
Rwanda walipelekwa na ufaransa ili kulinda mradi wa gesi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…