flyingcrane
JF-Expert Member
- Oct 17, 2014
- 241
- 88
Wakuu nimeliwaza hili jambo kwa muda mrefu sasa. Rais Kaguta Museveni wa Uganda anaheshimika sana nchini Kenya. Yaani anapoongea wakenya humshangilia na kuhisi kama wanahutubiwa na Rais wao. Amekaa na mawaidha mazuri na kuwa na imani na muungano wetu wa EAC (namaanisha CoW).
Wakenya kumkubali Museveni kunadhihirisha ukubaliano wa waganda nchini Kenya hivi basi kutuonyesha mfano mema kwa majirani zetu hapa EAC. Miaka ya Nyuma museveni alidharau wakenya na jeshi letu hivyo wananchi kumkemea hadharani, kuchoma sanamu yake na kung'oa Reli.
Rais wa pili anayehishimiwa Kenya ni Kagame kwa kutembea nasi kimaendeleo na kuheshimiana nasi kimaendeleo. Rais wa tatu asiyejulikana na Kuheshimika ni Jakaya Mrisho Kikwete, licha ya kuwa Tanzania na Kenya zimekuwa rafiki wa toka nitoke, majirani wema sawa tu na ndugu pacha miaka ya nyuma, hali hii imegeuka kwenye hatamu yake na Kikwete sababu ya dharau na ubinafsi, kutoshiriki kimaendeleo na wenzake na kutoa sababu.
Hutawahi sikia Rais Kikwete kapewa nafasi kuhutubia wakenya katika sherehe kubwa, na akipatiwa ruhusa basi atazomewa tu bure, asipokanyaga yeye kwa sherehe kubwa za Kenya hutasikia wakenya wakiongea lakini Museveni ama Kagame asipohudhuria sherehe za Kenya, wakenya watalalamika sana kutosikia sauti za viongozi hawa wanaoongoza kwa matendo.
Chukulia mfano makaribisho ya Museveni na Kagame wanapokuja Kenya hao hukaribishwa vizuri kwa heshima ikilinganishwa na Kikwete anapowasili. Hii tofauti baina ya Kenya na Tanzania ni hatari sana kwa uhusiano wa wananchi kwa mataifa haya mawili.
Tanzania imejitenga na CoW hivi basi kutoshirikishwa kwa miradi mikuu ya pamoja, biashara n.k hili si jambo zuri kwa watanzania Itabidi wabadili sera zao na mataifa jirani bila hii watabaki kuchelewa barabarani wakati basi limewaacha.