Kwa nini naiheshimu baby walker yangu

Kama unajua kusoma na kuandika nilisema "uzoefu unaonesha" mtu alietoka kutembea kwa miguu au kutumia usafiri wa umma hua ana hulka ya kua na matumizi madogo haswa pale unapofikia muda anataka kumiliki chombo cha usafiri ni nadra sana mtu anunue gari lake la kwanza liwe SUV linaloanzia 3000CC 98% ya wanunuzi wa gari kwa mara ya kwanza huanzia kununua magari ya 990CC - 1500 wakizidi sana ni 2000CC na miongoni mwa hayo ya 990-1500CC ni baby walker na baby walker hua zinafujo sana barabarani hauwezi kukubali hilo maana wewe ni miongoni mwa baby walkers wale wanaopenda kuweka mafuta 15,000-20,000 wanataka watembelee na gari wiki nzima kwa mafuta hayo hayo..
 
Wana akili za kitoto sana aisee, hasa kwenye kukazia bila sababu ya msingi ukitaka kumu overtake ndio balaa unaona ghafla ki passo kinapepea kuonyeah kwamba SUV yako si chochote
Hao unaoona Wana fujo...hizo gari hawajanunua wao...pengine walipewa zawadi siku ya graduation..
Mwanaume aliyepambana akanunua gari kwa pesa make lazima awe na nidhamu barabarani
 
Sasa mafuta ya elfu 15 au 20 ukitembelea wiki nzima huoni ni raha[emoji3][emoji16]
 
Sasa mafuta ya elfu 15 au 20 ukitembelea wiki nzima huoni ni raha[emoji3][emoji16]
Si ndo maana mnajitetea wewe na baby walkers wenzako...kwa kiwango chako ni raha kwa wengine ni karaha body size ndogo, kushindwa kwenda popote..etc
 
Si ndo maana mnajitetea wewe na baby walkers wenzako...kwa kiwango chako ni raha kwa wengine ni karaha body size ndogo, kushindwa kwenda popote..etc
Body sizes ni kwa nje tu...Sasa kwa taarifa yako gari Kama spacio ndani ina nafasi nzuri kukiko hata hizo baadhi za suv...
Mfano ukikaa ndani ya Prado TX siti ya nyuma kwa mtu mrefu magoti yanabanwa kuliko kukaa ndani ya spacio
 
Mwenye Passo analikazia Land Cruizer Amazon njia ya kwenda Dodoma.

Hadi ana overtake kabisa, sijui anapata wapi hiyo courage.

Tulicheka sana.
 
I'm proud of my baby Walker coz najua inavyonisaidia...
Hao wenye Prado tuwaache waendeleze dharau....ila mwisho wa siku watambue wote tunauziwa petrol Bei moja[emoji16][emoji16]
Uzuri wa baby walker, trip za mjini huumizi kichwa kama hela ni ya mawazo.

Kwenye safari ndefu na nje ya mji, baby walker mnasumbuka sana.
 
Body sizes ni kwa nje tu...Sasa kwa taarifa yako gari Kama spacio ndani ina nafasi nzuri kukiko hata hizo baadhi za suv...
Mfano ukikaa ndani ya Prado TX siti ya nyuma kwa mtu mrefu magoti yanabanwa kuliko kukaa ndani ya spacio
Hahaha daah kweli wewe ni jambo lingine kwaio unalinganisha Spacio na Prado..Spacio imeacha kutengenezwa tangu 2009 yani unafananisha baskeli na gari mkuu duu kisa siti ya nyuma daah unafeli sana mkuu..sema Prado ya mwaka gani na Spacio ya mwaka gani? Kwamba Spacio ina body size ndogo kwa nje na ndani ni kubwa?
 
Mzee baba tutatengeneza ligi ambayo haina mwisho..
Ok..ok..ok tumeshaelewa unamiliki SUV..

Mimi ninamioiki baby Walker na mker ni NISSAN

Bado hujatuweka wazi maker wa SUV yako ni Nani.. Toyota,Nissan,BMW,VW ,Range au Ford.
Pia ni vyema ukituwekea uliinunua hela ngapi[emoji39][emoji39][emoji39]
 
Pamoja na umuhimu wa kuwa na gari binafsi kama hoja iliyo mezani inavyoelekeza. Hivi sisi kama taifa/ jamii iliyostaarabika , hatuwezi kuwa na mfumo wa usafirishaji wenye hadhi na staha kwa watu wake? mambo yafuatayo yafanyike :-
  1. DART waongeze mabasi.
  2. Abiria wapange foleni, waingie kwa kufuata foleni.
  3. Watu wakae level sit ikibidi excess ya watu wachache wanao askari wa ku-enforce hii kitu.
  4. Mabasi yaanzie katika kati ya route (baadhi), sio lazima yote yaanzie terminal,
  5. Ni kweli tuweke jitahada za kupata hivyo vi-baby walker, lakini tu-demand kupata usafir bora na wenye staha, ni haki yetu, haiingii akilini kuwekeza investement kubwa kwenye ujenzi wa DART kama adha ya usafiri haitatuliwi.
 
Una hoja nzuri Sana
Lakini sirikali yetu si unaijua babaangu..
imejikita katika kuunga mkono hoja na kusifia awamu hii zaidi kuliko kutatua kero za wananchi
 
Tatizo unadhani huwa ni kuwa na usafiri, tatizo ni kuwa na usafiri halafu ukaanza kuvimbiana na wenye magari yao. Ukianza oo hii passo ni noma, speed 180 sijui ina pulling ya kipekee, juzi nimemwacha jamaa ana vx kama kasimama maeneo ya bagamoyo ndo utawaona sasa wajuaji magari wakikuelekeza kwamba una usafiri tu na majina kama unaendesha baby sijui walker yanazaliwa. Ukiwa na gari yako ya kawaida we itumie kwa raha zako, endesha udhaifu wako kwa amani usitake ligi na wengine.
 
#4, 7 & 10 ni FURSA, sio KERO.
 
Na ndo shida yetu kubwa. Una passo halafu unataka recognition badala ya kuwa mpole.
 
Body sizes ni kwa nje tu...Sasa kwa taarifa yako gari Kama spacio ndani ina nafasi nzuri kukiko hata hizo baadhi za suv...
Mfano ukikaa ndani ya Prado TX siti ya nyuma kwa mtu mrefu magoti yanabanwa kuliko kukaa ndani ya spacio
usianze ligi mkuu. hizo gari si za kubishania na SUV, zina uzaifu mwingi sana, watakudharau wanayoyajua magari. we tulia na gari yako usitake recognition.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…