Ndugu zangu...
Picha nilizotupia zinajieleza..
Ukitafakari adha ya usafiri wa jumla mfano mwendo kasi, basi huna budi kuheshimu chombo cha usafiri ambacho mwenyenzi Mungu amekujalia kuwa nacho.
Imezoeleka sana watu wanaomiliki SUV na magari mengine makubwa kuwanyanyapaa wamiliki wa magari madogo mfano passo,vitz, ist, March to mention the few.
Ukitafakari kero za usafiri wa jumuiya, basi utagundua kuwa gari unalomiliki ni la thamani kubwa kwa sababu gari hilo linaweza kukusaidia kuondokana na adha zifuatazo..
1.kuchelewa kazini/kwenye biashara yako
2.kuepuka kero ya kubanana ukizingatia joto la Dar....kwa Arusha msimu wa baridi ni kero kubwa unakuta watu wamejifungia vioo vyote ndani ya daladala..ukipanda tu unahisi kuishiwa pumzi...vioo vyote vinakuwa na ukungu...kama unaugua pumu hapa utakiona cha moto.
3.kero ya kushikwa kiuno na mwanaume mwenzako
4.Kero ya kujikuta umelaza kichwa chako kwenye matiti ya mke wa mtu
5.kero ya kuchanganywa na mifugo ndani ya daladala...hii ipo sana Arusha huko Ngaramtoni na Kikatiti...usishangae kupanda daladala na kondoo wanne mpaka sita.
6.Matusi. wahudumu wengi wa daladala wana lugha chafu sana za kukukera na kukuharibia siku.
7. kijana mdogo wa kiume kujikuta umemshika mama mtu mzima kiuno ili usidondoke. Adha gani hii?
8.Msimu wa joto unaweza kubanana na jamaa ananuka jasho,kikwapa na wakina dada baadhi wananuka mawigi kama gari la kubeba ngozi....kuwaambia huwezi coz huwalipii nauli wewe
9.Kuibiwa....ni swala la kawaida sana kuibiwa simu au wallet wakati unagombania siti
10. Wadada wenye shepu zao unabanana nao unakuta wamekugeuzia makalio.....basi huwa ni tafrani tupu kwa vijana rijali
11.na kero nyingone nyiiingi ambazo sijaziweka hapa
Hitimisho.
Wewe mmiliki wa baby walker usijihisi mnyonge kisa jamaa anaendesha prado. Wote mpo ndani ya gari, wote hamnyeshewi, wote hamuungui na jua, wote mnakula kiyoyozi, wote mnauziwa peteol bei moja
na mwisho kabisa tusidharau chombo cha mtu...hakuna chombo cha moto kinachouzwa laki mbili
View attachment 1067431View attachment 1067435View attachment 1067437View attachment 1067440
Sent using
Jamii Forums mobile app