Kwa nini naiheshimu baby walker yangu

Kwa nini naiheshimu baby walker yangu

Mzee baba tutatengeneza ligi ambayo haina mwisho..
Ok..ok..ok tumeshaelewa unamiliki SUV..

Mimi ninamioiki baby Walker na mker ni NISSAN

Bado hujatuweka wazi maker wa SUV yako ni Nani.. Toyota,Nissan,BMW,VW ,Range au Ford.
Pia ni vyema ukituwekea uliinunua hela ngapi[emoji39][emoji39][emoji39]
Sijanunua ni gari ya urithi..ni 1KZ -TE..bila shaka umeshaelewa
 
Hilux Surf mkuu...najisikia fahari kuendesha baby walker mbili kwa mpigo mkuu..hahaha
[emoji23][emoji23][emoji23]
Mimi ngoja nipambane na cc 1490 ...kwa Sasa naona zinanitosha saana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndugu zangu...
Picha nilizotupia zinajieleza..
Ukitafakari adha ya usafiri wa jumla mfano mwendo kasi, basi huna budi kuheshimu chombo cha usafiri ambacho mwenyenzi Mungu amekujalia kuwa nacho.

Imezoeleka sana watu wanaomiliki SUV na magari mengine makubwa kuwanyanyapaa wamiliki wa magari madogo mfano passo,vitz, ist, March to mention the few.

Ukitafakari kero za usafiri wa jumuiya, basi utagundua kuwa gari unalomiliki ni la thamani kubwa kwa sababu gari hilo linaweza kukusaidia kuondokana na adha zifuatazo..

1.kuchelewa kazini/kwenye biashara yako

2.kuepuka kero ya kubanana ukizingatia joto la Dar....kwa Arusha msimu wa baridi ni kero kubwa unakuta watu wamejifungia vioo vyote ndani ya daladala..ukipanda tu unahisi kuishiwa pumzi...vioo vyote vinakuwa na ukungu...kama unaugua pumu hapa utakiona cha moto.

3.kero ya kushikwa kiuno na mwanaume mwenzako

4.Kero ya kujikuta umelaza kichwa chako kwenye matiti ya mke wa mtu

5.kero ya kuchanganywa na mifugo ndani ya daladala...hii ipo sana Arusha huko Ngaramtoni na Kikatiti...usishangae kupanda daladala na kondoo wanne mpaka sita.

6.Matusi. wahudumu wengi wa daladala wana lugha chafu sana za kukukera na kukuharibia siku.

7. kijana mdogo wa kiume kujikuta umemshika mama mtu mzima kiuno ili usidondoke. Adha gani hii?

8.Msimu wa joto unaweza kubanana na jamaa ananuka jasho,kikwapa na wakina dada baadhi wananuka mawigi kama gari la kubeba ngozi....kuwaambia huwezi coz huwalipii nauli wewe

9.Kuibiwa....ni swala la kawaida sana kuibiwa simu au wallet wakati unagombania siti

10. Wadada wenye shepu zao unabanana nao unakuta wamekugeuzia makalio.....basi huwa ni tafrani tupu kwa vijana rijali

11.na kero nyingone nyiiingi ambazo sijaziweka hapa

Hitimisho.
Wewe mmiliki wa baby walker usijihisi mnyonge kisa jamaa anaendesha prado. Wote mpo ndani ya gari, wote hamnyeshewi, wote hamuungui na jua, wote mnakula kiyoyozi, wote mnauziwa peteol bei moja
na mwisho kabisa tusidharau chombo cha mtu...hakuna chombo cha moto kinachouzwa laki mbili
View attachment 1067431View attachment 1067435View attachment 1067437View attachment 1067440

Sent using Jamii Forums mobile app
Kikatiti...usishangae kupanda daladala na kondoo wanne mpaka sita.[emoji112][emoji112][emoji112][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kikatiti...usishangae kupanda daladala na kondoo wanne mpaka sita.[emoji112][emoji112][emoji112][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]huko kikatiti Kila ijumaa Kuna mnada....daladala zinazokwenda huko zimechoka mpaka tuziita kichaka au banzi..
Huko saa ya kurudi ni kawaida Sana kondoo kupakiwa kwenye buti au wakati mwingine mteja anachukua siti nne za nyuma yanajaa makondoo..

Tunashukuru polisi siku hizi wameingilia Kati
Ilikuwa unapanda daladala unafika home unanuka Kama kondoo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuwa proud na ulichonacho kama uwezo wako ni baby walker shukuru hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom