Maboso
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 5,164
- 5,762
Ni kweli, ni kweli kabisa nimefurahi Diamond kukosa tuzo za MTV. Mnaweza kushangaa lakini huo ndio ukweli wangu. Na ninampongeza kwa dhati kabisa Wizkid kwa kupata tuzo. Lakini kwa nini nafurahi?
1. Namtakia Diamond mafanikio mema Zaidi
Binafsi ninamkubali sana Diamond, na kwangu ndiye mwanamuziki bora Zaidi anayejua kufanya biashara ya muziki. Kukosa kwake tuzo najua hakuwezi kumfanya akate tamaa, bali kutazidi kumfanya awe mbunifu Zaidi na aongeze juhudi. Na hicho ndicho ninachokitaka kutoka kwake, napenda Diamond apate mafanikio.
Jinsi ninavyomfahamu Diamond ni kwamba akikosa kitu huwa hakati tamaa, bali huwa anaongeze nguvu na ubunifu ili kuweza kukishinda kile alichoshindwa. Ni wazi kwamba mwaka huu kafanya nyimbo nzuri na kazi nzuri Zaidi mbele ya jamii. Lakini ni ukweli ulio wazi kwamba hizi kazi hazikuwa sehemu ya kushindania hizo tuzo za mwaka huu.
Bila shaka mwakani zitaingizwa kwenye ushindani. Na wakati zinaingizwa kwenye ushindani, tayari atakuwa ametengeneza popularity na fun base kubwa. Rejea tour ya UK akiwa Neyo inayotarajiwa kuanza kufanyika mwezi December.
2. Apate muda mnzuri wa kujipanga
Diamond amekuwa na mafanikio makubwa katika muziki, na karibu kila tuzo ameshinda ukiacha BET ambayo bado hajafanikiwa pamoja na kwamba amekuwa nominated mara mbili mfululizo. Mfano mnzuri mwaka jana ambapo alifanikiwa kushinda tuzo ya MTV World.
Ni mafanikio makubwa sana ambayo msanii yoyote mwenye vision kubwa anaota kuyafikia. Kukosa tuzo za mwaka huu ni chnagamoto kwake kuweza kujiangalia upya ni wapi ameteleza na ni wapi anapaswa kuongeza nguvu. Maana wakati mwingine kujiona unashinda kila siku kunaweza kujifanya ukalewa sifa na ukajisahau.
3. Kuleta mshikamano na kuachana na hizi team nanii
Ni ukweli ulio wazi kwamba mwaka huu utimu ndio umetuangusha watanzania. Mashabiki hawakuwa na mwamko kabisa wa kupiga kura. Tofauti na miaka iliyopita ambayo tuliona mitandao ya kijamii ilichafuka kwa mabandiko ya kuhimiza upigwaji kura.
Kwa mwaka huu haikuwa hivyo hata kidogo. Watu tumekosa mshikamano. Nadhani ni wakati muafaka wa sisi sote kujifunza kwamba hizi timu siyo zinatujenga bali zinatuangusha taifa nzima. Angalia tuzo za jana, wasanii wetu wote wamekosa kwa sababu ya huu utimu wa kipuuzi. Ni vema tukajifuza kupitia haya makossa.
Nina Imani kubwa na uongozi wa WCB na timu yote kwa ujumla. WCB ni timu inayopenda challenge na isiyokubali kushindwa. Pale inapotokea changamoto kama hii ya kuambulia patupu MAMA awards hukaa chini na kuanza kutafakari wapi wamechemka na wapi waboreshe.
Babu Tale, Mkubwa Fela na kubwa la wazima mic Sallam SK nawakubali sana. Najua mtasoma huu unzi naombeni msianguke bali ongezeni juhudi. Tuna safari ndefu ya kufika kimataifa Zaidi, changamoto ni sehemu ya kujifunza na ndio magurudumu yenyewe ya maisha. Chukua mfano wa pencil ikuvunjika huwa tunachonga kipande kilichopaki na kuendelea kuandika. Maisha yanasonga.
Pamoja na hayo yote. Kwangu mimi Diamond ndiye anabaki kuwa msanii bora kabisa. Na ubora huu unathibitishwa na idadi ya tuzo za nje ya Tanzania alizoshinda tangu alipoanza safari ya muziki mwaka 2009. Kwenye list hapa chini nimeonyesha baadhi ya tunzo tu, ila zipo nyingine ambazo zimetolewa nan chi kama Nigeria, Ghana na nyinginezo ambapo sijaweka hapa.