Kwa nini nzige ni tatizo?

Kwa nini nzige ni tatizo?

Mwanitu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,036
Reaction score
594
Nimekuwa najiuliza,bila majibu,

Kwa nini ujio wa Nzige unachukuliwa kuwa ni tatizo badala ya fursa?unachohitaji ni nyavu ndogo zilizotegeshwa njia watakayopita.technologia ipo ya kujua hilo.

Nzige ni chakula chenye protein nyingi.usindikaji wake ni rahisi,pia chaweza tumika kusagwa na kulishia mifugo. Kwa nini tutumie gharama nyingi, kuwamwagia Sumu na kuharibu chakula. Hilo pia kwa ndege waharibifu jamii ya Quelea Quelea. Afadhali kidogo hao ndege mtasema vigumu kuwanyonyoa. Au tatizo letu ni jadi ya wengine kutokula wadudu?, Nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa na campaign ya kimataifa kuhimiza ulaji wadudu, Sina uhakika iliishia wapi.
 
Nzige anaandiliwaje kuwa Chakula cha binadamu au mifugo.Nikijua naenda kulifanyia kazi.Kuliko kuhangaika na senene kwa ajili ya binadamu au Mende na Funza kwa mifugo,bora niwapate hao Panzi.Lete maujuzi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ni fursa tosha Mkuu ni kama Mimi hapa tayari nina mende kama 1000 hivi na watu wanashangaa ila ngoja nitulie
 
Acha nitege hapa nisubirie maelezo yakinia zaidi kuhusu hawa wadudu.
 
Back
Top Bottom