Kwa nini pilau tu katika x- mass?

Kwa nini pilau tu katika x- mass?

vengu

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
739
Reaction score
535
Wadau katika pitpita zangu mitaani harufu ya chakula ninayoisikia ni pilau tu,jamani kwa nini pilau tu na isiwe chakula kingine?
 
....... pilau? .............................
 
Full kukamua wali wenye miti miti siku za sikukuu sio xmas tu
 
Wadau katika pitpita zangu mitaani harufu ya chakula ninayoisikia ni pilau tu,jamani kwa nini pilau tu na isiwe chakula kingine?

Mkuu kheri ya Christmas.

Pilau ni mchele uliopikwa pamoja na viungo vyote muhimu kuifanya iitwe jina hilo la pilau.

Mchele asili yake ni pwani na ukiwa unapikwa kawaida basi hupikwa pamoja na nazi ambayo nayo upatikana sehemu za pwani mwa nchi yetu.

Kwahio nafikiri kwa wale waishio maeneo yote ya pwani ambao wanafahamu hasa namna ya kupika pilau kama mzee mmoja maarufu dar anaitwa Juma mapilau, ambae hata kwenye sherehe hualikwa kupika chakula hiki adimu basi hutaweza kukosa harufu nzuri ya pilau.

Sehemu zingine mbalimbali duniani huwa na vyakula maalum kama bata mzinga ambae kuokwa tu kwa moto (roasting) pamoja na viazi au kuku pia.

Kwahio hali ndio hiyo mkuu kama umealikwa uende ukale pilau.
 
Hawa wenzetu si unajua mapishi yamewaendea kombo wao chakula walicho kariri ni Pilau tu ,ndio maana wakipata wapwani wakionjeshwa Nazi wanahamia kabisa!!Mambo yote Eid bwana BIRIANI juu ya Mkeka!!!Enzi zile kipindi hiki kila Nyumba ukipita utasikia vinu vinatwangwa,ukiuliza nini "......eti viungo vya Pilau".
 
Hahahaa pilau nomaaa,yan nimevimbiwa!
 
...Ya kuku, mbuzi, kondoo au nyama ya ng'ombe? Hapa kwetu naona itakuwa pilau ya sikukuu yenye nyama ya kongwa.

Biriani mwenziwe ng'ombe 😀

Kongwa ndo mnyama gani? Manake bado kidogo nidhani mko Gambosh mshamkamata kikongwe na kumla nyama 😀
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nyama ya Kongwa inapatikana katika wilaya ya Kongwa kule Dodoma. Kuna ranchi kule wanazofuga ng'ombe, ranchi za Taifa (www.narco.co.tz) ni nyama nzuri sana na ni ile yenye mafuta na pia ni laini sana.

Biriani mwenziwe ng'ombe 😀

Kongwa ndo mnyama gani? Manake bado kidogo nidhani mko Gambosh mshamkamata kikongwe na kumla nyama 😀
 
nayale mavipandepande ya miti (sijui mbao) na mambegu kama vile pine (au papai) wanayoweka eti fasheni yananiuzi!!! Kwetu huku Ugali choma na chang'aa mpaka mapambazuko
 
Nyama ya Kongwa inapatikana katika wilaya ya Kongwa kule Dodoma. Kuna ranchi kule wanazofuga ng'ombe, ranchi za Taifa (www.narco.co.tz) ni nyama nzuri sana na ni ile yenye mafuta na pia ni laini sana.

Ndio tabu ya kuita maeneo majjina kama wanyama! Lol

Basi biriani kwa nyama ya Kongwa ndo mwake kabisa na sharbati pembeni
 
  • Thanks
Reactions: BAK
...lol! biriyani kwa nyama ya kongwa!...unaweza ukajitafuna vidole kwa utamu, pembeni kuna sharbati.

Ndio tabu ya kuita maeneo majjina kama wanyama! Lol

Basi biriani kwa nyama ya Kongwa ndo mwake kabisa na sharbati pembeni
 
Back
Top Bottom