Safety last;2149786]nakubaliana na ww huwa tunawakamilisha watu ktk uhusiano!sasa baya moja linafuta yote yanini kufanya mazuri mengi huku ukijua kosa moja litaharibu kila kitu.. Kweli ubatili upo mwingi tu.
Ni tabia ya mwanadamu kuwa tunapenda mambo mazuri, mabaya hatuyataki. Ndiyo maana ukikosea mwenzi wako anakasirika ila ukifanya jema anafurahi au kuona ni kawaida anadeserve kutendewa yaliyo mema. Level ya chuki au kukasilika nayo ni tofauti kutokana na ukubwa wa kosa, Mengine kama Infidelity kupata msamaha ni kwa mbinde sana hatari ya kuachana ni kubwa zaidi. Hata kama ulikuwa unatenda mema siku zote, kuiba/kutoka nje ya mahusiano yako linafuta kumbukumbu ya mambo mema mlofanya mkiwa pamoja na mkafurahi. Kama ni kosa dogo tu mnaombana msamaha yanaisha. Sidhani kama ni ubatili kwa mwenzako kukasilika na kusahau mazuri ya nyuma, bali ndiyo huruka ya mwanadamu kutopenda kukasilishwa. Binadamu tunapenda mambo mazuri yanayotupa furaha siyo shida. Hatupendi kuumiza mioyo bali kuipa raha.