Kwa nini Rais Kikwete hakumteua prof Shivji kuwa mjumbe kwenye Tume ya Katiba?

Kwa nini Rais Kikwete hakumteua prof Shivji kuwa mjumbe kwenye Tume ya Katiba?

zamlock

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
3,840
Reaction score
659
huyu mzee shivji ameichambua rasimu ya katiba leo kuhusu muundo wa serikali tatu na mengine mengi...huyu mzee angekuwa kwenye tume ya katiba angetoa ushauri mzuri na kwa upande mwingine uwenda angeweza shirikiana na wajumbe wenzake kutupatia katiba nzuri zaidi
 
Angesimamia sheria kama ilivyo taaluma yake..hivyo maslahi binafsi na ya kichama yasingezingatiwa kwenye maoni ndio sababu akawateuwa wale watafuata matakwa na maslahi yyaaaoo.
 
kikwete anapenda kuzungukwa na wajinga hawezi kumteua mtu mwelevu kama Shivji.
 
huyu mzee shivji ameichambua rasimu ya katiba leo kuhusu muundo wa serikali tatu na mengine mengi...huyu mzee angekuwa kwenye tume ya katiba angetoa ushauri mzuri na kwa upande mwingine uwenda angeweza shirikiana na wajumbe wenzake kutupatia katiba nzuri zaidi

Kasemaje? anaunga mkono 3? au 1, au 2?
 
Kajua asingeweza mtumia kuzimisha issue.Kuwepo CCM kunge compromise kinachoitwa "Kuboboea" kwake.SHivji kapewa too much space ya ku manipulate Taifa.

Kunahitajika watu wenye fikra tofauti wasiameme.Bila kuhofia elimu yako au reputation yake.Trust me nae ni km Lipumba tuu.
 
Anaunga mkono 2 kulinda Muungano ila kuna marekebisho kidogo kwenye Bunge!
 
ana mapungufu shivji hawezi ng'ang;aniza serikali MBILI NA NUSU, nilijionaga sijui kupambanua lkn kwa kauli zake nzuri analack mambo kadhaa, bado amauimla kwene baadhi ya mambo...kulazimisha jambo

leo ndio nilimuona ni neo liberali....ingawaje hoja zake zina mshiko ktk mambo kadhaa kama umakini ktk kuuunda kuna hatari kuvunja muungano. na kwamba kweli tulikuwa na serikali 1 zanzibar, 2 ya muungano, na 3 Tanganyika ilikuwa kama msukule
 
Waislam wengi tume ya katiba ndio sababu hajamteua,mzee mtei
 
Anamfahamu vizuri kuwa ni mbabaishaji tuu. Huwa hana jipya ila kujipendekeza kwa utawala uliopo madarakani.
 
huyu mzee shivji ameichambua rasimu ya katiba leo kuhusu muundo wa serikali tatu na mengine mengi...huyu mzee angekuwa kwenye tume ya katiba angetoa ushauri mzuri na kwa upande mwingine uwenda angeweza shirikiana na wajumbe wenzake kutupatia katiba nzuri zaidi
Kitendo cha kumuacha ndiyo kimefanya tupate fursa ya kupata uchambuzi wake makini. Angekuwa ndani kusingekalika kule. Ama angejitoa au ingebidi wakubali ukweli ulivyo kitu ambacho nadhani isingekuwa rahisi. Hivi sasa tumepata mawazo mbadala. Profesa hakutaka kusema tu moja kwa moja. Muungano huu ndio kwa heri tena. Suala kubwa tujue mipaka kati ya Tanganyika na Zanzibar. baada ya hapo Wapemba na wa Unguja watajuana wenyewe kwe wenyewe huko!
 
Anaunga mkono 2 kulinda Muungano ila kuna marekebisho kidogo kwenye Bunge!
Swala la serikali mbili kama anavyopendekeza Profesa bado litakuwa ni tatizo hasa kwa Zanzibar ambayo siku zote inasema muundo huo unaibana. Mimi nadhani serikali (dola) mbili ni sawa ila ziwe Tanganyika - au labda kwa kuwa Tanganyika haipendezi masikioni mwa wengi - Azania/Dar es Salaam/Rubia na Zanzibar. Kwa vyovyote vile kuweko Serikali ya Tanganyka iliyojibandika jina la Muungano haiingii akilini mwangu-au kwa lugha rahisi - Tanganyika kwa jina lolote lile lazima ionekane dhahiri bila kutumia mwenge/tochi/kuruzi.
 
Kwa nini tusitengane ili wote tuingie EA kivyake?? Kwani ni lazima Bara waungane na Visiwani ndo wajiunge na EA?
 
huyu mzee shivji ameichambua rasimu ya katiba leo kuhusu muundo wa serikali tatu na mengine mengi...huyu mzee angekuwa kwenye tume ya katiba angetoa ushauri mzuri na kwa upande mwingine uwenda angeweza shirikiana na wajumbe wenzake kutupatia katiba nzuri zaidi
Ni mkweli na anajua nn anafanya hii serikali hawezi kumpenda mtu kama yy
 
Back
Top Bottom