Mhe Rais wakati unakabidhiwa nchi hii na aliyekutangulia nchi hii ilikuwa moja,katiba ya zanzibar ilitambua zanzibar kama sehemu ya jamuhuri ya muungano wa tanzania.
Wewe ulipoingia madarakani ukaruhusu nchi mpya kuzaliwa ndani ya Jamuhuri ya muungano,pale zanzibar ilipobadili katiba na kujiita nchi.Haya yalifanyika bila ridhaa ya wananchi wote wa jamuhuri ya muungano.kwa hilo ninapokuita kuwa umeihujumu jamuhuri nakusimanga au ni ukweli ulio wazi?.
Mhe Rais unatambua vyema kabisa kuwa hata mwasisi wa Taifa hili alijenga nchi moja,yenye serikali inayotambulika kimataifa moja na ile ya zanzibar kwa ajili ya zanzibar pekee. kwa maana hiyo Nyerere alijenga umoja. sasa unapoanzisha nchi ndani ya nchi tukueleweje?umekusudia kuligawa taifa vipande vipande?.
Mhe Rais pamoja na kuihujumu jamuhuri hukutosheka nalo ukaona hujuma uipeleke mpaka ndani ya chama chako cha ccm ambacho kimekupa uenyekiti, Mhe Rais unaposhiriki vikao na kuwa na msimamo ya serikali mbili ndani ya nchi mbili unakuwa na maana gani?Mwasisi wa chama chako na Taifa hili alipotoa msimamo wa serikal mbili kulikuwa na nchi moja,ila wewe unachanganya vichwa wanachama wako kuwaamba wakubali mfumo usio kuwepo tangu awali.