Kwa nini Rais Kikwete umeamua kuihujumu Jamuhuri ya Muungano?

Kwa nini Rais Kikwete umeamua kuihujumu Jamuhuri ya Muungano?

Tuna mlaumu mzee wa watu bure,huu Muungano ulikuwa unashida nyingi na kunakundi hasa Zanzibar nikama walilazimishwa kuwa humu,katika tawala zote ilitumika nguzu kubwa kuyaficha haya hata ikiwemo watu kwenda uhamishoni au kuuwawa lakini Kikwete kwakuwa nimuuni wa uwazi akakubari kila mmoja atoe dukuduku lake katika utawala wake,kwanza ndo raisi wa kwanza kukiri nyufa katika muungano nakutumia kila namna kulikabiri hili..

kulikuwa na kero ni kweli. unapotatua tatizo unatakiwa kutoa best solution sio just solution. ukiwa na watoto watatu na mkate mmoja alafu mtoto mmoja akalilia mkate wote kutatua tatizo ukampa mkate wote wale wengine wasio lia wakabaki na njaa sidhani kama hiyo ni best solution.
Muungano huu wazanzibar wameukuta,wengi unaoskia hawautaki hawana sababu mama zaidi ya za kitoto kuwa atapata ubalozi maana wasomi wachache znz.kama kiongozi lazima kuangalia best solution.
 
Nyerere alikuwa anajua na alisema kuwa wananchi wa tanzania ni masikini sana,sio Tanganyika wala zanzibar wote. kwa mtu anayeelewa maisha ya vijijini tanganyika atakubali kuwa maisha ya vijijini zanzibar yana walau kauafadhali ingawa nayo mabaya.maana kote kuna fikika kwa lami ,umeme kote umefika.ila mwanadamu haridhiki serikali imeshusha kodi ya mizigo inayoingia znz ili kuboresha maisha yao mpaka kufikia watanganyika kuacha bandari yao kwenda kushishia mizigo huko, serikali haichaji kodi vyakula vinavyoenda visiwani tokea bara ili kuboresha maisha lakini yote hayo hawatosheki sasa ilitakwa kiongozi mwenye kutoa kauli nzito za kuwanyamazisha.
 
Mtu anayeelewa maana ya upamoja na muungano hawezi kuwa na sera za umimi ubinafsi, tunapokuwa na taifa moja kubwa mwananchi anakuwa huru na wigo mpana wa kiuchumi.

Mimi nakubaliana nawe kuhusu swala la upamoja na muungano, lakini muungano huo unapaswa kuwa wa haki na wenye kuheshimu wanahisa/wahusika jambo ambalo kwa muungano huu Tanzania Bara/Tanganyika inakula keki kana kwamba ni yake pekee na kuifanya Zanzibar ni ya kufikiriwa tu. Inapofika hapo ile dhana ya upamoja na faida zake inakuwa haipo tena. Kuna haja ya kuuondoa uruhani wa Tanganyika ili ionekane wazi na kwa hili baadhi wa Watanzania Bara/Watanganyika hawalitaki kwani kwao Zanzibar kufurukuta ni dhambi/haistahiki. Hili lazima lirekebishwe
 
Tanzania haiinyimi zanzibar kufurukuta au kuneemeka kiuchumi,msaada mingi inaingia zanzibar mbona toka mataifa ya nje?Hao mawaziri na rais wa zanzibar mbona wenyewe wana sema mambo shwari. kuna mwekezaji katika kujenga viwanda zanzibar akazuiliwa na Tanzania?
miradi mingi ya UN mbona iko zanzibar,mbona oman wanasaidia zanzibar muda hawajanyimwa na Tanzania. kitu pekee ninachojua ni OIC ambayo imeruhusiwa kwa majirani zetu kama uganda lakini hamna kimya hali ya maisha ile ile tu .ni kama islamic bank mtu anaweza kuwa analia miaka 20 tukiwa na islamic bank watu tutainuka kiuchumi haya sasa nbc mwaka wa 5 wameanzisha,PBZ mwaka wa tatu wameanzisha watu waende sasa wakachukue pesa wafanye biashara si haina riba,mbona hali ya maisha iko vile vile tu.watu wanalalama bila kujua wanalalama nini.
 
Tusiwe na akili za mgando au mgando wa akili wa kufanya kila kitu as Business as Usual. watu wasasa wanatafakari na kujiamulia ustakabali ya maisha yao na nihaki yao ilimradi wanafuata katiba za nchi. Mbona hata Scotland wanataka kujitenga na Uingereza? hawa nao unawasemea nini?

Inatbidi kufanya Muungano wa kuridhiana sio kulzamishana na tusielewane vibaya kwamba hatuutaki muungano bali tuujadili na kuridhiana.
 
Tanzania haiinyimi zanzibar kufurukuta au kuneemeka kiuchumi,msaada mingi inaingia zanzibar mbona toka mataifa ya nje?Hao mawaziri na rais wa zanzibar mbona wenyewe wana sema mambo shwari. kuna mwekezaji katika kujenga viwanda zanzibar akazuiliwa na Tanzania?
miradi mingi ya UN mbona iko zanzibar,mbona oman wanasaidia zanzibar muda hawajanyimwa na Tanzania. kitu pekee ninachojua ni OIC ambayo imeruhusiwa kwa majirani zetu kama uganda lakini hamna kimya hali ya maisha ile ile tu .ni kama islamic bank mtu anaweza kuwa analia miaka 20 tukiwa na islamic bank watu tutainuka kiuchumi haya sasa nbc mwaka wa 5 wameanzisha,PBZ mwaka wa tatu wameanzisha watu waende sasa wakachukue pesa wafanye biashara si haina riba,mbona hali ya maisha iko vile vile tu.watu wanalalama bila kujua wanalalama nini.

Nilposema "kula keki peke yake" nilikuwa namaanisha Tanganyika kuchukua fursa kama kwamba ni yeye pekee mwenye haki hiyo katika Muungano. Hebu niambie kuna wafanyakazi wangapi katika balozi za TZ nchi za nje ambao ni Wazanzibari? Wangapi katika wizara za Mambo ya ndani, ulinzi nk. Mwaka jana tu ilikubaliwa Zanzibar ipate asilimia ishirini na tano ya ajira za Muungano hakuna hata mmoja aliajiriwa. Sikwambii nafasi za juu katika taasisi za Muungano kama vile jeshi na polisi. Inapokuja swala la misaada hapo ndiyo balaa kwani misaada yote ni lazima kwanza mawaziri wa Bara wakubali ndiyo Zanzibar ifaidike jambo ambalo hufanyika kwa nadra. Kuhusu kuendelea kwa umaskini licha ya kuanzishwa benki za kiislamu nadhani hilo linahitaji kuangaliwa kwa upana wake. Haakuna mahala watu hutajirika moja kwa moja (automatically) kwa sababu tu kuna benki zinatoa mikopo.
 
unaposema mawaziri wa bara nashindwa kukuelewa maana kama wizara ya ulinzi juzi ilikuwa chini ya waziri mzanzibar Nahodha, sasa yuko mzanzibar mwinyi sasa nashindwa kuelewa. sifa za uwaziri ni utanzania sio uzanzibar.
 
Back
Top Bottom