Kwa nini Sepp Blatter kaungwa mkono na nchi maskini?

Kwa nini Sepp Blatter kaungwa mkono na nchi maskini?

Ambiente Guru

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Posts
2,605
Reaction score
1,085
Licha ya kulitumbukiza shirikisho la Fifa kwenye kashfa ya rushwa. Blatter anaungwa mkono na nchi maskini za Asia, Amerka kusini na Afrika. hii inaashiria nini?

Tofauti, nchi tajiri za bara la Ulaya, Marekani pamoja na makampuni tajiri ya Cocacola na Adidas wamekaa mbali naye. Nao Viongozi wa nchi Tajiri km Uingereza, Marekana na Umoja wa Mataifa wanataka aondoke.
 
Licha ya kulitumbukiza shirikisho la Fifa kwenye kashfa ya rushwa. Blatter anaungwa mkono na nchi maskini za Asia, Amerka kusini na Afrika. hii inaashiria nini?
Njaa na kupenda rushwa
Ndo maana mtashinda uchaguzi lakini mtashindwa kimpira na hao Europe,America na Australia
Yaani in short "Fitna"
 
Mkuu, kwa kuwa FIFA kuna utaratibu wa kulindana na vyama vya nchi na mashirikisho ya kanda. Sisi hatuungi mkono, ila Rais wa FA yetu ndio anaunga mkono na uamuzi wake ndio wetu!
 
Mkuu, kwa kuwa FIFA kuna utaratibu wa kulindana na vyama vya nchi na mashirikisho ya kanda. Sisi hatuungi mkono, ila Rais wa FA yetu ndio anaunga mkono na uamuzi wake ndio wetu!
Tukubalitu kwamba umaskini ni ugonjwa, ni upofu.
 
Anaungwa mkono kule gozi la ng'ombe linakopendwa,Marekani na mpira wapi na wapi bhana..
 
Licha ya kulitumbukiza shirikisho la Fifa kwenye kashfa ya rushwa. Blatter anaungwa mkono na nchi maskini za Asia, Amerka kusini na Afrika. hii inaashiria nini?

Tofauti, nchi tajiri za bara la Ulaya, Marekani pamoja na makampuni tajiri ya Cocacola na Adidas wamekaa mbali naye. Nao Viongozi wa nchi Tajiri km Uingereza, Marekana na Umoja wa Mataifa wanataka aondoke.

Kwakuwa anawatumia marais wa vyama vya mpira vya afrika wanafaidika na uongozi wake kwakuwa wanakuwa na uwezo wa kutumia pesa wanazopata kutoka fifa moja kwa moja jambo ambalo mpizani wake alitaka kulibadili
 
Mkuu, kwa kuwa FIFA ........ Sisi hatuungi mkono, ila Rais wa FA yetu ndio anaunga mkono na uamuzi wake ndio wetu!
Kila kurahununuliwa kwa pesa nyingi. ukipiga mara moja umaskini unasahau. Huu ni mwanzo natutaanikiwa mengi mbele ya siku Mkuu. .
 
Uingereza kukosa kuandaa kombe la dunia 2018 ndo majanga yote hayo Blatter anayoyapata..chezea nchi ya malkia wewe...hayo makampuni ya Coca cola na adidas ni yanapigishwa ngoma na UK...usichezee watawala wa dunia hii...
 
Inawezekana Sepp Blatter a.k.a Sefu Abdallah akawa na matatizo lakini shida hii imeongezwa na hasira za Uingereza na Marekani kunyimwa uenyeji wa fainali za kombe la dunia 2018 & 2022.. Ukweli mchungu ambao hata Blatter mwenyewe amewaambia ni kwamba kama wangepata uenyeji kusingekuwa na storm hii ya leo..

Kipinda cha uongozi wa Blatter ni wa neema kwa nchi zinazoendelea.. Kama kweli tungekuwa na viongozi wanaojua kuongoza soka na wenye vision basi tungekuwa mbali sana.. Kwa miaka kadhaa TFF ilikuwa inapata gawio la dola laki 250 kila mwaka toka FIFA.. Walipewa upendeleo wa aina mbali mbali ikiwa na kuletewa wataalam kwa ajili ya mafunzo mbali mbali..

Bahati mbaya kwa wazungu wa Ulaya Blatter anatazamiwa kupita soon japo raisi wa UEFA ametishia kuitoa Ulaya FIFA..
 
Uongozi wake umekuwa Baraka kwa nchi masikini na hawababaikii nchi zinazojiona kwamba zinastahili kila kitu hususan Europa.....

Amefanya pesa nyingi ziwe channelled kwenye grassroot football hususan nchi masikini, na mfumo wa kufanya kombe la dunia kuwa zamu zamu kwa mabara kumefanya Africa na Asia nao kupata faida hii tofauti na kabla.. pia Africa kuwa na Timu tano kwenye World Cup kumekuja on his watch...(in short Zimwi likujualo hatujui kama akija kiongozi mwingine anaweza akawa anajipendekeza kwa Europe .... ukizingatia hawa ndio hawampendi kwa sasa)

By the way where there is money there is crime ....., Rushwa Fifa imekuwepo tangu enzi na enzi some call it lobbying...
 
Licha ya kulitumbukiza shirikisho la Fifa kwenye kashfa ya rushwa. Blatter anaungwa mkono na nchi maskini za Asia, Amerka kusini na Afrika. hii inaashiria nini?

Tofauti, nchi tajiri za bara la Ulaya, Marekani pamoja na makampuni tajiri ya Cocacola na Adidas wamekaa mbali naye. Nao Viongozi wa nchi Tajiri km Uingereza, Marekana na Umoja wa Mataifa wanataka aondoke.
Hayo mataifa tajiri wanachotaka ni kujitajirisha kupitia FIFA na ni aina ya unyonyaji unaoendelezwa kwa nchi masikini! ukiangalia vipaji vya soccer asilimia 95% vinatoka inchi masikini lakini wanalazimishwa kuvifanyia kazi vipaji vyao katika nchi matajiri ili walipe kodi na hata kuzitangaza hizo nchi chache matajiri! jaribu tu kuangalia ikiwa uingereza kutakuwa hakuna hata mchezaji mmoja kutoka hizo nchi masikini hilo soccer litakuwa soccer au jezi tu! Blatter anaplan nzuri ya usawa katika mchezo huu sasa hawa mabepari hawataki kuona nchi masikini zinapata fursa ya ku handle shughuli za Soccer vizuri maana baada ya mafuta soccer ndio inafuata kwa kuingiza fedha!
 
Back
Top Bottom