Kwa nini Simba na Yanga zisianzishe Foundations zao wenyewe badala ya kutegemea Mo na GSM Foundation?

Kwa nini Simba na Yanga zisianzishe Foundations zao wenyewe badala ya kutegemea Mo na GSM Foundation?

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Kwa muda mrefu, vilabu vya Simba na Yanga vimefungamana na Mo Foundation na GSM Foundation katika shughuli za kutoa misaada kwa jamii.

Sina uhakika kama kuna mtu amekaa akawaza ni kwa nini hivi vilabu vimeunganana na taasisi hizi badala ya kuanzisha taasisi zao za kutoa kwa jamii.

Hivi vilabu vinapokwenda katika vituo vya watoto yatima vinatoa msaada ambao kwa makadirio ya gharama za haraka ni 500,000. Tuchukulie wanafanya hivyo mara moja kwa mwezi, kwa mwaka hiyo ni takribani milioni 6. Jiulize hizi timu hazina milioni 6 ya kutenga kwa shughuli hizi kwa msaada wa mwaka mzima?

Pia jiulize, nani hasa kati ya klabu na Foundation anagharamia hizi shughuli au wanatoa 50/50?

Nadhani imefika wakati hivi vilabu vianzishe foundations zao wenyewe. Waanze kidogo kidogo pale wanapoweza na washirikiane na foundations zingine pale wanapohitaji kuongeza nguvu kutoa msaada mkubwa zaidi.

Kuendelea kutegemea Foundations za wengine kwa asilimia 100 ni kujilemaza na kutotaka kukua.
 
Back
Top Bottom